Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
Nionavyo na mimi ndiye chimbuko la haya maoni TUNDU LISSU ndiyo habari ya mjini na URAISI haukwepeki kabisa kupitia karata ya UKAWA 2020.
Na huu ni mlolongo wa sababu zangu:-
1) UMRI.
Lowassa hana mvuto sijui ni afya au umri wapigakura wengi hawamwoni mkakamavu wa kuyafanya yale MAAMUZI MAGUMU ambayo amekuwa akihimiza yafanyike.
Ikumbukwe katika uchaguzi wa 2020, karibu 70% watakuwa vijana kwa maana ya umri wa kuanzia 18-55
Magufuli naye anaonekana ni habari ya jana. Anajaribu aonekane ni kijana lakini kitaswira na matendo hana mvuto. Teuzi zake nyingi zinabagua na kuwanyanyapaa vijana na kama kateua vijana ni kuzijenga familia za wanasiasa awaonao ni jembe kwake kisiasa.
2) KUTENDA HAKI
Tundu Lissu kwa nyakati zote yuko upande wa wale wanaonewa huku Lowassa bado anaiota CCM.
Lowassa hasikiki na hana majibu ya kero za vijana. Mfano kwenye tatizo la ajira analiita Bomu linaloweza kupasuka wakati wowote lakini yuko bubu kwenye ufumbuzi wake. Kwenye mazingira ya namna hii anakosa mvuto wa kisiasa.
Magufuli yeye ni mpiga debe wa BOENG na BOMBARDIER pesa alizolazimisha kuwatajirisha makampuni tajwa zimeongeza ugumu wa maisha ya vijana nchi nzima. Badala ya kuwapa mikopo ya riba isiyozidi 5% kwa mwaka kwa kutumia mabilioni tajwa na kuwawezesha vijana wapunguze makali ya maisha yeye amekuwa akihimiza walipe kodi ambazo hawana.
Pia kupitia sheria ya kodi kainua viwango vya kodi na kupanua maeneo yake na kusababisha biashara nyingi kufa na kuongeza vijana kupoteza ajira.
Kwenye mwelekeo huu tegemea Magufuli kupata mapokezi hasi kama yale ya Mbeya 2015 kwenye kampeni za 2020.
Hii yathibitisha bila ubishi wowote kaulimbiu yake ya 'HAPA KAZI TU' ni pingamizi kubwa kwa "HAPA HAKI TU" Bila haki, taifa lolote hudimia. Magufuli katanguliza mkokoteni na farasi ambao ndiyo haki yenyewe kawaacha nyuma.
Hiyo safari hajaianza na kamwe hataianza na ninahisi hili analijua ndiyo maana hupayuka hovyo kututisha tusimulike mapungufu yake ambayo ni mengi mno!
3) USIKIVU.
Tundu Lissu ana mawasiliano na unyenyekevu mkubwa na ndiyo maana iwe ni ushindi wa Tsunami ndani ya TLS huku watawala wakimwekea vikwazo debe au kukubali kuishauri jamii kwenye mambo mbali mbali ya kisheria au kuwatetea wahanga mahakamani bila kujali kipato imemjengea sifa za usikivu, uvumilivu na unyenyekevu sifa muhimu za uongozi ambazo ni adimu mno kwenye ulingo wa watawala wetu katika nyanja mbali mbali.
Lowassa huko nyuma alikuwa anatoa misaada ya minoti lakini siku hizi kapoa sana sijui kaishiwa au kachoka au kaona hailipi au hana siha tena. Tatizo ni kuwa mchango wake kati ya 2015-2017 ni kiduchu na hivyo kukosa hoja ya kuteuliwa na chama chake na kugombea URAISI
Magufuli yeye anawajenga maprofesa na madokta wengi wao wana makabrasha lakini hawana uzoefu wowote kwenye kazi anazowateua na matokeo yake wanatumia ngwe hii kujifunza hayo majukumu siyo kuleta ufanisi au tija kwani kazi hata hawazijui!
Mbali ya bomoa bomoa bila fidia Sera aliyoianzisha akiwa Waziri ikilenga kumfilisi mnyonge hamjali mnyonge hata kidogo. Nafasi nyingi za kumjali mnyonge hakuzitumia bali kuthibitisha yeye ni wa daraja la juu na hao wa daraja la chini watajijua. Iwe chaguzi ndani ya CCM, iwe ni teuzi, iwe ni kuwafidia wahanga wa majanga kama tetemeko au njaa Magufuli hamjali mnyonge na hao ndiyo wenye karata ya kuamua nani kuliongoza taifa hili mwaka 2020-2025.
HITIMISHO.
Lowassa kama kweli ni mpenda mabadiliko basi ni vyema akatambua hana sifa za kuushinda URAISI mwaka 2020. Ni vyema akawa kama Seneta Edward Kennedy wa Massachusetts (marehemu sasa) ambaye pamoja na kugombea URAISI wa marekani mara kadhaa na kushindwa alizisoma alama za nyakati mwaka 2007 na kumtangaza Barrack Hussein Obama kuwa ndiyo dili pekee ya wamarekani kwa kutumia kauli hii,.........IT IS TIME TO PASS THE BUTTON OF POWER TO THE YOUNGER GENERATION.....IT IS TIME TO PASS THE TORCH!
Matatizo yaliyopo hapa nchini yanaathiri zaidi mustakabali wa vijana nao uchaguzi ujao hawawezi kuwaamini wazee ambao wakishinda hujaza wazee wenzao kwenye teuzi zao na kama ni vijana ni kuimarisha familia za wanasiasa tu.
Vijana wengi wanaona mfumo mzima wa kodi ni kandamizi na kuwanyima fursa sawa kwenye soko la ajira likiwemo kujiajiri. Magufuli hana jipya zaidi ya kututapikia yale aliyokariri miaka takribani 20+ kwenye baraza la mawaziri na siyo mbunifu zaidi ya kujidanganya maprofesa na madokta ndiyo ufumbuzi wa kero zote kumbe ni sehemu ya tatizo kwani wanapewa majukumu ambayo hawana uzoefu nayo.