Ni vizuri tukafahamu.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni vizuri tukafahamu..

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MwanajamiiOne, Feb 17, 2010.

 1. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #1
  Feb 17, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,476
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Wadau hii nimeikuta kule kwenye Mlima wa Utajiri (The Hill of Wealth)

  Mke Mleaji:

  Mume akiwa na hitaji lolote hulitimiziwa. Mume akiwa mgonjwa ajue chicken soup hakosi.
  Anakuwekea love note kwenye bag lako la kazini au lunch yako ya kubeba kazini. Anafanya kazi zote za nyumbani kama kuosha vyombo na kufua nguo bila malalamiko.
  Pia anajua mume anachoka na kazi hivyo jambo la msingi ni kuhakikisha nyumbani kuna amani hivyo mke wa aina hii hujichosha na kazi.
  Wanawake wa aina hii huchoka sana na kutoa (give) kwa waume zao kila kitu kwa jina la amani.
  Tatizo la mke wa aina hii akiamua kugombana anagombana kwelikweli
  Mke Kama Mama:
  unamtengenezea breakfast ya nguvu mumeo asubuhi, unahakikisha unamkumbusha ratiba za mambo anatakiwa kuhudhuria.
  Unamkumbusha kumeza dawa alizopewa na daktari.
  Unapanga nguo zake za kazini kila siku.
  Unahakikisha anakula chakula tena balance diet hata kama hataki vegetables unahakikisha anakula.
  Unafanya yote hayo kuhakikisha unamtunza.
  Na wanaume wenye mke wa aina hii wakati mwingine hufurahia kwa kuwa wanaume wengi hupenda kutunzwa ingawa wakati mwingine huudhika Kutokana na tabia zao za kukefyakefya kama mama na hakuna mume anayependa kuoa mke ambaye ni kama mama yake.
  Mke ni mke na mama ni mama na haipaswi kuchanganywa.
  Tatizo la mke wa aina hii humzoesha vibaya mume kiasi kwamba anakuwa tegemezi na mke hujikuta mume amekuwa kama mtoto mwingine.
  Mke kama Binti:
  Ni mwanamke ambaye hawezi kufanya vitu mwenyewe au peke yake.
  Hawezi hata kubadilisha bulbu, hawezi hata kuwasha Computer au TV mpya kuifanya ifanye kazi.
  Kulipa bills bila msaada wa mume, hawezi kufan bank hadi mumewe awepo. Kila anachofanya anajiona hawezi hadi mumewe awepo.
  Anakuwa kama vile ni binti ambaye anahitaji directions zote kutoka kwa baba yake.
  Mke wa aina hii huvumiliwa sana mwanzo wa mahusiano hata hivyo mahusiano yanavyozidi kwenda mume hujiona ni usumbufu.
  Wanawake wa aina hii inawezekana wakati watoto walikuwa neglected na hawakupata attention kutoka kwa wazazi wao hivyo hujikuta hajiamini kila analofanya.
  Mke Bosi:
  Mke wa aina hii huweza kumpa mume orodha ya vitu anatakiwa kufanya, mume hupewa taratibu za kusaidia kazi za nyumbani. Huweza kutoa amri za nani awe rafiki wa mume wake au la. Anampa mume kikomo cha muda anatakiwa kutazama Tv au kujihusisha na masuala ya sports na rafiki zake.
  Wanawake wengi wa nchi zilizoendelea wapo kwenye kundi hili.
  Hii tabia huondoa uhuru wa mwanaume na hivyo anaweza kuwa disconnected kwani mwanaume huhisi anaondolewa heshima yake ya kuwa mwanaume (manhood and ego).
  Mke Super:
  mwanaume hafanyi kazi yoyote ya nyumbani kama kupika na kufua labda mwanaume aamue mwenyewe.
  Anahakikisha watoto wanapata kila wanachohitaji.
  Hapa haijalishi mke wa aina hii ana kazi yenye kipato kuliko mume wake au la.
  Mwanamke wa aina hii huchoshwa na kazi kiasi kwamba anakosa na usingizi.
  Pia mwanamke wa aina hii huweza kujihisi mume hana appreciation kitu ambacho kinaweza kumfanya ajisikia hana furaha na matokeo yake anaweza asiwe na mawasiliano mazuri na mume.
  Mke kila kitu ni mtoto/watoto:
  Wakati mwingine kuwa mzazi huongeza stress katika ndoa.
  Na tatizo kubwa ni kwamba baada ya mwanamke kuwa na mtoto hujikuta mume hana nafasi tena kwake.
  Mke hujikuta ana hitaji kubwa la kutumia muda au uwezo wake kwa mtoto kuliko mume.
  Wanawake wa aina hii hutumia muda wote kwa ajili ya kuhudumia watoto na ni wapo wonderful kuitwa mama ingawa husahau kuhusu mume
  Kuchangia hii mada ngoja........Narudi........................................
   
 2. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #2
  Feb 17, 2010
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,590
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Hahah hivi hayo mambo yapo siku hizi? Tunahitaji kufanyiana yote siyo kusubiri upande mmoja.
   
 3. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #3
  Feb 17, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  naamini kla jambo ni zuri accoeding to circumstances na kila aina ya mke hapoinaweza kuwa nzuri au mbaya kutegemeana na hizo circumstances.
  muhimu wote wawili mke na mume "wabaki" kwenye nafasi zao za asili (natural roles). badala ya huu ulimbukeni wa kuvamia hoja za majukwaani za usawa potofu na kuzihamishia nyumbani........................
   
 4. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #4
  Feb 17, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,640
  Likes Received: 625
  Trophy Points: 280
  hahaha du na kweli inabidi tusaidiane jamani mie kama mama najua wajibu wangu kama mama lakini wakati mwingine nahitaji kusaidiwa ile tuweze kuendeleza gurudumu la ndoa
   
 5. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #5
  Feb 17, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  hii nimependa,imekaa vizuri.
   
 6. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #6
  Feb 17, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,292
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  mj1 hili jukwaa likifungwa sidhani kama utatamani kuishi!...:D:D
   
 7. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #7
  Feb 17, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,468
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Tehe tehe tehe tehe !! Aisee mimi hapo bora unipe huyo mke kama bosi kuliko huyo mke kama binti! Mambo ya LUKU imeisha unarudi nyumbani unakuta giza eti hajui hata jinsi ya kuingiza LUKU hilo balaa!
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...