Ni ushauri tu wana jf wenzangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni ushauri tu wana jf wenzangu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kichenchele, Jun 23, 2011.

 1. k

  kichenchele JF-Expert Member

  #1
  Jun 23, 2011
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 490
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Ndugu zangu wana JF, nawaombeni sana tujaribu kuwa watu wenye mtazamo wa kusaidiana na kuelimishana, ukweli kuna mada zinazoletwa humu ni nzuri na zenye tija na zipo nyingine ambazo kweli zinakuja hazina mashiko, sasa mimi nawaomba ndugu zangu tusaidiane ili mwisho wa siku tupate elimu japo kwa kifupi tu, maana nategemea watu wengi sana wanaaamini Jamii Forum ni mahala ambapo unaweza kuweka mada, tatizo au hata kuomba msaada uwe wa kisheria, kitabibu, kimasomo, kijamii n.k ukawa ni sehemu nzuri ya kuanzia kabla hujaanza kufuata taratibu nyingine zinazotakiwa. lakini kiukweli mtu unapokuwa unaweka mada yenye mantiki harafu badala ya watu kuchangia au kushauri juu ya nini kifanyike tunaleta utani na dharau na hata kutukanana bila sababu zozote za msingi, hali hii inasikitisha sana, nawaombeni wana JF wenzangu tushirikiane kwa nia njema tu ili hata wale tulio na ufahamu mdogo au tusio juwa juu ya mambo mengi yanayoletwa humu tuyaelewe na tuone watalaamu waliomo humu wanasema nini. Ni kweli kila mtu anajiunga JF kwa lengo tofauti na tumeachana kwa umri, elimu, kipato, ufahamu, uwezo wa kuchambua na kuelewa hoja, lakini hili haliwezi kutufanya tushindwe kusaidiana, ningependa kuiomba jamii iliyomo humu ndani ielewe kwamba inafika wakati hata adui yako akaja kuwa rafiki mzuri na rafiki yako mzuri akawa adui mkubwa. Panapoutani tutaniane, na palipo na hoja nzuri basi ni budi tusaidiane ndugu zangu, naomba kuto hoja, Mungu wabariki wana JF- Mungu Ibariki JF .Siku njema.
   
 2. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #2
  Jun 23, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 9,853
  Likes Received: 3,132
  Trophy Points: 280
  hujui kuwa magamba ndio yametumwa kuichafua jf?hilo unalolisema haliwezekani as long as magamba yana unrestricted access to jf,kazi yao ni kumwaga upupu tu humu,..so learn to live with it,..pumba zitajitenga zenyewe na mwisho wa siku watakimbia..
   
 3. k

  kichenchele JF-Expert Member

  #3
  Jun 23, 2011
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 490
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  nashukuru sana
   
 4. Majoja

  Majoja JF-Expert Member

  #4
  Jun 23, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 610
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Pumba za aina hii ndio zinafanya elimu isipande JF.
  Kuna watu wenye mawazo finyu wanaoiona dunia kwa miwani ya CDM na CCM.
  Kwa watu kama hawa kuingia ufalme wa U-GREAT THINKER ni sawa na ngamia kupita tundu la sindano.
   
 5. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #5
  Jun 23, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 17,334
  Likes Received: 3,600
  Trophy Points: 280
  Suala ni kwamba hakunaga hoja nzuri au mbaya always, these are ''relative terms''
  Mfano ukileta hoja ya 'posho kwa wabunge zisiwepo', mtu kama Nape (mfano) atakuambia sio poa wakati mwingine kama mimi (mfano) nitakuambia poa tu zisiwepo, hivyo lazime tulumbane, tunyukane na tutofautiane kwa sana tu
   
 6. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #6
  Jun 23, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 12,806
  Likes Received: 1,592
  Trophy Points: 280
  Mkuu uko sahihi kabisa. Nadhani mtoa hoja hajakataa kulumbana, kunyukana wala kutofautiana. Binadamu lazima tutofautiane na huo ndio ubinadamu. Tatizo ni kwamba mtu anaweza kuweka mawazo yake ambayo ni tofauti na mawazo ya wengine badala ya kumuelimisha kwa hoja utakuta watu wanamshambulia kwa matusi. Ni vyema watu tukalumbana kwaa hoja
   
 7. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #7
  Jun 23, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,743
  Likes Received: 832
  Trophy Points: 280
  hapa tupo wengi,hatuwezi kufanana,wengine wanapenda utani,wengine jeuri,wengine wema,wengine wametumwa
  lakini kwa upande wangu NAPATA ELIMU TOSHA,KILA SIKU NAJIFUNZA MAMBO MAPYA
   
Loading...