Uchaguzi 2020 Ni wakati muafaka wa kufanyika midahalo kwa Wagombea wa Uraisi !

kambiyamkaa

Senior Member
Aug 9, 2020
122
110
Niwaombe Sana Wasome kutoka Vyuo mbalimbali hapa Nchini , Wanaharakati , Na Wadau wote wa Maendeleo Na wanaoitakia Maendeleo zaidi Nchi yetu kwamba , huu Ni wakati muafaka wa kumfahamu kila Mgombea hususani hii ya Rais !

Ninaonavyo Mimi , Ni muhimu Sana , Sana ukaandaliwa Mdahalo Na Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali ( NGO's ) mbalimbali kwa Wagombea wa nafasi hii ya Urais angalau Mara mbili Mara tu baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kukamilisha kazi ya Uteuzi tarehe 25 August mwaka huu !

Watanzania tuna haki ya kuwajua Wagombea kwa undani ili tufanye Maamuzi sahihi ya kumpigia Kura Mgombea sahihi , Na hatimaye tumpate Rais ambaye kweli atakuwa Ni Chaguo la Watanzania !

Hatutaki kuchezewa safari hii ! Kwa mara ya kwanza na ya mwisho kama nakumbuka vizuri , mdahalo wa Wagombea Urais ulifanyika mwaka 1995 wakati wa Uchaguzi wa kwanza wa Vyama vingi . Tokea wakati huo , Chaguzi zilizofuata , Wagombea wamekuwa wakiikwepa Midahalo!Na hata wengine kuibeza miongoni mwa Presidential Candidates !

Mwaka 2010 , Kituo cha television cha TBC kinachomilikiwa na Shirika la Utangazaji la Taifa ( Shirika la Umma ) Shirika letu sote Watanzania, Shirika lilianzisha mdahalo kwa Wagombea Ubunge . Huwezi kuamini , ghafla midahalo hiyo ilifutwa ! You can not believe !

Chama za Mapinduzi kiliwazuia haraka Sana Na kutoa agizo zito kwamba wanachama wake ( wagombea ubunge ) , Ni marufuku kushiriki midahalo hiyo ! Uamuzi ule wa TBC kusitisha midahalo ile kwa kweli binafsi niliumia Sana , Sana !

Ni kuwanyima fursa wapiga Kura kuwajua wagombea Na kuwapima Na pia kuwanyima fursa Wagombea kuulezea Umma Sera zao pamoja na Mikakati huku wakisiliza changamoto kutoka kwa wapinzani Wao . Ili Uchaguzi uweze kuwa huru Na haki , Ni lazima wapigakura wawaelewe vizuri Wagombea Wao , Sera na ilani za vyama vyao ili tunapofanya uamuzi tarehe 28 October wa kumchagua mgombea mmoja , tufanye kwa usahihi badala ya kufanya maamuzi ya kishabiki !

Ni hatari Sana kufanya maamuzi ya kishabiki ! Narudia tena kwa Msisitizo Sana , kuyaomba mashirika yasiyo ya Kiserikali , na hata TBC Shirika la Umma , nanyi pia bado mnaweza kuandaa Midahalo hii !

Nikuombe Mkurugenzi wa TBC , asiogope . Midahalo inajenga na bila shaka tutawapata Wabunge Wazuri na Rais ambaye kweli atakuwa Ni chaguo la Watanzania .

Vyama pia vya Siasa , niviombe Sana vitoe Ushirikiano utakaohitajika na Mashirika hayo ili kufanikisha azma hii muhimu kwa mustakabali wa Taifa letu .

Naamini na mtakuwa pamoja nami kwamba , kwa yeyote Mgombea atakayekwepa Midahalo hiyo ,
 
Dunia ingependa na kufurahia huo mdaharo na kwa umuhimu huo basi mdaharo ufanyike kwa kiingereza.
 
Ni wakati muafaka Sasa kwa TBC kwa kushirikiana Na NGO's kuandaa Midahalo kwa Wagombea wa Uraisi ! Muda umetutupa mkono ! Ni muda muafaka wa kusikiliza Sera Na Mikakati ya kila Mgombea anatuambia nini ! Na anatupeleka mbele Na kututoa hapa tulipo .
 
Back
Top Bottom