Ni vita: Lowassa, Sumaye, Mwandosya - Madai ya matumizi ya fedha chafu yaibuka; Udini na Ukabila

huyu kijana anastahili awe mshauri wa CHADEMA yuko vizur
 
Lakini pia haiikatazi wala kuikemea. Hakuna KATIBA yenye kila kitu hapa duniani. Hata hivyo VITABU vitakatifu havina kila kitu.
Ukiangalia kwa undani hoja yangu imekuja baada ya yeye kusema "Kanuni na Katiba ya CHADEMA haziruhusu makundi" kwa hiyo nikataka kukuza uelewa wangu kama ni kutokana na Katiba ya CCM ndiyo maana ndani ya chama hicho kuna makundi hayo aliyoyafafanua!!
 
Wote wawili, Lowasa na Sumaye, hawatufai WATANZANIA kwa nafasi hiyo ya URAIS wa JMT. Ziangalieni hotuba za Mwalimu zinazorushwa mara kwa mara na ITV kuelekea maadhimisho ya kifo chake tarehe 14/10 ijayo.

Acheni ukanda nyie?Kwani kikwete alikuwa anafaa?CCM nani anafaa hadi leo?Hizi ni hila za CCM za kupiga vita Kaskazini tuu.CCm wote ni vimeo kama ni kura hakuna mwenye afadhali kwa hiyo kuchagua vyoyote hakuna harasara ya zidi ya mwingine.

tayari CCM wamepitisha viapo vyao vya kikanda vingi tuu,mara kaskazini ,mara mbeya sasa watakula ujinga wao.
 
Reactions: ral
Mikael P Aweda

Well you have as much as possible tried to connect the dots to come up with that good analysis katika thread yako ya https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-atangaza-kumvaa-lowassa-2015-a.html.....well done...ila nafahamu ww ni PRO-CDM kwahiyo u r good analysis inaweza ikawa na elements za biases...nadhani ujumbe wako mkuu katika thread ya hapo juu ni kuwa MAKUNDI NDANI YA CCM NI MTAJI (PLUS) KWA CHADEMA kuelekea kwenye uchaguzi wa 2015....Hapo ndio penye utata kwa upande wangu....hebu tujikumbushe kauli aliyoitoa JK tarehe 25/09/2012 pale Dodoma.

"Inashangaza kuona kugombea NEC tu watu wanataka kuuana, wanakimbilia nini huko ndani?" alihoji Rais Kikwete.
"Ina maana watu hawa wanaonyesha dhahiri kuwa hawana nia njema na chama, bali wanaingia kwa maslahi yao binafsi, hivyo tuna kila sababu ya kuwakataa ili tujenge timu ya ushindi ambayo ndiyo nia yetu," aliongeza mwenyekiti huyo.



Rais Kikwete alisema kama kuna wagombea ambao watajitoa ndani ya CCM na kuhamia chama kingine kutokana na majina yao kutopendekezwa, wajitoe.
"Hatuchagui wagombea wenye ndimi mbili ambao wanasema kama hatutapitishwa tutahamia chama kingine, hao tunawatakia kila la heri waende tu, kwani hawana nia njema na chama hiki," alisema kwa ukali.


