EWGM's
JF-Expert Member
- Jul 22, 2013
- 1,521
- 2,112
Uzalendo kwa Tiafa langu la Tanzania unanifanya naandika haya kwa uchungu mkubwa lakini ni ukweli usiopingika kuwa Kenya ndiyo taifa baba la Afrika Mashariki na Kati. Nakubali kabisa ndani ya Kenya kama taifa wanamatatizo yao mengi tu. Ila linapokuja swala linalohusisha mambo ya nje ya mipaka ya taifa lao, Kenya huwa hawateteleki na wanaungana kwa pamoja na kuwa kitu kimoja. Kwenye maslahi kwa taifa lao huwa wanaweka utashi mbele na tofauti zao pembeni tayari kupigania hadhi na heshima ya taifa lao kwa nguvu zote.
Taifa lenye sifa za uongozi kwa wengine huwa na hurka ya kufanya kila liwezalo kuwa juu ya wengine kiuchumi, kimaendeleo na kuonyesha ushindani kwenye kila nyanja na sekta. Japokuwa na mikwaruzo yao waliweza kukaa na kutunga katiba mpya inayoendana na mazingira ya dunia ya sasa. Viongozi waliopewa dhamana ile ya kutunga katiba waliheshimu kila kitu wananchi walichopendekeza na bado kuna mkakati wa kuiboresha zaidi.
Ijapokuwa tuliwashinda kwenye figisu figisu ya bomba la mafuta lakini kama Taifa baba la Afrika Mashariki wameendelea na ule mchakato wao na bila kujali maamuzi ya Uganda ya kushirikiana na Tanzania. Kwa miaka 15 iliyopita Kenya imekamilisha mipango mingi ya maendeleo wakati sisi tunazidi kutumia mtindo wa kuziba vilaka. Pia hurka za Taifa baba ni pale unapoona majanga kwa nchi jirani au zenye maslahi kwake huwa wanakuwa wa kwanza kusaidia na kuonyesha uwakilishi wao, tumeona kwa Kenya ikitenda kwa Sudan ya Kusini, Somalia, Uganda na Tanzania pia.
Unapokuwa Taifa baba mara nyingi maraisi wa mataifa mengine huwa ndiyo wanakuja nchini mwako kutia sahihi kwenye vitabu vya wageni na kujitambulisha uwepo wao kwenye nchi zilizo chini yako. Tumeona Magufuli pamoja na kupinga kwake safari za nje alipanda ndege kwenda Kenya kutia sahihi kitabu cha wageni. Tumeona michango mingi kutoka kwa viongozi wetu wakiitaja Kenya kama ni kipimo kwa taifa letu tunapotakiwa tuwe, hivyo hii ni ishara tosha kuwa wao ni taifa baba na viwango walivyoweka ni tunavyotamani tuvifikie.
Ni mtazamo wangu na utaendelea kuwa ukweli halisi kwa nchi yetu na watoto wetu kwenye siku nyingi zijazo.