#COVID19 Askofu Gwajima: Ni ujinga kuruhusu Taifa zima kuwa 'Experiment' kwa sababu tuna haraka ya Corona

Kwa nini tusifast track majaribio ya chanjo ya ukimwi pale Muhimbili?
Nyie mlimdanganya mwendazake kwa mapambio yenu mpaka mkampa na kombe eti la ''kushinda corona'' mkampoza akajiamini akidhani haitampata. Ona alivyoishia mwisho mbaya tena kwa corona hiyo hiyo ilivyofanya zake. Unadahni virus wa corona na ukimwi ni sawa? Someni basi ili angalau mkiandika ime-make sense.
 
Jamani US wameanza mchakato wa kuomba patent zilegezwe ili manufacturers wa chanjo waongezeke.

Sasa nilitegemea wabunge waombe serikali ipewe patent ili tuwe na pattern zote sie tutengeneze chanjo yetu. Sie tumekalia kulalamika tu na kukosoa chanjo kila siku.

Kwani nani amekataza waTZ kuwa na chanjo yetu? China wanatumia chanjo za UK? mbona EU haijawekea vikwazo nchi yao?

Huyu jamaa toka apotoshe eti 5G ndio inaleta Covid 19 na akaahidi Covid 19 itaishia kenya haitowahi tua Dar najiuliza nani bado anamuamini?? Kama nabii tu hawezi kupatia ubashiri je hta uchambuzi tu ndio ataweza.

Masuala ya kitaaluma tuachie wataalam ni hatari sana HKL kujadili epidemiology
Chanjo yetu ya nyungo ilikuwa the best medically and psychologically. Kwani hatukuwa na fatalities nyingi na pia social interactions ziliendelea kama kawaida. That was the best vaccination ever
 
Mbunge wa Jimbo la Kawe, Askofu Josephat Gwajima ametaka kuwepo umakini wa kuchagua Chanjo dhidi ya Ugonjwa wa COVID-19. Amesema hayo akiwa Bungeni Dodoma leo wakati wa Mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Afya iliyowasilishwa na Waziri Dorothy Gwajima.

Amefafanua, "Mimi sipo kinyume na Chanjo za Corona wala Chanjo yoyote. Mtu asininukuu napinga Chanjo, hapana! Tanzania tulishachanjwa Chanjo ya Kifua Kikuu, Surua, Kifaduro na Polio".

Amesema ni kweli Tanzania ikikataa Chanjo inaweza kuwekewa zuio la kwenda Ulaya. Ameeleza, "Tunakabiliwa na uchaguzi mbaya sana, tuchanjwe kitu tusichokijua sawa sawa au tusichanjwe tuzuiwe kwenda Ulaya".

Ameiomba Wizara ya Afya kuangalia suala la Chanjo kwa umakini, akisema waangalie madhara ya sasa, ya siku zijazo na ya Taifa. Ameongeza kuwa, tatizo lililopo ni kufikiri kila kinachotoka Ulaya kinafaa.

Amesema, "Before we venture into what kind of vaccine we should take, tunatakiwa tuwe na wataalamu wetu wa hapa".
Kwa hiyo huyu Askofu leo amekuwa Dr
 
Huku mtaani kwetu sijui tutamvika nani maana kwa hiari ni ngumuuuu
Haya yote yamesababishwa na JPM kupenda kupotosha kila kitu ni mabeberu!! Kiufupi hatochanjwa mtu maana watu wameshalishwa uongo kama enzi zile wakiona gari la Red cross wanasema wanyonya damu!!

Hapa kilichopo ni kuomba patent tutengeneze NEMC pale ndio watu watatumia.
 
Homa ya manjano ile Vaccine yake imeua watu zaidi ya laki 5 directly kabisa tokea iwe introduced mbona sijasikia mkiipiga marufuku na ndio kwanza tunatumia hiyo kila tukisafiri nje!!

Mkatae kwa sababu tu hamtaki ila msijustify eti madhara cjui nini.... Coz ikiwa hivyo inapaswa mpaka Radiotherapy isitishwe pale ocean road maana ile madhara yake ni makubwa sana kwa kila anayetumia tiba ile.

Tuache double standard
Ingawa kondoo hajawahi kubadirika akawa mbuzi, Ila ni mhimu kutambua, Kuna mabadiriko hufanyika Kati ya kondoo wa miaka ishirini iliyopita na kondoo wa Leo na atakayezaliwa Kesho
Hatuwezi kuuishi ukondoo wa miongo miwili iliyopita
 
hivi watalaamu wetu wa ndani wana capacity ya kujua ubora, udhaifu, madhara, faida ya cnanjo zilizopo kwa sasa na years to come?
Achana na huyu tapeli. Aulizwe dawa anazotumia mpaka simu aliyotumia kujichukuwa clip wakati anafanya uashereti si zimetengenezwa huko huko? Akatae na hizo basi.
 
Chanjo yetu ya nyungo ilikuwa the best medically and psychologically. Kwani hatukuwa na fatalities nyingi na pia social interactions ziliendelea kama kawaida. That was the best vaccination ever
But naibu waziri alikiri nyungu haikusaidia kitu...... Naamini yeye ana takwimu kuliko mimi na wewe.
 
Homa ya manjano ile Vaccine yake imeua watu zaidi ya laki 5 directly kabisa tokea iwe introduced mbona sijasikia mkiipiga marufuku na ndio kwanza tunatumia hiyo kila tukisafiri nje!!

Mkatae kwa sababu tu hamtaki ila msijustify eti madhara cjui nini.... Coz ikiwa hivyo inapaswa mpaka Radiotherapy isitishwe pale ocean road maana ile madhara yake ni makubwa sana kwa kila anayetumia tiba ile.

Tuache double standard
Point yako haina mashiko, chanjo ya homa ya manjano imekuwepo kwa zaidi ya miaka 70, na tafiti nyingi zimefanyika zikishirikisha nchi nyinyi Tanzania ikiwemo. Leo hii nionyeshe nchi ambayo inazalisha chanjo ya Corona walikubali kumshirikisha mtu au nchi yoyote ambayo inanunua chanjo ya corona. Unachopewa ni chanjo na kuambiwa tuambia hao uliowachanja wamepata madhara gani. kwa kifupi we are guinea pigs na mtu kama wewe unakubali tu. Nchi kama Kenya na Rwanda walikuwa wanashangilia walipopewa chanjo, soon after, side effects zikanaza kujitikeza kila kona. Leo hii wao wanahali mbaya kuliko sisi ambao we didn't care less.
 
Ingawa kondoo hajawahi kubadirika akawa mbuzi, Ila ni mhimu kutambua, Kuna mabadiriko hufanyika Kati ya kondoo wa miaka ishirini iliyopita na kondoo wa Leo na atakayezaliwa Kesho
Hatuwezi kuuishi ukondoo wa miongo miwili iliyopita
So una support Yellow card zipigwe marufuku? Ama ww hutaki tu chanjo ya Covid pekee ila uko tayari kwa Yellow card?
 
Haya yote yamesababishwa na JPM kupenda kupotosha kila kitu ni mabeberu!! Kiufupi hatochanjwa mtu maana watu wameshalishwa uongo kama enzi zile wakiona gari la Red cross wanasema wanyonya damu!!

Hapa kilichopo ni kuomba patent tutengeneze NEMC pale ndio watu watatumia.
Kabla huajawaambia wavae barakoa wao wanakuambia tangu mwaka jana wanafanya biashara zao kariakoo sokoni, tandika, karume na hakuna aliekufa kwa hiyo corona

Sasa hapo ujipange kuwapa sababu inayoeleweka
 
Wapuuziaji watampinga.
Nazidi kuona maono mema ya Hayati Magufuli, alipambana sana Gwajima aingie bungeni. Jamaa yupo vizuri kichwani.
'Nileteeni Gwajima, Nileteeni Gwajima, Nileteeni Gwajimaaaaaaa!"
 
