WAZIWAZI
JF-Expert Member
- Mar 10, 2014
- 1,815
- 1,575
Ndugu wanajanvi nampa pole zangu ndugu yangu Lowassa kwa ajali ya kisiasa iliyomkuta na kutengenezewa zengwe la Richmond jambo lililobabisha ajiuzuru uwaziri mkuu wakati badae watu walewale walioshadadia kung'oka kwa nguli huyu wa siasa wakairudia jamii na kuiambia yaliyomkuta lowassa yalikuwa ni mambo ya kupika tu na hayakuwa na ukweli wowote na hata list of shame waliyoisoma pale mwembe yanga pia yalikuwa ni majungu kuihadaa jamii ili imchukie lowassa.
Tukijikumbusha siku za karibuni kuna kikundi chenye mienendo ilele iliyofikia lowassa kuchafuliwa nchi nzima sasa kinamuandama Makonda usiku na mchana kwa sababu zisizo na mizizi mpya ikidaiwa yeye kuiteka media ya Clouds, kwa watu wenye akili ya kawaida na wasio mashabiki kindakindaki wa upande wowote wanaweza kujiuliza hivi hao wanaodai kutekwa wanajua maana ya kutekwa tena kwa mtutu wa bunduki ingekuwa ni kweli wale maaskari wamepania kushinikiza habari itangazwe waandishi wa clouds wangegoma!! ? tafakari, pili tunajua kwa sasa kama Rais asipompa makonda ulinzi mkubwa kiasi kile kufuatia vita aliyoianza na wahalifu wa dunia genge la wauza madawa ya kulevya basi maisha yake yatakuwa hatarini ndo maana alionekana kwenye kamera akiwa na walinzi na walinzi hawakuonekana kumsumbua mtu yeyote zaidi ya kuhakikisha uasala wa kiongozi wao ambayo ndo kazi yao kubwa waliyopewa na sidhani kama mkuu wa mkoa kuingia sehemu yeyote na ulinzi ni kosa bila kumuumiza au kumbughudhi yeyote.
Nimeyasema haya kuwakumbusha tu kwamba endapo Lowassa angekuwa waziri mkuu enzi hizi za Magufuli na kukumbwa na kashifa za kupika kama yaliyomkuta, Rais Angemlinda na kumkatalia kujiudhuru na hii ndio sifa mojawapo kubwa ya kiongozi kwa wasaidizi wake na niwambie ndugu zangu makonda saga ni vilevile kama Lowassa saga enzi hizo.
Asubuhi njema.