Ni vigumu kumtoa CAG madarakani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni vigumu kumtoa CAG madarakani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Madcheda, Nov 19, 2011.

 1. M

  Madcheda JF-Expert Member

  #1
  Nov 19, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 416
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  kwa mujibu wa katiba ya jamuhuri ya muungano wa tz kifungu cha 144

  144.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengine yaliyomo katika ibara hii, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu wa Jamhuri ya Muungano atalazimika kuacha kazi yake atakapotimiza umri wa miaka sitini au umri mwingine wowote utakaotajwa na Sheria
  iliyotungwa na Bunge.

  (2) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu aweza tu kuondolewa katika madaraka ya kazi yake kwa sababu ya kushindwa kutekeleza kazi zake (ama kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote) au kwa sababu ya tabia mbaya, au kwa kuvunja masharti ya sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma na hataweza kuondolewa kazini ila kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (4) ya ibara hii.

  (3) Iwapo Rais anaona kwamba suala la kumwondoa kazini Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu kwa mujibu wa masharti ya ibara hii lahitaji kuchunguzwa, basi katika hali hiyo mambo yatakuwa ifuatavyo:

  (a) Rais atateua Tume Maalum ambayo itakuwa na Mwenyekiti na Wajumbe wengine wasiopungua wawili. Huyo Mwenyekiti na angalau nusu ya wajumbe wengine wa Tume hiyo itabidi wawe watu ambao ni Majaji au watu waliopata kuwa Majaji wa
  Mahakama Kuu au Mahakama ya Rufani katika nchi yoyote iliyomo kwenye Jumuiya ya Madola;

  (b) Tume hiyo itachunguza shauri lote halafu itatoa taarifa kwa Rais kuhusu maelezo ya shauri lote na itamshauri Rais kama huyo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu aondolewe kazini kwa mujibu wa masharti ya ibara hii kwa sababu ya kushindwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufanya kazi kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote au kwa sababu ya tabia mbaya.

  (4) Ikiwa Tume iliyoteuliwa kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (3) itamshauri Rais kwamba huyo Mdhibiti na Mkaguzi
  Mkuu wa Hesabu aondolewe kazini kwa sababu ya kushindwa kufanya kazi kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote
  au kwa sababu ya tabia mbaya, basi Rais atamwondoa kazini.

  (5) Ikiwa suala la kumwondoa kazini Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu limepelekwa kwenye Tume kwa ajili ya uchunguzi kwa mujibu wa masharti ya ibara hii, Rais aweza kumsimamisha kazi huyo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu, na Rais aweza wakati wowote kufuta uamuzi huo wa kumsimamisha kazi, na kwa hali yoyote uamuzi huo utabatilika ikiwa Tume itamshauri Rais kwamba huyo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu asiondolewe kazini.

  (6) Mtu ambaye ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu au aliyepata kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu hawezi kuteuliwa kushika au kushikilia madaraka ya kazi nyingine yoyote katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

  (7) Masharti ya ibara hii hayatatumika kwa mtu yoyote aliyeteuliwa kuwa Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu.
   
 2. Didia

  Didia JF-Expert Member

  #2
  Nov 19, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 721
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 45
  palipo na utashi wa kisiasa bado kuna nafasi maana neno tabia ni la ujumla mno na linaweza tafsriwa kumtia hatiani. Tatizo huyu bwana ameisadia serikali na viongozi wake sana na hivyo hawezi kuchukuliwa hatua. Labda atapewa tu onyo kama gelesha lakini kwa monopoly watawala waliyonayo kwa Spika wa Bunge utekelezaji wa mapendekezo ya tume utakuwa cosmetic na hakuna atakaye jali
   
 3. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #3
  Nov 19, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Hivi kuna mtu ataachia ngazi hapo kweli? Mi mbona sitegemei hata huyo Jairo ataendelea kudunda na kutupiga piga mashavu pande zote huku tukiwa tumeinama kwa aibu za yale tuliyochangia mjengoni kuhusu Jairo - Report.
   
 4. M

  Madcheda JF-Expert Member

  #4
  Nov 19, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 416
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Cpingan na wewe ila ukisoma kifungu cha 3 utaona kwamba lzm majaji watoke nchi za jumuiya ya madola! Sio process ndogo kaka
   
 5. M

  Madcheda JF-Expert Member

  #5
  Nov 19, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 416
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Kweli itakua kma repoti ya mwakyembe tu
   
 6. a

  asakuta same JF-Expert Member

  #6
  Nov 19, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 15,065
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 0
  km tungekuwa serious hiyo namba 2 ingemuondoa kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake aidha kwa kulindana au rushwa.
   
 7. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #7
  Nov 19, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Amekiuka maadili ya kazi anang'oka.
   
 8. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #8
  Nov 19, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,320
  Likes Received: 5,611
  Trophy Points: 280
  Tunasubiri producer wa series atengeneze episode za series mpya yaitwa Jairo!!
   
Loading...