Ni usafi Jumamosi au kufunga biashara?

Ni usafi Jumamosi au kufunga biashara?

Ghiti Milimo

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2011
Posts
5,136
Reaction score
7,655
Wadau, wote tunafahamu kuwa, Serikali(Rais)ilitangaza kuwa, kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi, itakuwa ni siku ya usafi kitaifa.

Wananchi, wakalipokea agizo hili, kwa mikono miwili. Lakini, ki-uhalisia, imekuwa ni kero kubwa!

Maisha kwa sasa yamekuwa magumu, wateja nao wamekuwa ni wa shida, patikana yao japo ni wachache, ni asubuhi, pamoja na mzigo wa kodi, lakini siku hii tunalazimishwa kufungua shughuri zetu saa nne na tano asubuhi! Ukifungua kabla ya hapo, unakamatwa!
Cha kushangaza, hao WAKAGUZI, wanachokagua, si USAFI, bali nani kafungua Duka/biashara yake kabla ya muda waliojipangia!

Mimi nawashauri, wangeturuhusu, tuwe tunafanya usafi kwa wakati wetu. Ila wao, wawe na muda maalumu, wa kukagua huo usafi. Kama mimi nitafanya usafi, usiku, alfajiri, hiyo iwe ni juu yangu!

Sina shaka hili tatizo lipo Nchi nzima! Mimi nipo Shinyanga mjini!
 
Duh! Ungewauliza
 
hakuna usafi wowote unaofanywa watu wanakaa nje wanasubiri saa 4...
bora wangesema kila ofisi, duka wahusika wahakikishe mazingira yao ni safi ukaguzi unapita jmosi...ofisi nyingine na maduka yana watu wa usafi maalum wangeendelea na usafi wakati biashara zinaendelea manake uchumi umekuwa tabu pesa hamna
 
Tatizo suala la usafi jumamosi ya mwisho wa mwezi limewekwa kisiasa zaidi.

Na ndio maana utasikia jumamosi hii tutakuwa na mkuu Wa wilaya mara sijui wa mkoa eneo Fulani tukifanya usafi yaani watu tukarundikane eneo Mona eti tukifanya usafi ...ujinga mtupu..

Ni vema kila mmoja afagie eneo lake kuanzia ile saa 12 mpaka SAA moja baada ya hapo kila mtu aende kwenye shughuli zake.

Hii sijui kusema tusifungue biashara mpaka saa tatu ni kukosa mengi, mwisho wa siku wanachotaka ni kodi.
 
Za asubuhi wana bodi.

Nipo najiuliza hapa hili suala la usafi kila jumamosi ya mwisho wa mwezi, najiuliza pesa ambazo wafanyabiashara wanazipoteza kwa kutofanya biashara kwa hayo masaa mawili, najiuliza kodi ambayo serikali inapoteza kwa hayo masaa mawili ambayo shughuli zinazimama kabisa, najiuliza jinsi ambavyo viongozi wa serikali za mtaa wanavyofuatilia kuhakikisha maduka hayafunguliwi ili hali mitaani kwao kuna mambo chungu nzima, mitaa kwao kuchafu mpaka jumamosi ya mwisho wa mwezi, najiuliza jinsi ambavyo polisi wanavyofanya patrol mitaa kuangalia maduka yaliyofunguliwa,najiuliza hivi usafi ni jumamosi ya mwisho wa mwezi tu, hivi usafi ni ratiba ya mwezi au.ni tabia, mila na desturi?
 
Jumamosi kunapokucha mpaka saa nne ni usafi, saa nne mpaka nane ni kubeti (mikeka) na kuanzia saa nane na kuendelea ni EPL au VPL. Sielewi tuendako ukitegemea nguvu kazi ya taifa ndo ifanyacho
 
Daaaa kweli mwenyewe linanikwaza sana hili la kila jmos ukifungua tu duka mgambo wanakuja na kufanya fujo bora wangeruhusu tu tufungue maduka ili tufanye usafi sehemu zetu za biashara hapa nimesubir saa nne naenda kufungua sasa inshapoteza pesa
 
Imenikuta Leo tanga.yaaan in kelo.unaweza kua na Shida mhimu sana ukashindwa kupata huduma.yaan SAA mbili mji maduka yote yamefungwa.kwa kweli hili suala liangaliwe kwa jicho LA tatu.tunaleteana kero zisizo na msingi.very stupid..nmekereka leo adi nikahisi kupasuka kwa hasira
 
Za asubuhi wana bodi.

Nipo najiuliza hapa hili suala la usafi kila jumamosi ya mwisho wa mwezi, najiuliza pesa ambazo wafanyabiashara wanazipoteza kwa kutofanya biashara kwa hayo masaa mawili, najiuliza kodi ambayo serikali inapoteza kwa hayo masaa mawili ambayo shughuli zinazimama kabisa, najiuliza jinsi ambavyo viongozi wa serikali za mtaa wanavyofuatilia kuhakikisha maduka hayafunguliwi ili hali mitaani kwao kuna mambo chungu nzima, mitaa kwao kuchafu mpaka jumamosi ya mwisho wa mwezi, najiuliza jinsi ambavyo polisi wanavyofanya patrol mitaa kuangalia maduka yaliyofunguliwa,najiuliza hivi usafi ni jumamosi ya mwisho wa mwezi tu, hivi usafi ni ratiba ya mwezi au.ni tabia, mila na desturi?
N kufunga maduka na sio usafi maana hata usafi wenyewe haufanyiki,
Na kingine kumbuka serikali haina hasara sema hizo hela ninazozikosa asubuhi na sio kodi za serikali, kwanza serikali inakunyonya na bado unaifikilia we kila kona kodi bado tu unaiwazia, Serikali haina hasara
 
Imenikuta Leo tanga.yaaan in kelo.unaweza kua na Shida mhimu sana ukashindwa kupata huduma.yaan SAA mbili mji maduka yote yamefungwa.kwa kweli hili suala liangaliwe kwa jicho LA tatu.tunaleteana kero zisizo na msingi.very stupid..nmekereka leo adi nikahisi kupasuka kwa hasira
Kuna ndugu Leo asubuhi alikuwa ana shida ya hela ya haraka aiseee naenda vibanda vya kuwekea hela nakuta vimefungwa
 
Back
Top Bottom