Ni tukio la namna gani linastahili bendera kupepea nusu mlingoti?

MZALENDOWAKWELIKWELI

JF-Expert Member
Feb 5, 2012
330
210
Wadau,

Kuhusu msiba wa wa wanafunzi 32 wa shule ya Lucky Vicent Arusha.Taifa zima limetetema.Taifa zima linaomboleza.

Ni msiba mkubwa kitaifa kuwahi kutokea kwa miongo kadhaa kwa tukio kubwa namna hii je, haipaswi bendera kupepea nusu mlingoti? Ukizingatia kifo cha kijana wa Taifa la kesho ni zaidi ya kifo cha watu wazima 10+.

Kama haifai, je ni tukio la namna gani lina 'qualify' bendera kupepea nusu mlingoti?
 
Unataka kumlazimisha rais aamrishe nusu mlingoti kama mlivyomlazimisha atangaze njaa?
Kwani umemjua yeye ni nani hata useme "mlivyomulizamisha?" Mbona kaongea vzr tu kwa kuuliza swali zuri pia au kama kawaida umeshampa chama?!!....
 
eeh Mungu watie nguvu wazazi waliopotelewa na watoto, unakuta mwingine mtoto ni huyo huyo tu halafu naye ndio hivyo....
ila angekuwa mkwele angesafiri hadi Arusha akawape pole, sijui huyu .
 
Kama serikali yetu imeshindwa kushusha Bendera Nusu mlingoti kwa kuondokewa na

Watoto na wadogo zetu Hawa Basi sisi katika simu zetu kuanzia facbook whats app Jf

Tuweke mishumaa Yenye kuashiria Majozi katika sakata hili

Msiba huu umemsababishia hadi mama alie kuwa mzima nae kupata presha na kufariki hakika sio jambo la kuchukulia kawaida

Hili nipigo lataifa
a14b4226ea8ff7c6396f9c8bf32f5182.jpg
 
umri mdogo,ndoto kubwa zmezmika...hapa ndo napoamini ndoto zipo makaburini watu wanakufa nazo...Wapumzke kwa Amani.
 
Kifo cha kijana wa taifa LA kesho ni zaidi ya vifo vya watu 10
FUTA KAULI YAKO
tunaomboleza Sawa ila be realistic
Kilicho kushtua n nn sasa. ? Wakati hawa wa Leo ndio wanaonekana vilaza na Mangu kawapiga chini. . Lakini wangekuja kuwa na vyeti halali
 
eeh Mungu watie nguvu wazazi waliopotelewa na watoto, unakuta mwingine mtoto ni huyo huyo tu halafu naye ndio hivyo....
ila angekuwa mkwele angesafiri hadi Arusha akawape pole, sijui huyu .
Kwa jinsi Kikwete alivyokuwa na ukaribu na jamii, na kushiriki matukio mengi ya kijamii, angekwenda kwenye huu msiba.
Nadhani na viongozi wetu wa sasa pia watashiriki, iwapo itawekwa misa/sala/ibada/dua ya pamoja kwa marehemu hawa, mmoja kati ya top three atahudhuria.
 
Back
Top Bottom