Ni uwendawazimu kuuvunja Muungano kwa hoja ya "Wazanzibar na Watanganyika hawakushiriki kuunda"

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Kumekuwa na malalamiko, manung'uniko, vibweka na kila aina ya vituko vya kutaka kuuvunja Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulioasisiwa 1964 na Wananchi wa pande zote za Muungano wasiozidi 100 kila upande, wakiongozwa na Julius Nyerere upande wa Tanganyika na Sheikh Abed Karume upande wa Jamhuri ya Zanzibar,

Hoja kuu inayotembezwa na wanaotaka kuuvunja muungano huu ni kuwa

Wananchi wa nchi hizo mbili hawakushirikishwa, kwa lugha moja ama nyingine wanataka kura ya maoni ya kuuhitaji muungano ama kuukataa,

Mimi naamini hawa hawajafanya utafiti yakinifu kujenga hoja zitakazo shawishi kuuvunja Muungano huu,

Kwabahati mbaya baadhi ya wakuu wa mamlaka za nchi wameingia kwenye mtego huu bila kujiuliza japo kidogo,

Hivi hoja ni kushirikishwa kuunda au ni UBORA wa kilichoundwa?

Hapa mimi naona muhimu si wingi wa wafanya maamuzi, bali ni umakini wa maamuzi yenyewe,

Tujiulize, mbona hawa wanaopinga Muungano kwa madai Wananchi hawakushirikishwa hawakuipinga TANU iliyoasisiwa na Watanganyika 17 na ikaleta Uhuru huu tunaouishi leo?

Taifa la Tanganyika liliundwa na Watanganyika/Tanzania wasiozidi 17 na leo lipo na wote tunaliishi bila kudai hatukushirikishwa kuliunda,

Jambo baya zaidi watu hawa wanasahau ama hawaelewi kuwa MKATABA wa MUUNGANO ulipelekwa katika mabunge ya nchi hizi mbili na UKARIDHIWA na kisha UKASAINIWA

Mpaka hapo tu inatafsiriwa kuwa WANANCHI walishirikishwa kupitia wawakilishi wao BUNGENI tena Bunge la ASP na TANU,

Watu waje na sababu za msingi za kutaka kuvunja Muungano sio hili wanalolihubiri

Mimi ni mmoja ya wanaunga mkono kuvunjwa kwa Muungano huu, lakini nikiwa na mtazamo tofauti na walio na hoja ya kuwa "Wananchi hawakushirikishwa kuunda",

Mtazamo wangu nikuwa Manung'uniko ya Wazanzibar ya mezidi, ikiwa serikali haionyeshi juhudi za kushughulikia kwa vitendo ni bora Muungano huu uvunjike haraka kunusuru chuki hii kali,

Wazanzibar hawajapewa elimu yakutosha juu ya Muungano huu na faida zake kwao, hivyo akitokea mpuuzi yeyote akapatanda jukwaani na kuwalisha ngano za uzushi na upotoshaji wanaamini,

Muungano limekuwa jambo la siri kubwa jambo linalotafsiriwa kuwa kuna hujuma ndani yake,

Njia rahisi ya kutatua chuki za Muungano huu ni kuwa na serikali TATU tu,

Zanzibar ipate mamlaka kamili ya ndani na Tanganyika irudi tena irudi kwa heshima ile ile ya Nchi HURU,

Kuweka serikali MOJA ndani ya MUUNGANO huu ni kuwasha hasira ya Mzanzibar aliyekwisha aminishwa kuwa anatawaliwa na Mtanganyika,

Vile vile kuacha serikali MBILI kama ilivyo sasa ni kuukwepa mgogoro uliopo na kulea BOMU,


Nauliza ndugu zangu, ni HOJA gani ya kuuvunja Muungano? Kama haipo basi tuulinde MUUNGANO huu kwa kuunda SERIKALI TATU tu,

Hebu tusome mkataba wa Muungano hapa chini:


MKATABA WA MUUNGANO BAINA YA JAMHURI YA TANGANYIKA NA JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR


Kwa kuwa Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar zinafahamu uhusiano wa muda mrefu watu wake na mshikamano na kukuza uhusiano huo na kuimarisha mshikamano na kukuza umoja wa watu wa Afrika, zimekutana na kutafakari Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar.

Na kwa kuwa Serikali za Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar, zinapendelea ya kwamba Jamhuri hizi mbili ziungane kuwa Jamhuri moja huru moja kwa amasharti ya makubaliano yafuatayo:

Kwa hiyo IMEKUBALIWA baina ya Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika na ya Jamhuri ya watu wa Zanzibar kama ifuatavyo:-

I) Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar zitaungana na kuwa Jamhuri huru moja.

II) Katika kipindi cha kuanza kwa Muungano mpaka Baraza la Kutunga katiba lililotajwa katika ibara ya (vii) litakapokutana na kupitisha katiba ya Jamhuri ya Muungano (Kuanzia hapa kitaitwa kipindi cha mpito), Jamhuri ya Muungano itaongozwa kwa masharti ya ibara ya (iii) mpaka ya (vi).

