Ni uongo upi usio na mantiki umewahi kutana nao kwenye Bongo Movie?

Mahindaa maidotaaaa nikupe nini mama yaangu

MZEE-MAGARI.jpg
 
Kaangalie hizi uje na mrejesho wako;

Moses
Dar to Lagos
She is my Sister
Village Pastor
Uncle JJ
This Is It
Renthal Poison
Hazina ya Kanisa
Devil Kingdom
Magic House
Fake Smile
na nyingine kibao 🤣🤣🤣🤣
 
Watanzania ni watu wazarendo sana kwa vitu vilivyo vya kwao! Lakini inafikia mahali wawasilishaji wanaviwasiliaha kimakosa!

Uwanja pekee ambao kwa sasa umefifia na uko karibu kufa ni katika tathnia ya filamu za kitanzania (maigizo), walibaki wakina mama kuwa watazamaji na mashabiki wao! Lakini kwa sasa na wao wamehamia kwenye series za kikorea!

Huwezi amini kuwa makosa kwenye tathnia hii yalikuwepo hata kipindi cha uigizaji wa Steven Kanumba! Japo kwa asilimia ndogo sana!

Twende kwenye kiini
Tufahamishe uongo wowote uliokutana nao kwenye bongo movie ambao ulikukata stimu za kuendelea kuzifuatilia!

Kwa kuanzia, mtu kuflash back na kukumbuka matukio yaliyofanyika ambapo yeye hakuwepo! Mtu anakumbuka, halafu kwenye tukio hayupo!
Kuna movie moja nyoka anatembea kama garimoshi
 
Halafu na ile watu wasiohusika kushangaa shangaa wakat movie ikishootiwa mpaka wanatokea kwenye movie na mishangao yao inabd waanze kuweka traffic control wakati wa shooting
 
Mimi ukiachana na maswala ya uongo ..nitazunguzumzia maswala ya makosa ya kiufundi kama editing n.k.

Kwa mfano cinematographic technique bado sana ...kumbuka hata mjongeo wa kamera katika kurekodi tukio huvuta hisia kwa mtazamaji.

Unakuta tukio labda la kukimbia ni kamera moja peke yake inatumika..hivyo kukosa baadhi ya angle kwenye scene.

Kwenye editing pia unakuta boom mic inaonekana. na mambo mengi kibao tu
Sometimes cameraman naye ankimbia na camera yake
 
Kuna hiyo bongo movie niliangalia sikumbuki inaitwaje

Kulikua na huyo mwanafunzi anasoma shule mazingira magumu wanafunzi wenzake wanamcheka sasa wakaonesha baada ya miaka kumi yule mwanafunzi amefanikiwa ana majumba magari akarudi shule aliyosoma kuwapa ushuhuda wanafunzi ila cha ajabu wanafunzi wenyewe ndo wale wale waliokua wanamcheka zamani
Alihitimu akawaacha wenzie
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom