Unatakiwa kwenda ofisi yoyote ya Uhamiaji then ukifika pale watakupatia barua ya kupeleka serikali yako ya mtaa kwa ajili ya utambulisho ukisharudisha hiyo barua then atapatiwa form za kujaza kwa ajili ya kuaply passport, form hizo nadhani kama hawajapandisha bei ni elfu hamsini tu.Ukishamaliza kuzijaza utazirudisha uhamiaji then utachukuliwa alama za vidole.Kama upo Dar ni ndani ya wiki unapewa passport kama upo mkoa naskia inaweza ikawa wiki mbili mpaka wiki nne.All the best nakutakia safari njema maana sisi waTanzania bwana ukisikia mtu anatafuta hiyo kitu ujue anasafiri tu