III) Katika kipindi cha mpito katiba ya Jamhuri ya Muungano itakuwa katiba ya Tanganyika iliyorekebishwa ili kuweka:

a) Chombo tofauti cha kutunga sheria na Serikali kwa ajili ya Zanzibar kwa mujibu wa sheria zilizopo za Zanzibar na vitakuwa na mamlaka ya mwisho katika Zanzibar kwa mambo yote isipokuwa yale tu yaliyo chini ya bunge na Serikali ya Jamhuri ya Muungano

b) Nafasi ya makamo wawili wa Rais mmoja kati yao akiwa ni mkaazi wa Zanzibar atakuwa ndiye kiongozi wa Serikali iliyotajwa kwa ajili ya Zanzibar na atakuwa ndiye msaidizi mkuu wa rais wa Jamhuri ya Muungano katika utekelezaji wa kazi za Serikali kwa upande wa Zanzibar.

c) Uwakilishi wa Zanzibar katika bunge la Jamhuri ya Muungano.

d) Mambo mengine yatayofaa au kuhitajika ili kuipa nguvu Jamhuri ya Muungano na mkataba huu.

IV) Mambo yafuatayo yatakuwa chini ya bunge na Serikali ya Jamhuri ya Muungano:-

a) Katiba na Serikali ya Jamhuri ya Muungano
b) Mambo ya nchi za nje
c) Ulinzi
d) Polisi
e) Mamlaka yanayohusika na hali ya hatari
f) Uraia
g) Uhamiaji
h) Mikopo na biashara ya nchi za nje
i) Utumishi katika Jamhuri ya Muungano.
j) Kodi ya mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika, ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa nchini na kusimamiwa na idara ya forodha
k) Bandari, mambo yanayohusu usafiri wa anga, Posta na Simu

V) Bunge na Serikali vilivyotajwa vitakuwa na mamlaka ya mwisho juu ya mambo yote yahusuyo Jamhuri ya Muungano na kuongezea mamlaka juu ya mambo yote yahusuyo Tanganyika.

Sheria zote zilizopo za Tanganyika na za Zanzibar zitaendelea kutumika katika maeneo yao bila kuathiri:-

a) Masharti yoyote yatakayowekwa na chombo chenye mamlaka ya kutunga sheria.

b) Masharti yatakayowekwa kwa amri ya Rais wa Zanzibar juu ya sheria yoyote inayohusu jambo lolote lililotajwa kwenye ibara ya (iv), na kufuta sheria yoyote inayolingana Zanzibar.

c) Mabadiliko yoyote kama yataonekana yanafaa au kuhitajika ili kufanikisha Muungano na mkataba huu.

a) Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano atakuwa ni Mwalimu J. K. Nyerere na ataongoza Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa kufuata masharti ya mkataba hu na kwa kusaidiwa na maofisa wengine atakaowateuwa toka Tanganyika na Zanzibar na watumishi wa Serikali zao.

b) Makamo wa kwanza wa Rais kutoka Zanzibar aliyeteuliwa kwa kufuata marekebisho kama yalivyoelezwa na ibara ya 3, atakuwa Sheikh Abeid Karume.

VI) Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa kukubaliana na Makamo wa Rais ambaye ni kiongozi wa serikali ya Zanzibar

a) Atateua tume kwa ajili ya kutoa mapendekezo kwa ajili ya katiba ya Jamhuri ya Muungano.
b) Ataitisha Baraza la kutunga katiba ikiwa na wawakilishi kutoka Tanganyika na Zanzibar katika idadi itakayoamuliwa likutane katika kipindi cha mwaka mmoja tokea kuanza kwa muungano kwa madhumuni ya kutafakarimapendekezo ya tume iliyotajwa juu na kupitisha katiba ya Jamhuri ya Muungano.

VII) Mkataba huu utahitaji kuthibitishwa kwa kutungiwa sheria na Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi la Jamhuri ya Watu wa Zanzibar kwa kushirikiana na Baraza lake la Mawaziri, na mkataba kupitishwa na kuundwa kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano na ya Zanzibar kwa kufuata masharti yaliyokubaliwa.

KWA KUSHUHUDIA HAPA Julius K. Nyerere, Rais wa Jamhuri ya Tanganyika na abeid Karume, Rais wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, wametia saini nakala mbili za mkataba huu, hapa Zanzibar siku ya tarehe Ishirini na mbili ya mwezi Aprili, 1964.

…………………………………………………………………………………………………….
Umepitishwa na Bunge siku ya tarehe Ishirini na Tano ya Aprili, 1964.


…………………………………………………………………………………………………….
Pius Msekwa, Karani wa Bunge

…………………………………………………………………………………………………….
Adam Sapi Mkwawa, Spika
25 Aprili 1964

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
SOURCE:

1: {THE PATNERSHIP, ISBN: 9789987880553, pg. 156, Author: Aboud Jumbe, }

2: {Zanzibar hadi mwaka 2000: ISBN: 9789987898015, pg. 201, Author: Ali Shaaban Juma}
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
 
Sasa kama wananchi hawajashirikishwa huo ubora utatokea wapi?zanzibr kwanza.
 
