Benki ya dunia iliunda njia mpya ya makundi ya uchumi mwaka 2016 baadala ya kutumia makundi kama Developing Countries na Developed Countries.
Benki ya dunia imezitenga nchi wanachama katika makundi manne.
1. Uchumi WA Chini.
2. Uchumi WA Kati WA Chini (tz imo humu)
3. Uchumi WA Kati wa juu
4. Uchumi WA juu
Ambapo GDP per capita ya Tz ni 1159 USD Kwa mwaka 2021.
Hii benki ilifanya hivyo ili kila kundi lipate vipaumbele vinavyostahili.
Kwa sababu wakati walipokuwa wanatumia makundi kama NCHI ZILIZOENDELEA na NCHI ZINAZOENDELEA, Nchi kama TZ na China zilikuwa zinawekwa kwenye mizani Sawa kitu ambacho hakipo Sawa.
Kumbuka China ni nchi inayoendelea.
Sioni hata haja ya kuanzisha Uzi Kwa sababu nchi zote zilizomo kundi la Kwanza na la pili zinafahamika kuwa ni nchi masikini ndio maana ikawekwa makundi Mapya ili kupewa vipaumbele vinavyostahili ikiwemo mikopo nafuu.
Hata nchi zenye uchumi WA Kati WA juu nyingi Pia ni masikini.
Vinginevyo labda thread iwe ni ya propaganda kama jinsi chama tawala walivyokuwa wanafanya propaganda na Neno "uchumi WA Kati"