Ni ushauri upi unafaa kufanyiwa kazi?

Izzi

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
553
1,135
9a9cce4598cb71a5efb618017be5427b.jpg

Chukulia una jambo unahitaji kulifanya, yaweza kuwa biashara au unahitaji kufanya maamuzi fulani... je, ikiwa anaekushauri hana uzoefu na hilo suala utaufanyia kazi ushauri wake au la?

Nini maoni yako juu ya mtazamo kwamba: "KAMWE USISIKILIZE USHAURI TOKA KWA MTU AMBAE HAJAFIKA UNAPOTAKA KUFIKA au HAJAPATA UNACHOTAKA KUPATA"

Mimi.. ninashukuru.
 
mkuu..!

ukifanya hivyo utajizibia baadhi ya riziki zako wewe mwenyewe..

Nakupa mfano; Mimi wazazi wangu hawajasoma hadi mahali nilipofikia mimi, Je, Ingekuwa ni jambo jema kupuuza ushauri wao hata kama naona unanisaidia katika masomo yangu na maisha yangu nje ya masomo? kisa tu hawajafika mahali nilipo au ninapotaka kufika!

Hapana; Mambo hayaendi hivyo, sio kila aliyefika mahali unapotaka kufika, basi na yeye atapenda ufike hapo, tena hao hao ndio wanaoweza kukushauri vibaya ili ubaki hukohuko chini ulipo.
 
Asante mkuu.
 
Inategemea na aina ya Ushauri
Kibiashara ukitaka kufanikiwa unaskia Ushauri wa watu wote mpaka wateja wako. MFANO Kuna jamaa Ana duka anataka aongeze bidhaa wakati mwingine lazima asikilize wateja wake. Pia Ushauri Kwa wafanya biashara wengine. Kuna WATU WANA mawazo mengi mazuri kichwani na wamekosa mtaji. Ushauri Wao unaeza kuchukua na ukafanyia kazi ukakutoa. Naunga mkono hoja Kwa hoja yangu kwamba. Unapokuwa UNAPANGA kufanya kitu wakati mwingine Kuna vitu hauviwekei manani Sasa unapokubali Ushauri wa kila mtu uwe mtu WA kupima ni ipi utakusogeza mbele. Akili zinahitaji kukumbushwa
 
Mkuu kama kweli unataka kupiga hatua kwenye jambo lolote ni busara kusikiliza watu bila kijali wana uelewa wa kiwango gani juu ya hilo jambo, ila baada ya kukusanya mawazo ya watu mbalimbali hapo utajua sasa pa kuanzia na kumalizia ,unayemdharau hana ujuzi na kitu fulan anaweza akakupa mwanga wa kuanzia au kutatua changamoto inayokukabili na ukafanikiwa
 
Back
Top Bottom