Nakuomba wewe hebu Nipe faida 3 tu za msingi ambazo Wa-Zanzibari wamenufaika na huo unaoitwa Muungano ambao kiukweli ni UKOLONI wa Tanganyika kwa Zanzibar
 
Nakuomba wewe hebu Nipe faida 3 tu za msingi ambazo Wa-Zanzibari wamenufaika na huo unaoitwa Muungano ambao kiukweli ni UKOLONI wa Tanganyika kwa Zanzibar

Faida zipo nyingi sana na tatu za msingi ni

1) Imenufaika na kupata BURE huduma za jamii kama elimu ya juu, Umeme,

2) Mahusiano ya kidugu

3) Uimarishwaji wa Ulinzi na usalama

Nyongeza, KUSAIDIA pengo la bilioni 500+ la BAJETI ya Zanzibar
 
Mwanasheria wa zanzbr anasema hakuna kikao wala hansad za bunge la zanzbr lilojadili muungano.

Huyo hajijui kuwa yupo ofisi gani,

Spika wa Bunge la Zanzibar wa (ASP) ni sehemu ya walioshiriki kusaini mkataba ule kwa Tgk alikuwapo Adam Sapi
 
Uendawazimu kasema nani?

kuulazimisha muungano ambao wapo watu wameuchoka pia ni uendawazimu
kilichopo ipigwe kura ya maoni tu

wanaoutaka waseme,wasioutaka waseme
 
Uendawazimu kasema nani?

kuulazimisha muungano ambao wapo watu wameuchoka pia ni uendawazimu
kilichopo ipigwe kura ya maoni tu

wanaoutaka waseme,wasioutaka waseme

Nikwekweli tusiulazimishe,

Lakini tuje na hoja za mafaa ili kuhalalisha matakwa yetu,

Je hoja ya msingi kuuvunja Muungano huu ni nini?
 
Ninayo ile ya kibunge, ikilazimu nitaileta hapa mkuu

Wanaotaka kuuvunja waje na hoja za msingi tukubaliane nao ama tuwakatalie

Bunge lipi?njoo na hati ya muungano ya nyerere na karume,tupate kuangalia tulipo jikwaa.
 
Kushirikisha wananchi katika maamuzi yanayo determine destiny yao hasa katika dunia ya sasa ni jambo jema,kwanini tuishi kama zamani.Hoja ya TANU haina mashiko kwa sasa,sababu vyama vyote vya siasa vinaanzishwa na watu wachache ,lakini vinapata ridhaa ya umma kupitia chaguzi hurur na za haki.
 
Kushirikisha wananchi katika maamuzi yanayo determine destiny yao hasa katika dunia ya sasa ni jambo jema,kwanini tuishi kama zamani.Hoja ya TANU haina mashiko kwa sasa,sababu vyama vyote vya siasa vinaanzishwa na watu wachache ,lakini vinapata ridhaa ya umma kupitia chaguzi hurur na za haki.

Real maamuzi ya zamani hayana mafaa leo?

Hivi nikweli hapa hoja ni ushirikishwaji na sio ubora wa kilichoundwa na wachache?

Mkuu hebu jenga hoja vizuri
 
Mtoa mada naona ushirikishwaji wa wananchi kwa upande wako sio hoja,hoja yako inalenga kuangalia ubora,unaonaje CC ya ccm waingie tena kambini dodoma na kutuletea katiba bora bila ya ushirikishaji wa wananchi,je utaikubali katiba hiyo,inawezeka ikawa katiba bora kwa ccm je kwa mwananchi asie chama?
 
Mtoa mada naona ushirikishwaji wa wananchi kwa upande wako sio hoja,hoja yako inalenga kuangalia ubora,unaonaje CC ya ccm waingie tena kambini dodoma na kutuletea katiba bora bila ya ushirikishaji wa wananchi,je utaikubali katiba hiyo,inawezeka ikawa katiba bora kwa ccm je kwa mwananchi asie chama?

Kwamda wa miaka 50 sasa katiba tunayotumia ni ile iliyotungwa na ccm,

Tumekubaliana Watanzania wote kwa hoja moja kuwa katiba hii inamapungufu ama baadhi yamepitwa na wakati hivyo tuje na katiba mpya,

Hivyo hapa hoja ni kuwa "tumekubaliana kuwa katiba iliyopo haikidhi matakwa ya sasa"

Je kwenye Muungano hoja kuu nini?
 
Faida zipo nyingi sana na tatu za msingi ni

1) Imenufaika na kupata BURE huduma za jamii kama elimu ya juu, Umeme,

2) Mahusiano ya kidugu

3) Uimarishwaji wa Ulinzi na usalama

Nyongeza, KUSAIDIA pengo la bilioni 500+ la BAJETI ya Zanzibar
Muungano ukivunjika wewe mdanganyika utafaidika na nini?
 
Back
Top Bottom