Seif Kazige Mbambizi
Senior Member
- May 7, 2016
- 135
- 92
Naikumbuka leo kauli ya headmaster Mkombo tulipo kuwa Kigoma Secondary School miaka hiyo. Nikiwa sehemu ya viongozi wa wanafunzi head Master Mkombo mara kadhaa katika semina zake alipenda sana kutuasa.
" Huwezi kutumia nguvu kuziba midomo ya wananchi(wanafunzi, waacheni wwaongee kisha mchukue changamoto hizo mzifanyie kazi".
Nashangaa sasa katika mazingira ambayo watanzania wengi wanao uwezo wa kuongea na kuikosoa serikali inayojinasibu kuwa ni serikali ya watu masikini wanazibwa midomo wasiseme yale wanayo dhani kuwa ni madudu ya serikali.
Kwa uelewa wangu mdogo ninacho fahamu ni kwamba kazi ya kufuli sio kufunga midomo ya watu isipo kuwa mlango, kabati na kadhalika. Sasa hili kufuli la kutufunga midomo linatoka wapi.