Urban86
JF-Expert Member
- Jan 26, 2014
- 279
- 132
Maswali ya msingi kujiuliza
1. Ni mambo gani yanatakiwa kuaminiwa ili mtu kuokoka?
2. Umeokoka? Uliamini nini?
3. Unaweza kuelezea kwa maneno rahisi nini maana ya kuokoka?
Imani katika Kristo ni KUPOKEA kutoka kwa Kristo na sio KUMPA Yesu au kutoa kwa Yesu.
“Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;”
— Yohana 1:12 (SUV)
KUAMINI SIO KUTOA BALI KUPOKEA.
Katika wokovu mtu anapokea maisha/uzima kwa imani katika injili ya Yesu Kristo pekee.
“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.”
— Yoh 3:16 (SUV)
Yeye(MUNGU Baba) alitoa uzima na sisi tunaupokea. Sisi ni kazi ya mikono yake tu.
Ef 2 (SUV)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁸ Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;
⁹ wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.
¹⁰ Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.
Wokovu hautokani na sisi, sio kwa kupenda kwetu, sio kwa kustahili kwetu, sio kwa matendo yetu bali kwa neema ya bure ya Mungu.
“Akasema, Kwa sababu hiyo nimewaambia ya kwamba hakuna mtu awezaye kuja kwangu isipokuwa amejaliwa na Baba yangu.”
— Yoh 6:65 (SUV)
Mtu ambaye bado hajaokoka hana kitu cha kutoa. Sote tulikuwa tumekufa katika dhambi zetu na makosa yetu, hatukuwa na maisha ya kutoa.
“Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu;”
— Ef 2:1 (SUV)
Hii ndio maana ya wokovu --MUNGU ndiye mtoaji na sisi ni wapokeaji.
“Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye?”
— Rum 8:32 (SUV)
Matendo yetu yote yalikuwa kupokea kile ambacho Mungu alitoa. Mwitikio wetu ulikuwa kuamini tu.
Hatukutoa maisha yetu ili tuokolewe. Badala yake tulipokea maisha yake na tukaokolewa.
Hivyo wokovu sio KUBADILISHANA MAISHA ILA MAISHA MAPYA KUTOKA MAUTINI KWENDA UZIMANI.
“Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani.”
— Yoh 5:24 (SUV)
“Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.”
— Rum 8:2 (SUV)
Hivyo haiwezekani kwa mwamini kukosa kile Mungu alikwisha kutoa, kilichopo ni yeye(mwamini) kuja kwenye uhalisia wa kila kitu chema kilichoko ndani yake ndani ya Kristo.
IMANI KATIKA KRISTO
2Timotheo 3:15-16 (SUV)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁵ na ya kuwa tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu.
¹⁶ Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;
Wokovu ni kwa imani iliyo katika Kristo Yesu.
“Paulo, mtumwa wa Kristo Yesu, aliyeitwa kuwa mtume, na kutengwa aihubiri Injili ya Mungu;”
— Rum 1:1 (SUV)
“Sasa na atukuzwe yeye awezaye kuwafanya imara, sawasawa na injili yangu na kwa kuhubiriwa kwake Yesu Kristo, sawasawa na ufunuo wa ile siri iliyositirika tangu zamani za milele,”
— Rum 16:25 (SUV)
Kujua maandiko haina maana ya kuyakariri bali kuyaelewa kiasi cha kuweza kuyaelezea/ kuyafasiri kwa usahihi wake.
2Petro 1:16
Kuyaelewa maandiko matakatifu sio kipaji, au uwezo ambao mtu anazaliwa nao bali kwa kuyapata maarifa yaani kufundishwa, kuwa stadi/mahiri.
Ustadi/umahiri wa Timotheo ulionekana katika uwezo wake wa kufundisha maandiko matakatifu kwa usahihi.
Wokovu ambao ni kwa imani katika Kristo ni ujumbe wa maandiko matakatifu ukiwa umejikita katika utu wa Yesu Kristo.
Waamini hawatarajiwi kwa njia yoyote kuishi katika msingi wa dhahania, hisia au misemo ila katika msingi wa imani katika maandiko matakatifu.