Hiyo kauli ya JK kwenye Red ndio inayowatisha wale wote wanao lobby u presidaa 2015 kutodhubutu kujitoa CCM...ni dhahir shahir kati ya Sumaye/Sitta/Membe hakuna mwenye ubavu na uthubutu wa kujitoa CCM.....mm naamini SSM (Sumaye + Sitta + Membe) wanaihitaji CCM kuliko CCM inavyowahitaji wao....ila nakiri kuna mbunge ndani ya CCM ambaye siku zinavyokwenda nguvu yake ndani ya Chama inashika hatamu, huyu mbunge ni UNSTOPPABLE, kwa lugha ya kiswahili tunasema ni KISIKI CHA MPINGO....Ndugu yangu Nape alijaribu sana kuutikisa huu mti cha ajabu akabaki yeye anatikisika na ule mpango wake wa Kujivua Gamba ukazikwa Rasmi na Mzee Msekwa hivi majuzi.....Mzee wetu Sumaye naye alijaribu kuutikisa huu MPINGO lakini kilichotokea wote tunakifahamu...kwa kumbukumbu Mzee Sumaye alibwagwa huko HANANG ambayo ndio ngome yake kuu....Mzee Sumaye aliambulia kura 481 kati ya 1129 wakati Mshindi Katika Uchanguzi huo Dkt. Mary Nagu alipata kura 648...Kwahiyo Ni Dhahir Shair Mzee Sumaye hawezi na hataweza kupambana na Mbunge Huyu Ambae huko anapotokea ni Mfalme.....BUT, Kuna Mama Mmoja ambaye ni former UN Senior Figure anaonekana kuwa ni threat kwa Mbunge huyu katika harakati zake za kuelekea Magogoni....Huyu Mama Hana Ushawishi ndani ya Chama ila kuelekea uchaguzi wa 2015 wakereketwa wa CCM wanaweza kuaminishwa kuwa sasa ni wakati wa nchi hii kuongozwa na Mwanamke ( Kama Wabunge Walivyoaminishwa Katika Uchaguzi wa Spika na wakafyata) na pia kashfa za ufisadi mbali mbali ambazo bado zinamtesa Mbunge Huyu Kisiki zinaweza zikatumiwa kuzika ndoto zake za kuelekea Magogoni...Hakika mpambano wa Urasi ndani ya CCM ni TWO-HORSE RACE....

Inaweza ikawa....( Probability ni 0.9)

Mbunge huyu Kisiki cha Mpingo VS Mama Huyu wa United Nations - Hapa Mpambano Utakua Mkali Sana

Pia, inaweza ikawa.....(Probability ni 0.3)

Mbunge huyu Kisiki cha Mpango VS Waziri wa Mambo Ya Nje - Je, wapinzani wake watakimbilia Kenya 2016 kama alivyosema??

Hakika......Itakua ni Mpambano mkali hata zaidi ya mpambano wa leo kati ya Simba na Yanga....


NA DECLARE INTEREST

Viva
Mnyama Simba...Funga Yanga Hao
 
Mkuu Aweda
Tunashukuru kwa taarifa tujuze makundi ya Chadema au huko shwari makundi hakuna?

Chama
Gongo la mboto DSM

Mkuu Chama
Chadema haina makundi yoyote.Unaweza kunitajia makundi walau 3 Chadema kama yapo na wafuasi walau kumi kwa kila kundi? Jibu ni Hapana.Ila mimi ninaweza kukutajia makundi 4 au 5 yaliyoko CCM na wafuasi wa kila kundi.Hiyo ndiyo tofauti kubwa iliyoko.Nikuhakikishie CDM haitakaa iwe na makundi,katiba imeeleza wazi juu ya hilo na atakayebainika kuanzisha kundi atazimwa mara moja.Hiyo ndiyo Chadema mkuu wangu.
 
Msomali,kooooote umenifurahisha hitimisho lako tu!!! By the way CDM wameshatangaza mwisho wa kujiunga kwa vigogo wa CCM ni lini hivyo kazi kwao!
 
Msomali,kooooote umenifurahisha hitimisho lako tu!!! By the way CDM wameshatangaza mwisho wa kujiunga kwa vigogo wa CCM ni lini hivyo kazi kwao!
Watu hawakwenda Zenji kuchuma Karafuu au kujifunza kupika urojo!! Habari ndiyo hiyo hiyo.
 
Sio suala la ukanda hapa. Hawa jamaa wanafanana sana kwenye jambo moja: WOTE WAWILI NI WAWEKEZAJI WAKUBWA KWENYE SIASA. Kwao, UONGOZI wa KISIASA ni uwekezaji. Unalipa. Hawajali wala hawaangalii umewahakikishia MAFAO, MSHAHARA na MARUPURUPU kiasi gani kwenye ngazi hizi kubwa za kisiasa.

