UMEKOMBOLEWA? INA MAANA GANI KUKOMBOLEWA?[emoji848]
Na Pastor Felician Makarios
Wakati mwingi tunaimba tumekombolewa na Yesu halafu hatukai katika kina cha maana ya maneno hayo. Tunaimba au kutamka tu kama kasuku.
Imekua kawaida katika jamii ya Kikristo, kusema tu maneno ya kidini hata kama hatuamini tunachosema au hatuelewi tunachosema.
Neno "ukombozi" linarejea gharama iliyolipwa, hiyo gharama ni thamani ya mtu.
1Timotheo 2:5 Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu; 6 ambaye alijitoa mwenyewe kuwa ukombozi kwa ajili ya wote, utakaoshuhudiwa kwa majira yake.
Neno "ukombozi" limetafsiriwa kutoka katika neno la kigiriki 'lutron' linalomaanisha gharama iliyolipwa.
Kwa hiyo Paulo anasema Yesu alijitoa kua gharama inayolipwa
Mathayo 26:28 kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.
Damu ya Yesu (maisha ya Yesu) ndiyo gharama iliyolipwa kwaajili ya dhambi.
Tazama hapa,
Luka 22:20 Kikombe nacho vivyo hivyo baada ya kula; akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu.]
Hapa tena,
Warumi 3:23 kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; 24 wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu; 25 ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake,ili aonyeshe haki yake ,kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili wa MUNGU dhambi zote zilzotangulia kufanywa.
Damu ya Yesu ndiyo gharama iliyolipwa, ni bure, na ni katika Kristo. Hakuna gharama nyingine inayohitajika kwa ajili ya ukombozi.
Angalia hapa, nani aliyenunua;
Matendo 20:28 Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe.
Hapa tena;
Wagalatia 3:13 Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti;
Kwa kifo chake, alitukomboa kutoka katika dhambi.
Ni kazi ya Kristo, siyo kazi yetu. Ni yeye mwenye kufanya ukombozi.
Angalia hapa;
Tito 2:14 ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema.
Tumekombolewa na maasi yote, tumesafishwa kuwa miliki yake na ndipo tuna juhudi katika kutenda mema.
Si kwa matendo ya haki tuliyotenda;
Tito 3:4 Lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu, na upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa,alituokoa; 5 si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu; 6 ambaye alitumwagia kwa wingi, kwa njia ya Yesu Kristo Mwokozi wetu; 7 ili tukihesabiwa haki kwa neema yake, tupate kufanywa warithi wa uzima wa milele, kama lilivyo tumaini letu.
Gharama ililipwa kwa niaba yetu.
1Wakorintho 6:19 Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; 20 maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.
Hapa tena;
1Wakorintho 7:23 Mlinunuliwa kwa thamani; msiwe watumwa wa wanadamu.
Hivyo, tulinunuliwa kwa gharama iliyolipwa, kwahiyo ukombozi wetu ni katika Kristo.
Hivyo tunao ukombozi, siyo tutakua na ukombozi; ni sasa, tunamiliki ukombozi.
Waefeso 1:7 Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake.
Neema maana yake ni kwamba ilitolewa bure, na msamaha wa dhambi unapatikana kwa sababu ya wingi wa neema yake.
Wakolosai 1:12 mkimshukuru Baba, aliyewastahilisha kupokea sehemu ya urithi wa watakatifu katika nuru. 13 Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake; 14 ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi;
Katika ukombozi, tuna masamaha ya dhambi. Mungu hakuomba badiliko la moyo kutoka kwetu kabla hajatusamehe; ilitolewa kwetu kwa msingi wa kile ambacho Kristo amefanya.
Hapahitaji kujitutumua, ni kazi yake. Ni neema yake kwetu.
Waebrania 9:11 Lakini Kristo akiisha kuja, aliye kuhani mkuu wa mambo mema yatakayokuwapo, kwa hema iliyo kubwa na kamilifu zaidi, isiyofanyika kwa mikono, maana yake, isiyo ya ulimwengu huu, 12 wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika Patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele.
Alipata ukombozi wa milele kwaajili yetu kwa damu yake! Huku ndiko kuachiliwa kabisa kutoka kwenye dhambi.
Mwamini hayupo tena katika dhambi, ameachiliwa kabisa, amekombolewa milele.
Kumbuka kwamba Wokovu una msingi katika kweli tatu; kifo cha Yesu, kuzikwa kwake, ufufuo wa Yesu katika mwili na kwasababu hiyo kupaa kwake.
1Wakorintho 15:17 Na kama Kristo hakufufuka, imani yenu ni bure; mngalimo katika dhambi zenu.
