Ni Ugonjwa au uchafu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni Ugonjwa au uchafu?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by NGULI, Nov 20, 2009.

 1. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #1
  Nov 20, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Nilikuwa najiuliza kila saiku kwa nini vijana wengi wakitoka tu chuo Mungu akiwajalia kazi wakikopa tu cha kwanza gari nilidhani ni ubishoo kumbe ni swala la msingi achana na adha ya usafiri kuwa wa shida pia mazingira ndani ya gari yanasikitisha.

  Kwa mfano utoke posta mchana uwe unaelekea feri au mbagala au hata basi za mwenge usimame umkute mtu aliyeshiba vizuri/mnene mbele yako then anyooshe mikono kujishika kwenye bomba au kiti harufu kali ya kwapa itakayotoka utatamani ushuke utembee kwa miguu. Je huwa watu hawaogi au ni ugonjwa unaohitaji dawa? Kondacta akiwa anapita kukusanya nauli ndio balaaaa kabisa wengine utazani wanatembea na jalala akinyoosha mkono tu unatoa hela hapo hapo hata chenchi hutamani irudi.

  Na kuna wengine wanaotoa harufu mwili mzima mpaka viatu japo amevivaa sijui akivua nini kitatokea. Inakera sana,
   
 2. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #2
  Nov 20, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Ni hulka tu ya uchafu njia za huko wala sio ugonjwa. Mbona magari yanayoenda Masaki wadereva na makonda wao ni wasafi.
   
 3. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #3
  Nov 20, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,034
  Likes Received: 23,790
  Trophy Points: 280
  Hahaha! Kama limetokea feri, usisahau na shombo la samaki hasahasa kwa ma DCM yaendayo Mbagala.
   
 4. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #4
  Nov 20, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Unajua sisi Mungu anatulinda sana na Magonjwa.......
   
 5. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #5
  Nov 20, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hahahahaha joto kali mpwa unafikiri huyo haogi? Anaoga sana asubuhi na jioni sema wengi wa vijana hawapendi kutumia manukato makali ya kuficha harufu yeye akisha oga basi ndo imetoka hiyo kikwapa kina tabia ya kuchacha na hili joto kikichacha akiinua mkono mtakimbiana utahisi kajamba.
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Nov 20, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Those guys dont love their job!

  Na ukitaka kuiona kazi yako mbaya, basi anza kuidharau wewe mwenyewe!

  Mimi kila siku huwa najisemea kuwa, hivi hawa makonda wangekuwa wanajitahidi wavae hadi tai siku mojamoja, ndhani hata trafiki wasingewashikashika, maana wangeonekana wastaarabu japo kwa minimum grade!
   
 7. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #7
  Nov 20, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Ha ha ha ha,

  Inabidi watu wa manukato wagawe bure kama promo ili wazoee jamani hali ni mbaya, mitaro michafu watu wanatema tuishi wapi sasa?
   
 8. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #8
  Nov 20, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  PJ hata mie nashangaa watz wanavyopenda kuiga wanayoyaona kwenye runinga! Hawajaona tu madereva na makonda wa majuu wanavyotinga suit na tie? wako bling bling!
  Ila joto la bongo nalo mhhh!Labda kama magari yatakuwa na AC lakini bei nayo ikipanda watz watakubali?
   
 9. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #9
  Nov 20, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  lakini si kila anaemaliza chuo ananunua gari!mwingine ananunua TUKUTUKU:D
   
 10. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #10
  Nov 20, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,034
  Likes Received: 23,790
  Trophy Points: 280
  Hahaha! Lakini hakusema chuo gani. Kuna vile vya miezi mitatu unapata international Advanced Diploma!
   
 11. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #11
  Nov 20, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Ha ha ha aha ha[​IMG],[​IMG] nimecheka hapa ofisini hadi watu wameniona kichaa, kwa atakayekuelewa atacheka sana ngoja XSPIN na Fidel80 warudi hapa.
   
 12. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #12
  Nov 20, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0

  Ukishaoga vizuri unahitaji kuficha harufu ipi tena kwa manukato makali?

  Au una maana kutumia anti-perspirants/deodorants..... hizi ni za kukuweka ubaki fresh lakini siyo kufunika uvundo.
   
 13. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #13
  Nov 20, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135

  Da ni kweli kwa sababu mtu akiwa anatema harufu kali then achanganye na manukato mchnganyiko utakao tokea hapo utakuwa worse.
   
 14. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #14
  Nov 20, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  sasa mpwa unacheka halafu unasahau SENKSI!mpwa bwana!
  vipi unalizungumziaje tukutuku?hasa likiwa halina breki zote na linatoa sauti kubwa?
   
 15. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #15
  Nov 20, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,034
  Likes Received: 23,790
  Trophy Points: 280
  Halafu nyumba zenye huruma za kusimamia zikakosekana. Halafu nyuma uwe umepakia mziki wa Carmel! Hahaha!
   
 16. GP

  GP JF-Expert Member

  #16
  Nov 20, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  HAHAAAAA, TUKUTUKU LINASEVU SANA, wataalam wanasema linaadvanteji nyingi kuliko motokaa, kasoro kwenye mvua!, asee unakumbuka ule MSHIKAKI wa siku ile?, duh.
   
 17. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #17
  Nov 20, 2009
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,168
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145

  ni ugonjwa!
   
 18. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #18
  Nov 20, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,034
  Likes Received: 23,790
  Trophy Points: 280
  Si utani; Biashara ya foleni unaitupilia mbali. hakuna kero mbaya kama foleni. We na kistaleti chako unatoka home kuwahi kikao sinza unamkuta mzee wa tukutuku kashatafuna kokoto kadhaa na taska ya nne. Hahahaha!
   
 19. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #19
  Nov 20, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  huyu mpwa anasifia magari anasahau tukutuku bana!wakati chawote tukipaki pale tunaonekana kama miungu-watu
   
 20. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #20
  Nov 20, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  hapa tukutuku linakuwa kama JEEP!linayeya vibaya
   
Loading...