Katika kipindi cha Jukwaa kwa wasiokua na jukwaa kinachorushwa hewani na Radio Kheri saa tatu hivi jana walizungumzia kadhia ya kupigwa risasi sheikh Ponda,Pamoja na mambo mengine walizungumzia utata wa Jeraha la Shk Ponda kwa namna lilivyoripotiwa na vyombo vya habari vya Tanzania na vya nje, Sheikh Bassaleh akiwa mgeni wa jana, aliweka wazi kauli zinazokinzana kutoka kwa Kamanda Shiyogile, ambaye kwa magazeti ya ndani yamemripoti anadai kwa nyakati tofauti kuwa hawahusiki na jeraha la Shk Ponda, yeye huyohuyo alipokuwa akihojiwa na gazeti la Uingereza alieleza kuwa wamepiga risasi katika juhudi za kumkamata Shk Ponda wakimhusisha na tukio la kumwagiwa Tindikali Raia wawili wa Uingereza huko zanzibar.
Aliendelea kuweka wazi jinsi mashirika, taasisi mbalimbali na vyama vya siasa (sio CCM) Vilivyolaani tukio la kupigwa risasi kwa Shk Ponda, na kutaka tume huru iundwe ili wahusika wachukuliwe hatua stahiki.
Katika hali isiyo ya kawaida na kinyume kabisa na haki ya kupata matibabu, na pamoja na daktari kutoa siku 14 za matibabu hospitalini ili jeraha la sheikh Ponda lipone, Polisi walimchukua Sheikh Ponda(na kidonda kibichi) na kumpeleka Gereza la Segerea, wakisindikizwa na Defender 6 za polisi.
Kwa kuwa kiofisi polisi wanakana kumpiga risasi Shk Ponda, na kwamba wanamaanisha ni tukio la kihalifu kama matukio mengine ya uhalifu. Na kwa kuwa sheikh Ponda ni kiongozi wa juu (katibu wa jumuia na Taasisi za kiislamu Tanzania) wa kiimani mwenye ushawishi mkubwa kwenye jamii ya kiislamu Tanzania, narejea jana kwa msikilizaji aliyehoji kama kuna kiongozi yeyote kutoka chama kinachotawala au kutoka serikalini amelaani kitendo cha kinyama cha kutaka kuuliwa kwa kwa risasi kwa sheikh Ponda? Jibu ni hapana.
Km ilivyo kwa msikilizaji wa radio, nami sijamsikia, ukiachilia mbali mtoto wa malechela (ambaye inadaiwa ni kiongozi wa chini wa CCM) aliyeibuka na kumtukana Sheikh Ponda kwa kumwita Mende kwenye jukwaa hili, na kwa ukimya wa CCM labda hilo ndio tamko lao! Mtoto huyo alipotakiwa na wanajukwaa wenye busara alete ushahidi wa uchochezi wa Shk Ponda hakuweza kujibu lolote kuonesha kuwa anasukumwa na chuki binafsi dhidi ya waislamu na uislamu.
Matukio la kupigwa risasi kwa viongozi wa dini hasa Mapadri kutoka kwa watu wasiojulikana yametokea na mara zote viongozi wa juu wa chama na serikali wamekuwa wakitoa matamko makali sana, kwa kifupi watawala, watawaliwa, vyama vyote vya upinzani na taasisi zisizo za kiserikali waliungana kwa kulaani matukio hayo. Hoja hapa ni kwa nini serikali na chama tawala baada ya kukana kuhusika hawajatoa tamko lolote kulaani unyama huu kama walivyotoa kwa viongozi wengine wa dini?
Je serikali itakwepaje madai ya waislamu kuwa ilitaka kumuua Shk Ponda? Ili kuzima madai ya waislamu (yanayorudiwa na Shk Ponda mara kwa mara) kwamba inaendeshwa na mfumo Kristo, mfumo ambao huwafanya waislamu kuwa raia wa daraja la pili: Wao ni kudharauliwa kwa kila jambo lao,walikataliwa ushauri wa kujiunga na OIC, wakatupiliwa mbali mahakama ya kadhi,wanafelishwa kwa kusudi na baraza la mitihani, hawaruhusiwi kuhoji MOU kati ya serikali na makanisa inayoilazimu serikali kuzipa mabilioni ya fedha za taasisi za kikristo, waliuliwa Mwembe chai na sasa anataka kuuliwa Sheikh Ponda kwa ajili ya kusimamia madai ya waislamu.
Tunangoja matamko kama yale yaliyojaa simanzi na hasira (watakamatwa mara moja na kufikishwa kwenye mikono ya dola ) kutoka kwa viongozi wa juu wa kiserikali alipopigwa Padri Mushi risasi na watu wasiojulikana! NAWASILISHA