Maana kuwepo kwa dhambi kunategemea kutofufuka kwa Yesu. Ikiwa alifufuka basi imani yetu siyo bure na tayari tuna msamaha wa dhambi, hatumo dhambini tena.
Ufufuo wa Yesu ni ushahidi kwamba gharama imelipwa kwaajili ya dhambi. Ufufuo wa Yesu unathibitisha kazi ya ukombozi. Inaweka muhuri wa mwisho kabisa na inatoa uhakika wa wokovu wa milele kwa mwamini.
Angalia hapa;
Waebrania 5:9 naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya
wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii;
Wanaomtii katika matumizi ya mwandishi wa Waebrania inarejea “wanaomwamini”. Kuamini ndiko kutii.
Wokovu huo, unaitwa wa milele. na Kristo ndiye anayeutunza. UKOMBOZI WA MILELE
Siyo wewe unayetunza, hapana. Ni mkombozi anayetunza ukombozi wa aliyekombolewa.
Angalia mstari huu.
Waebrania 7:22 basi kwa kadiri hii Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi...., 25 Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee.
Mwandishi anasema anaweza kuwaokoa kabisa, ni muhimu kuzingatia hili
Neno kabisa ni neno milele katika andiko hilo. Hiyo inamaanisha kwamba Yesu anaokoa milele kwa sababu amefufuka na yu hai hivi leo. Yaani Yesu haokoi kwa mwaka mmoja, hapana, anaokoa kwa milele.
1Yohana 2:1 Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki, 2 naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote.
Yeye ndiye mtetezi wetu mbele za Baba. Hivyo, hatuhukumiwi kwa dhambi tena.
Uwepo wake mbele za Baba siku zote ndiyo utetezi wetu na ndiyo hakikisho la usalama wa kile tumepokea katika Yeye, kwa kua yuko hai milele na sisi tuko hai milele. Dhambi haina nguvu tena, tuna huduma yake ya ukuhani kwa ajili yetu milele.
Warumi 8:1 Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.
Mwamini yuko huru kutoka katika hukumu. Hakuna ina maana ya hakuna, usiweke “lakini”, hiyo inatoka kwa adui.
Waebrania 8:8 Maana, awalaumupo, asema Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, Nami nitawatimizia nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda agano jipya; 9 Halitakuwa kama agano lile nililoagana na baba zao, Katika siku ile nilipowashika mikono yao niwatoe katika nchi ya Misri. Kwa sababu hawakudumu katika agano langu, Mimi nami sikuwajali asema Bwana. 10 Maana hili ndilo agano nitakaloagana na nyumba ya Israeli Baada ya siku zile, asema Bwana; Nitawapa sheria zangu katika nia zao, Na katika mioyo yao nitaziandika; Nami nitakuwa Mungu kwao, Nao watakuwa watu wangu. 11 Nao hawatafundishana kila mtu na jirani yake, Na kila mtu na ndugu yake, akisema, Mjue Bwana; Kwa maana wote watanijua, Tangu mdogo wao hata mkubwa wao. 12 Kwa sababu nitawasamehe maovu yao, Na dhambi zao sitazikumbuka tena.
Hakuna kumbukumbu ya dhambi katika wokovu, Mungu hashikilii dhambi kwa mwamini.
Angalia hapa tena;
Waebrania 10:17 Dhambi zao na uasi wao sitaukumbuka tena kabisa.
Wewe kwa nini unakumbuka dhambi zako? Yeye hakumbuki tena.
Unyenyekevu ni kukubali kile Mungu anasema kwako, hakumbuki! Usitake kuanza kukumbusha!
Katika uzao mpya, tuna zawadi ya kutokuwa na hukumu.
Waebrania 10:12 Lakini huyu, alipokwisha kutoa kwa ajili ya dhambi dhabihu moja idumuyo hata milele, aliketi mkono wa kuume wa Mungu; 13 tangu hapo akingojea hata adui zake wawekwe kuwa chini ya miguu yake. 14 Maana kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa.
Chote ambacho Kristo amefanya, amekifanya milele na ameketi mkono wa kuumne wa Mungu.
Yesu hakufanya kazi ya siku mbili au ya kujirudia rudia.
Waebrania 13:5 Msiwe na tabia ya kupenda fedha; mwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa.
Tazama sentensi, "sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa", inaonyesha kujitoa. Ni maneno ya uhakika (absolute words), ni ahadi yake na kujifunga kwake HATAKUACHA KAMWE!
Isitokee wakati wowote ukajiskia au kuona umeachwa, hawezi kukuacha kwa sababu yeyote ile. Kuwepo kwake pamoja na wewe kunategemea alichofanya Kristo na sio unachotenda wewe.
