Ni uongo upi usio na mantiki umewahi kutana nao kwenye Bongo Movie?

Melki the Storyteller

JF-Expert Member
May 3, 2022
5,701
9,779
Watanzania ni watu wazarendo sana kwa vitu vilivyo vya kwao! Lakini inafikia mahali wawasilishaji wanaviwasiliaha kimakosa!

Uwanja pekee ambao kwa sasa umefifia na uko karibu kufa ni katika tathnia ya filamu za kitanzania (maigizo), walibaki wakina mama kuwa watazamaji na mashabiki wao! Lakini kwa sasa na wao wamehamia kwenye series za kikorea!

Huwezi amini kuwa makosa kwenye tathnia hii yalikuwepo hata kipindi cha uigizaji wa Steven Kanumba! Japo kwa asilimia ndogo sana!

Twende kwenye kiini
Tufahamishe uongo wowote uliokutana nao kwenye bongo movie ambao ulikukata stimu za kuendelea kuzifuatilia!

Kwa kuanzia, mtu kuflash back na kukumbuka matukio yaliyofanyika ambapo yeye hakuwepo! Mtu anakumbuka, halafu kwenye tukio hayupo!
 
Mimi ukiachana na maswala ya uongo ..nitazunguzumzia maswala ya makosa ya kiufundi kama editing n.k.

Kwa mfano cinematographic technique bado sana ...kumbuka hata mjongeo wa kamera katika kurekodi tukio huvuta hisia kwa mtazamaji.

Unakuta tukio labda la kukimbia ni kamera moja peke yake inatumika..hivyo kukosa baadhi ya angle kwenye scene.

Kwenye editing pia unakuta boom mic inaonekana. na mambo mengi kibao tu
 
Kama miezi mitatu iliyopita nilikuwa kwa mshkaji kuna mchezo unarushwa na azam

Jamaa anagombana na mkewe kamtupia mabegi nje akaondoka
kwenye screen wakatuambia baada ya miezi sita hi cha kushangaza demu karudi na dela lake na mtandio uleule kupiga hodi jamaa anatoka na kipensi kilekile na vesti ile ile ilibidi tugairi kuangalia huo ujinga
 
Kuna hiyo bongo movie niliangalia sikumbuki inaitwaje

Kulikua na huyo mwanafunzi anasoma shule mazingira magumu wanafunzi wenzake wanamcheka sasa wakaonesha baada ya miaka kumi yule mwanafunzi amefanikiwa ana majumba magari akarudi shule aliyosoma kuwapa ushuhuda wanafunzi ila cha ajabu wanafunzi wenyewe ndo wale wale waliokua wanamcheka zamani
 
Duuh hii kali hakika Bongo muvi Kuna vitimbi asee😁
 
Kinachokera zaidi kwenye kukumbuka matukio ya nyuma ni pale ambapo..

Anapoanza kumsimulia mwenzie kilichotokea zamani, anaangalia darini na kidole juu ya pua baada ya hilo tukio kuoneshwa anashusha macho toka darini kumrudia anaezungumza nae na kusema "ndo ilivyokuwa" kana kwamba wote waliwekewa screen ya tukio darini
 
Kuna hiyo bongo movie niliangalia sikumbuki inaitwaje

Kulikua na huyo mwanafunzi anasoma shule mazingira magumu wanafunzi wenzake wanamcheka sasa wakaonesha baada ya miaka kumi yule mwanafunzi amefanikiwa ana majumba magari akarudi shule aliyosoma kuwapa ushuhuda wanafunzi ila cha ajabu wanafunzi wenyewe ndo wale wale waliokua wanamcheka zamani
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom