OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 52,035
- 114,474
Mahakama ni moja kati ya muhimili wa nchi yetu. Unatakiwa kuwa huru na usitomaswe tomaswe katika namna yeyote na mda wote.
Vilevile moja kati ya tuezi ambazo rais anaweza kuteua tu na hawezi kwa mujibu wa katiba kutengua ni Jaji Mkuu na Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. Hata kama utamuundia fitna vipi utaishia kumtazama tu.......
Baada ya Jaji Mkuu wa Tanzania Athumani Chande kumstaafu. Rais Magufuli alifanya uteuzi wa Prof.Ibrahim Juma kuwa Jaji Mkuu lakini akiwa Kaimu Jaji Mkuu yaani Acting Chief Justice. Kwa tafsiri ya kimtaa-mtaa Jaji huyu kwenye Ujaji Mkuu kaandikiwa kwa penseli na kwamba anaweza kufutwa mda wowote na akaandikwa mtu mwingine....nadhani mnanielewa....
Nimefanya utafiti nchi mbalimbali sijapata kuona Jaji Mkuu anakaimishwa. Hii ni kutokana na unyeti wa nafasi yake na kumuongezea mamlaka na nguvu. Lakini hapa kwetu ni kinyume.
Je,
1.Mamlaka ya uteuzi haioni kama kukaimisha nafasi kubwa kama hii kunamuondolea Jaji power ya kufanya maamuzi.
2.Kwa nini mamlaka haikuona haja ya kumteua bwana huyu kuwa Chief kamili
3.Nini madhara ya uteuzi kama huu kisheria?Hatuoni kama muhimili huu umewekwa rehani?
Naomba majibu na sio kashfa