Ni uwezo wa Zitto Kabwe au CHADEMA?

Ni uwezo wa Zitto Kabwe au CHADEMA?

mtaumbuka muda si mrefu, hamjakata tamaa na kuwaonea watanzania huruma baada ya mpango mzima wa masalia kufichuka? kama mnataka mwenyekiti au katibu kutoka kigoma si muanzishe chama chenu cha kikabila mueleweke kabisa? mnasubiri nini angali mnadai kinara wenu zzk anamvuto kwa jamii? hii ni baadhi tu ya mipango haramu ya ccm ya kutika kuuwa upinzani nchini! wameshindwa na watashindwa tena!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!


duh!!!!!! povu mzee, tena povu lenye harufu mbaya sana ya MBEGE... Bonsafooo
 
Hivi kwanini hao watu kijiweni wasifuati kauli ya Zitto mwenyewe? "fuata misingi ya chama na sio watu sababu watu wanayumba, misingi haiyumbi".
It is about time wanachama waache kukigawa chama kwa misingi ya udini na ukanda na waanze kupigana the real struggle.
Leo kuna more attacks from cdm members against cdm leaders than there are attacks from ccm.

Sure thing...kinachokila chama ni wanachadema
 
Last edited by a moderator:
changia uzi huu kwa maslahi ya chama na si kwa maslahi ya mtu fulani.maana huku mtaani chama kimechafuka na tunatumia nguvu nyingi kukitetea.

Serikali ya Denmark imetoa shilingi milioni 400 kwa lengo la kuimarisha BAVICHA na BAWACHA.... hiyo ni taarifa tu ...i thought its worth sharing... (Mwananchi, 2013)
 
Leo nilikuwepo katika kijiwe kimoja hapa Morogoro,hawajamaa ni marufu sana kwa kuichambua siasa ya Tanzania.Hoja kubwa ikawa ni umaarufu wa Zitto ambao wengi wanadai kwa sasa unazidi hata umaarufu wa chama,hivyo wadau wengi wakadhauri kua Zitto ni mtaji mkubwa kwa chama endapo wataamua kumtumia ktk uchaguzi mkuu wa 2015 kwa sababu zifuatazo.

1.Kuifuta propaganda ya udini iliyoanza kuenezwa kwa wa tz.

2.Kuifuta propaganda ya ukabila na ukanda inayoenea kwa kasi sana.

3.Zitto anakubalika sana maeneo mengi kutoksna na michango yake bungeni yenye maslahi kwa taifa.

4.Zitto kukosa kashfa zinazo mkabili.mfano wapo wanao shutumiwa kwa kuwa na kadi zaidi ya moja.hii ni ngumu kumuelewesha mwananchi wa kawaida.hivyo kwa zitto haitamkumba.

5.Watanzania sasa hasa vijana wanaimani kubwa na vijana kuliko wazee.hii ni kutokana na mapinduzi makubwa yaliyofanywa na vijana bungeni.

TUMUUNGE MKONO KIJANA HUYU MCHAPA KAZI ILI ATUSAIDIE KUINGIA IKULU 2015.
Uko sawa lakini sidhani kama vijana wenzako wameshafanya lolote zaidi ya kujitafutia umaarufu wa kisiasa. Vijiwe vya aina hiyo Mkuu vipo vingi sana, watu hawafanyi kazi kutwa kuchambua siasa, unafikiri tutafika kokote kwa kutokufanya kazi? Pato la taifa halitoongezeka kwa kukaa kijiweni kuchambua siasa.
 
kwa mtu yeyote makini anaefanya maamuz kwa UTAFITI
FIKRA
UKWELI&UJASIRI
asiyekuwa kibaraka atakubaliana na mada kuwa ZITTO ni chaguo sahihi na chaguo la wengi!!!
hata chadema,mbowe,slaa wanaliju hilo...!
Kwa mtu yeyote aliye makini na anayefanya maamuzi kwa UTAFITI atagundua kua migogoro mingi ndani ya CDM chanzo ni ZITTO, ni migogoro michache sana ndani ya CDM ambayo Zitto hana mchango. Tafakari kwa akili huru utaliona hilo lipo dhahiri sana!
 
Kwa kweli Tanzania kwa hali tuliyo nayo tunahitaji mabadiliko; mabadiliko hayo yapo mikononi mwa wenye nia ya kuleta mabadiliko hayo ; ni vizuri kuwatia moyo na kuielimisha jamii isiyojua chochote kuhusu uchafu unaofanywa na serikali ya sasa; si vizuri kuwachafua wanaharakati hawa ambao wanawaza mema juu ya nchi yetu
 
Zitto kweli yuko Bomba.
Ila ninawasiwasi nae kwa kuiga ung'ang'anizi wa rafiki yake fastjet kutaka urais kabla hajabarehe.
Yawezekana ndiomana ni rafiki mkubwa wa fastjet.
Kwanini hasisubir?
Kinachomfanya ang'ang'ane kinyume cha katiba nini?
Nakumbuka fastjet mwaka 95 naye alifanya kama zzk anavyofanya,so mnatupa picha gan hapa? Tena watu marafiki,
ZZK AKITULIA,AKAUNGANA NA WENZIE KTK HARAKATI MBALIMBALI MF:M4C N.K,NA KUSUBIRI WAKATI WAKE, NA KUACHANA NA VIRAZA WANAEMUUNGA MKONO KWA ITIKADI YA UDINI ATAKUWA MZURI KULIKO ALIVYO SASA.
Naamin ni kiongoz mzur na wa mhimu ktk chama, lakin wapo waliomzidi.
Kwa mf:Akiondoka Slaa,ama Mbowe cdm litakuwa pigo zaidi, so zzk puuza kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa.
 
Zitto aanzishe chama chake chadema hamfai


zzk alisema "Nitakuwa wa MWISHO kuisaliti CDM, CDM inadamu yangu,inamuda wangu,na inajasho langu"
pia alisema "CDM ni chama kisicho na udini ukanda,ukabila,na ni taasisi ya demokrasia iliyo imara"
nimethibitisha haya baada ya kuona wabunge na viongozi wa CDM wakiwa wa dini tofautitofauti,makabila tofauti, na wakiwa wanatoka pande zote za Tz.
Zzk ni mtu anayejitambua tofauti na mamburura wanaodhani watamshawishi kwa kigezo cha udini.
MMESHINDWA KWA KIGEZO CHA UDINI,
MMESHINDWA KWA KIGEZO CHA UKANDA NA UKABILA.
MMESHINDWA KWA KUZUSHA MAUAJI MNAYOYAPANGA WENYEWE,MMESHINDWA KWA KIGEZO CHA KADI,
MMESHINDWA KWA KIGEZO CHA BONGO MOVIE.
.Sukar 2000-2,500/=
.petrol zaidi ya lt@2,000/=, Zanzibar lt@3,500/=
.Dola 1@1,600/=
.Deni la taifa zaidi ya tril.22.
N.k
BADO MNALETA SIASA ZA MAJITAKA NA MAJUNGU YASIYO NA TIJA, na KUPAKA WATU MAFUTA KWA MGONGO WA CHUPA?
Kwa namna hii kufika tutachelewa saana.
WATZ TUBADILIKE.
 
changia uzi huu kwa maslahi ya chama na si kwa maslahi ya mtu fulani.maana huku mtaani chama kimechafuka na tunatumia nguvu nyingi kukitetea.

huku kwetu hali ni shwari labda kwako tu na usitumie kuchafuka kwa eneo lako kufanya tathimini ya nchi nzima, tuondolee umasalia wako hapa
 
Back
Top Bottom