Mbaya zaidi, TAMAA hii kubwa wanaitumia kuwaneemesha pia familia, ndugu, rafiki, wapambe wao. Kama ulimsikiliza Jenerali jana watu wa aina hii hawatufai. Hawa sio VIONGOZI. Ni walafi tu.
.
 
Kwa uchaguzi huu wa wajumbe wa NEC wa Wilaya ULIOISHA ambapo HAWA WASHINDI ndiyo watapiga kura 2015 kumchagua mgombea wa CCM kupambana na CHADEMA yenye nguvu;NATANGAZA RASMI KUWA LOWASSA KASHINDA NOMINATION!

Nawashauri akina Sitta wahifadhi hizo hela zao kwa shughuli ingine;LOWASSA ataongoza hadi WILAYA YA KYELA nyumbani kwa hasimu wake Dr Mwakyembe!Wao walilala ili hali Lowassa alihakikisha kamati kuu ya CCM inapitisha watu wake na akafanikiwa kwa hilo!

Lowassa is very determinant;tukileta utani huyu jamaa atakuwa Rais kimzaha mzaha!
 

Nani sio mlafi katika CCM?Hata Lowasa kwa vile kawashikia pabaya ila ukweli upo wazi watu wa Kaskazini hawapendwi ktk hii nchi, na mdio maana hata waliopo ktk upinzani CCM haijaacha wafuata kwa bidii sana.Hili halina kificho...pia hii imeanza onekana pia kwa watu wa Mbeya ambao nao wamekumbana sana mikasa ya watu wao kufanyiw amajaribio ya kifo.Kilimanjaro Chami kaonja hilo joto la jiwe, Kombe naye alionja.

A good thing kwa uduni wa kifikra watu wenye kufanya hizi hila hawatofanikiwa hili.Kwa taarifa yao siku Kaskazini wataamua kujilinda na kujiwekea mipa there is very big chance wataumia sana hawa tu duni.Watu wa kaskazini wanaweza well organised sana wakiwa katk hostile land.Sasa hivi ni wazi watu wengi wapo tayari kumpigia mshukiwa wa ufisadi Lowassa kuliko mwingine katk CCM kwa vile wanajua CCM ni chukizo machoni pao.
 
Huyo mbunge kisiki unayemtaja anazo data za kumuumbua yule mama aliyekuwa UN. Nasikia walikutana NY akamwambia yule mama kwamba data zako tunazo, siasa za Tanzania tuachie sisi. Nasubiri hii mechi.
 
Reactions: ral
Unaposema watu wa Kaskazini unawalenga watu gani hasa? Hawapendwi na watu wa wapi sasa, wa Kusini, Mashariki au Magharibi? Kwa kigezo gani hasa. URAIS? Ni Kaskazini ipi unayoiongelea? Manyara? Tanga? Arusha? Kilimanjaro? Mara?

Huko mbona kumetoa VIONGOZI wengi tu wa NCHI hii! Mawaziri wakuu Sokoine, Msuya, Lowasa. Rais Mwalimu, Mawaziri karibu kila Cabinet ya NCHI hii tangu uhuru wamo. Wakuu wa Mikoa kibao, Wanajeshi wazito wengi tu: Kiwelu, Sayore, Kiaro,... Kwenye uongozi taasisi, asasi za kiraia, DINI ndio usipime! Kaskazini wanachukiwa kwa lipi?

Kwenye vyama vya SIASA, CHADEMA, TLP, NCCR, SAU,..., vyote vinaongozwa na watu wa KASKAZINI. Mpewe nini ili mjue kwamba mnapendwa?
 
Ndani ya Chadema naamini hakuna mitandao kama hii ya CCM. Mitandao ni kinyume na kanuni na katiba ya Chadema.