Luka 24:25-27, 1Petr1:10-11, Rumi 1:1-4, Gal 3:6-8, Yohana 6:26-35 anza kwanza(1-25)
●Kumwamini Yeye ni kupokea uzima.
●Tofauti kati ya kupokea miujiza na kumpokea Yesu (mkate wa uzima)
●kumwamini Yeye ambaye Mungu alimtuma
●Yeye ni mkate wa uzima na yule amwaminiye Yeye hataona njaa kamwe.
●Alikuja toka mbinguni kufanya mapenzi ya Baba yake ambayo ni kuwapa uzima wale watakaomwamini.
●Aliyemwona Mwana na kumwamini anao uzima wa milele naye atamfufua siku ya mwisho.
●Atakaye mwamini Yeye anao uzima wa milele.
Yohana 6:60-66
●Imani ya uponyaji na miujiza sio sawa na imani kwa Kristo kwa wokovu. Mtu anaweza kutenda miujiza kwa jina la Yesu na asiwe mwamini.
Luka 10:1, 17, 9:49
Imani kwa Kristo kupata wokovu sio sawa na imani ya kupokea uponyaji na miujiza.
“Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.”
— Mat 7:21 (SUV)
Ni jinsi gani mtu anaingia katika ufalme wa mbinguni?
●Aliongea kuhusu kuingia mbinguni katika Yoh 3:3-5
●Kuzaliwa mara ya pili Yoh 3:16-17
●KUMWAMINI YEYE alirejea katika kuamini katika kufufuka kwake. Yoh 3:14,15,16-17
●Kuinuliwa ni ufufuo kutoka katika wafu
Mathayo 7:21
Hakusema "Yeye atakayebakia kufanya mapenzi ya Baba yangu" bali "Yeye afanye mapenzi ya Baba yangu"
Mathayo 7:22-23
Hakuwa anarejea juu ya kupoteza wokovu. (Angalia muktadha) bali kutokutii ambako ndiko kutokuamini
Mathayo 7:26, 7:24-25, 7:26-27
Yeye alikuwa akizungumzia wale ambao husikia maneno yake na wasiwe na imani kwa wokovu wake.
Watu wanaweza kupokea miujiza na hata kutoa mapepo kwa jina lake lakini wasiamini injili katika kufa na kufufuka kwake.
Yohana alimaanisha nini kwa "hawakumpokea?"
Yohana 1:12 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;
Hivyo, kumpokea kunamwamini Yeye- katika jina lake ni katika injili! Neno "kuamini" linamaanisha kuwa na imani ndani ya...
Angalia maneno "kama wengi waliompokea", sio "wengi waliopokea muujiza". Ndiyo sababu wengi waliopokea miujiza, uponyaji kutoka kwake, hawakupokea / kumwamini, kama ilivyokuwa katika Yohana 6.
Imani ya uponyaji au matendo ya nguvu/miujiza ni tofauti na imani katika Kristo iletayo uzima wa milele.
Kwamba mtu anaweza kuamini kupokea uponyaji lakini asimwamini Kristo atoaye uzima wa milele.
Sasa ni jinsi gani mtu anaokoka?
Mtume Paulo anaelezea katika Rumi 10: 8-17
Neno (ujumbe) wa imani (mstari wa 8) ni Injili (Mstari wa 16, 17), ambayo alikuwa amefafanua katika mstari wa 9 kama ufufuo wa Yesu kutoka kwa wafu.
ambayo ni nguvu ya Mungu kwa wokovu.
Hiyo tuu mtu anapoiamini anakuwa ameokoka/ kupata wokovu.
Kwa maneno mengine kama ujumbe aliohubiriwa mtu haumhusu(SIO) Yesu yaani kufufuka kwake kutoka kwa wafu ili kuhesabiwa haki kwetu, mpokeaji wa ujumbe huo mwingine HAJAOKOKA.
Hii haimjalishi mhubiri na msikiaji, kwa sababu injili pekee ndio ujumbe wenye nguvu ya kuweza kuokoa.
Imani katika Kristo ni imani katika injili ya Kristo; katika ufufuo wake. Hiyo ndiyo imani ya wokovu.