Waebrania 12:22 Bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi, 23 mkutano mkuu na kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika,
Umefika hauko safarini kuelekea. Wokovu wako au ukombozi wako ni halisi leo.
Waebrania 9:11 Lakini Kristo akiisha kuja, aliye kuhani mkuu wa mambo mema yatakayokuwapo, kwa hema iliyo kubwa na kamilifu zaidi, isiyofanyika kwa mikono, maana yake, isiyo ya ulimwengu huu, 12 wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika Patakatifu,
akiisha kupata ukombozi wa milele.
Gharama aliyolipa ni mara moja na milele. Halipi kila siku, hakusamehi kila siku. Umelipiwa milele, umesamehewe milele. Unyenyekevu ni kukubali neno lake. Acha kubishana naye, anasema amepata ukombozi wa milele.
Waebrania 9:15 Na kwa sababu hii ni mjumbe wa agano jipya, ili, mauti ikiisha kufanyika kwa kukomboa makosa yaliyokuwa chini ya agano la kwanza, hao walioitwa waipokee ahadi ya urithi wa milele.
Millele ni kinyume cha “ya muda tu”. Inamaanisha milele, kinachodumu. Wale waliomwamini Kristo wamepokea urithi wa milele kwa dhabihu ya Yesu ya mara moja kwa milele.
Utakua na maana sana ukikubaliana na neno lake ukaachana na stori za mtaani.
1Wathesalonike 5:23 Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo. 24 Yeye ni mwaminifu ambaye awaita, naye atafanya.
Haya hayakuwa maombi kwakuwa Paulo hakuwa anaomba kwasababu hatuombi kwaajili ya utakaso, ni kazi ya Mungu. Lakini Paulo alikua anasisitiza uaminifu wa Mungu hapa, anatuweka wakamilifu, watakatifu na salama. Anafanya hivyo kwa sababu YEYE NI MWAMINIFU.
Katika Injili nne, Bwana wetu Yesu alifundisha kweli iyo hiyo.
Yohana 5:24 Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani.
Mwamini hatahukumiwa. Amevuka mautini au hukumuni na ameingia uzimani.
Huu ndiyo uzima wa milele; kupita kutoka kifo cha kiroho kuingia uzimani, hii ilifanyika katika ufufuo, katika ukombozi. Ni kazi ya uhakika.
Yohana 10:28 Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu.
[emoji123]Yesu anatoa senstensi ya uhakika na ya kibabe hapa "hakuna mtu". Hivyo hakuna kitu, ikiwamo shetani kinaweza kutuchukua mbali kutoka katika wokovu wetu. Hii ni Jumla na kamili kiasi kwamba kila mwamini anapaswa authibitishe ufahamu wake. Mwamini amesalimishwa milele katika Kristo.
Hakuna hatari ya kupotea ama kupoteza wokovu wako. Ni yeye aliyeapa kua hutapokonywa.
Acha ushamba jubali hii, huwezi kupokonyoka hata ungetaka. Yuko na wewe milele.[emoji4]
Mathayo 28:20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
Yuko pamoja nasi hata mwisho wa dahari sio mwisho wa mwaka.
Jina la mwamini limeandikwa mbinguni.
Luka 10:20 Lakini, msifurahi kwa vile pepo wanavyowatii; bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni.
Sisi ni raia wa ufalme wa Mungu.
Waefeso 2:19 Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu.
Sisi ni washirika kabisa wa familia ya Mungu. Sisi ni raia wa mbinguni. Sio kwamba tunajipendekeza, ndivyo ametufanya.
Wafilipi 3:20 Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo;
Neno, "wenyeji" limetafsiriwa kutoka katika neno la kigiriki linalomaanisha uraia.
Hivyo wokovu wetu umepewa usalama wa milele, na hapa ndipo anaposimama mwamini, huu ndiyo uhakika wake. Huu ndiyo uhalisia wa ukombozi wetu. Simama hapo hapo, ndipo ulipo.
1Petro 1:18 Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu; 19 bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo.
Umekombolewa kwa bei ya thamani, usianze kujiona wa bei rahisi. Usianze kutumikishwa na utoaji wa vitu vya hovyo ili kupata kupatanishwa na Mungu au vipawa na baraka za Mungu.
Ufunuo 5:9 Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,
Hivyo, ukombozi wa mwamini ni katika damu ya Kristo, ni katika utu wa Yesu.
Na katika huo, tunastarehe!
Tuna amani, hakuna mashaka.
Unajisikiaje?
Fanya nijue.
Pastor Makarios
Sent from my Infinix X6816 using
JamiiForums mobile app