Mitandao ni vitu vinavyoibuka kutokana na vitamaa binafsi vya baadhi ya watu, kwa taarifa yako hata CCM sidhani kama Mitandao inaungwa mkono na kanuni na katiba yao lakini imejitokeza kutokana na roho za ubinafsi, hivyo basi hata SISI CHADEMA tukiruhusu hizi tabia tutakwenda na maji lakini naamini viongozi wangu akina ZITTO KABWE "hawana hizi tabia"
 

Nalenga hapo hapo kwenye Red.Na kuwepo kwao ni kwa vile inafikia stage ya kila kitu kuwa inevitable.Na hii huifanya serikali yoyote kushindwa watosa.Kama inavyowashinda kwa EL na wanavyojitahidi na mkanda na mdini mkubwa Zitto kuingilia CDM.Sasa wanawapeleka CUF kasakazini ili wakavuruge kura.

Usidhani kwa vile wazungu wamejiweka mahali penye nguvu ndio wanapoteza haki yao ya kulia wanapofanyiwa ubaguzi wa rangi, au mwanamume hana haki ya kulia kuwa kabakwa.
 
Mnachukiwa kwa lipi sasa! Au ni nyie mnafaa kututawala wakati wote, muda wote, nafasi zote? Nani hasa anawachukia?
 
Njia ya Chadema kushinda 2015 iwepo katiba mpya au ya zamani ni nyeupe mno. Hii ni kwa sababu, hata kama hakutakuwa na kundi litakalohamia chadema kati ya makundi hasimu (Naamini wako watakaokimbia) hakuna siri itafichika ambalo haitajulikana na Chadema ikiwepo mipango ya kuchakachua kura – hakuna ushindi bila uwezo wa kutunza siri.
NB; Nadhani nimepunguza sana ushabiki wa kisiasa na kuweka ukweli mtupu.


NAona unaota ndoto za mchana kweupe! chadema hata ifanye nini haitashinda mwaka 2015, labda mumuweke Zitto Zuberi Kabwe, lakini hicho kibabu chenu ni mnajisumbua bure! Lowasa ndio rais wetu mtukufu ajae ! hiyo nakuambia ! na kama unabisha subiri !
 
Sumaye Vs Lowasa? hii mechi haitakuwa na watazamaji, Lowasa atashinda kwa knock out ndani ya raundi ya kwanza
 

Na wewe naona unaota mchana mchana pia, ntahama nchi kama kweli nchi hii itatokea iongozwe na mwanamke ! yaani NI BADO KUONGOZWA NA MWANAMKE , ... hii nchi inataka huyo kisiki cha mpingo Lowasa, ! ndio anafaa ili kidogo tunyooke !
 
Mnachukiwa kwa lipi sasa! Au ni nyie mnafaa kututawala wakati wote, muda wote, nafasi zote? Nani hasa anawachukia?

Maswali ayko yanapingana ya kwanza yanaonyesha unawajua na wewe pia upo included na la mwisho linauliza tena ni akina nani.kama umefuatilia huku JF utaona postings nyingi zinavyowashambulia kuanzia TRA hadi ktk Siasa, wanakwenda hadi wizara ya elimu bila jua watu wa kaskazini walitoa kila kitu ili wawe na vitu vy akijamii hata vya kiwango cha chini ila uzao wao wapate elimu wakati wengine wakicheza ngoma, na kupiga soga hukuw engine wakioza mabinti tuu.Kaskazini average age ya mabinti muolewa upo juu sana ukilinganisha na mikoa mingi.

By the way hao watu si watawala,watwala si lazima wawe viongozi.Kwani watwala wanaweza weka vibaraka.Wa kaskazini hawajwa na hiyo interest ndio maana hawajaamua weka vibaraka.Wao wanaongoza ktk nyanja nyingi sana nchini hadi kufikia mafanikio na bado wanaendelea na hivyo si mbaya kuongoza taifa ktk upande wa kisiasa pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…