Point yako haina mashiko, chanjo ya homa ya manjano imekuwepo kwa zaidi ya miaka 70, na tafiti nyingi zimefanyika zikishirikisha nchi nyinyi Tanzania ikiwemo. Leo hii nionyeshe nchi ambayo inazalisha chanjo ya Corona walikubali kumshirikisha mtu au nchi yoyote ambayo inanunua chanjo ya corona. Unachopewa ni chanjo na kuambiwa tuambia hao uliowachanja wamepata madhara gani. kwa kifupi we are guinea pigs na mtu kama wewe unakubali tu. Nchi kama Kenya na Rwanda walikuwa wanashangilia walipopewa chanjo, soon after, side effects zikanaza kujitikeza kila kona. Leo hii wao wanahali mbaya kuliko sisi ambao we didn't care less.
Kwanza tukubaliane homa ya manjano pia chanjo yake ina side effects nyingi na nimekueleza kwa takwimu za WHO watu zaidi ya laki 5 wamekufa kwa chanjo-related cases!! Kwahyo nachohoji kwanini hampigi marufuku na ile? Au ni double standard

2. China wametengeneza chanjo yao na juzi tu hapa WHO wameipa endorsement kuwa ipo effective. Kwanini sisi hatutengenezi yetu tumekalia kulaumu wazungu na chanjo zao? Mbona Russia au China hawalii lii juu ya mabeberu conceding chanjo?

3. Side effects zipo kwa dawa na cjanjo zote duniani hakuna dawa hata moja haina side effects kutokana na variation kwa hali za miili ya watu. So sio chanjo ya covid tu ndio yenye madhara..... Ndio maana nimetoa mfano wa Radiotherapy pale ocean road ile tiba ukiitumia inakumaliza kabisa baadhi ya viungo lakini haipigwi marufuku coz hakuna namna nyingine ila humu huwezi sikia mkijadili mnaaminishwa ni chanjo tu yenye side effects ila ARVs cjui Yellow fever vaccine na Radiotherapy aaah ni sawa tu!!
 
Hapana mkuu mie nimejifunza kuheshimu taalum hivi kweli madaktari bingwa wa WHO kuanzia yule mama wa kihindi ambaye ni top expert wa epidemiology duniani yaani hajui hayo anayosema Gwajima?

Ukisikia mjenzi wa daraja anatumia miezi 6 kufanya upembuzi watu huwa wanatukana mitandaoni kwamba miezi 6 yote kufanya upembuzi??? Lakini ukikaa na mtaalam atakueleza kwanini miezi 6 maana kuna movement za kitectonic, ama misimu ya mvua ukipita n.k ndio utaweza kujua stability ya eneo husika kujengewa daraja n.k

So nadhani tukiheshimu taaluma za watu nchi itafika mbali. Maadam Rais kaunda tume yenye wataalam husika then watakacho recommend tuheshimu otherwise ujuaji haujatusaidia mpaka hii Leo.
Uko sahihi. Viongozi wa juu kule WHO wako 21. Wote 21 wana elimu ya PhD ya magonjwa haya. Wanne (4) ni Waafrika. Wawili (2) ni Marekani na Carribean weusi. Kuna huyo mama wa Kihindi na mama mwingine wa kiarabu wa Saudia. Watu hao ni wasomi, na wengi ni wenzetu. Elimu halisi ya Gwajima ni Form IV. Anamcheka mwenziye Makonda, lakini hana ground ya kumcheka. Kusema tuache kusikiliza wataalamu unaowasema eti twende na Gwajima.....! Yule Rais aliyetangulia ameharibu akili za watu. Amewaambia wakatae elimu, warudi walivyokuwa babu zao, na watu wanamfuata hadi sasa. Zindukeni!
 
So una support Yellow card zipigwe marufuku? Ama ww hutaki tu chanjo ya Covid pekee ila uko tayari kwa Yellow card?
Namshukuru Mungu amenipa mibaraka mingi nikiwa hapa hapa, ima iwe ni ushamba, lkn iwe iwavyo, sichanjwi na simshauli mwingine aige Imani yangu!!

Nilichotaka kusema, Gwajima ametahadharisha kuhusu kamati iliyopewa kufanya utafiti wa hizi dawa na Corona, niliyemu quote alimshambulia Kwamba, mbona Chanjo za magonjwa mengine mengi tuluchanjwa, na Kwa nini sasa iwe ni kuhoji kuhusu ubora wa dawa hizi ilihali hatuna uwezo wa kujitengenezea?

Nikasema, mambo hubadirika, na hatuwezi kuishi kama tupo nyuma ya miaka Elfu iliyopita
 
Back
Top Bottom