Ni wakati wa kila Jimbo kuwa na Mamlaka kamili ya Kikodi

Feb 18, 2019
50
532
Wanasiasa msituchezee. Hii sio Tanzania ya mwaka 80. Kama mlikuwa hamjui huu ni mwaka 2020 na tumeingia muongo mpya. Tanzania sio mali yenu ni mali ya wananchi. Kwenye uchaguzi nyote ni sawa na tutawachagua kulingana na mtakavyofaulu interview zenu.

Wanasiasa mnajisahau sana. Mnajisahau sisi ndio tunawaweka hapo mlipo. Pesa za kuendeshea nchi tunazitoa sisi. Maendeleo mnayojidai kuyaleta ni kwa ajili yetu sisi. Kila kitu ni kwa ajili yetu sisi.

Sasa iweje leo hii unakuja mbele zetu eti unatupangia watu wa kuwachagua? Eti msipomchagua fulani basi mtajuta miaka 5 mbele, like seriously? Unadhani hata usipojenga hivyo vi-miundombinu vyako jimboni kwetu ndio tutarudi nyuma kimaendeleo?

Unadhani jimbo letu ni locked? Kwani tukiona mambo magumu si tunahamia kule unakoelekeza malisho? Hivi we mgombea ushawahi kujiuliza kwa nini Dar inaongoza kwa watu wengi lakini walio wengi ni wahamiaji? Au utaweka sheria ya kila mtu arudi alikozaliwa?

Wewe umekuja kuomba kura za urais iweje uingilie mambo ya ubunge/udiwani. Jinadi wewe kama rais utatufanyia nini kisha nenda zako. Mambo ya ubunge na udiwani tuachie sisi ndio tunajua tunamuamini nani ambaye atasimama na sisi hata ww ukimuamrisha fyongo. Usitupangie watu ambao mwisho wa siku watakusikiliza wewe tuu pasipo kutusikiliza sisi.

Kwa matamshi yako haya itoshe tuu kusema ni muda muafaka wa mapato ya halmashauri zooote kuwa decentralized ili kila jimbo/halmashauri/mkoa kula kulingana na urefu wa kamba yake na serikali kuu ipelekewe % yake. Hii ya mapato yooote kwenda hazina kisha wao ndio waanze kugawa mafungu haikubaliki sababu ushasema wazi watakaochagua vyama tofauti na wewe watajuta miaka 5.

Haya ni mawazo na maneno ya mgombea ambaye ni UNFIT kwa position kama hiyo yako.

TOTALY UNFIT.
 
Siku hili jambo likiwekwa kikatiba,na kila halmashauri ikawa na autonomy maendeleo tutayapata ndani ya muda mchache sana
Naye JPM asome alama ya nyakati,ipo siku kama siyo chini yake basi kuna awamu hiki unachokililia kitatimia
 
Hapana mimi nafikiria kodi aendelee kutushikia JPM na kuzitumia aonavyo yeye inafaa!
JPM #tano tena 😂😂😂
 
Back
Top Bottom