Ni Tanzania ipi tunaitaka?

Pantosha

JF-Expert Member
Sep 22, 2022
349
464
Serikali nyingi duniani zinapambana kuwaletea wananchi wake maendeleo. Viongozi wa serikali ya Tanzania nayo hawapo nyuma katika kuhakikisha watanzania wanakuwa na maisha bora. Jitihada hizo zinaonekana.

Swali ambalo huwa najiuliza ni Tanzania ya aina gani watanzania wanataka? Katika utafiti wangu kwa watu wa rika/umri, elimu, ajira, na vipato tofauti haya na majumuhisho ya Tanzania iliyo katika ndoto za wengi.

1) Huduma za bora za matibabu, elimu, maji, umeme, nk. Wananchi wanatamani kuona serikali inafanikiwa kutoa hizo huduma kwa viwango bora kabisa.
N.B: Wananchi wengi wanaona ni vizuri kiingereza kiwe lugha ya kufundishia.

2) Miundombinu mizuri ya barabara, miji iliyopangiliwa, usimamizi wa ujenzi wa nyumba, viwanja vya michezo na sehemu za kustarehe.

3) Ajira na mishahara mizuri

4) Kupunguza kodi na tozo

5) Mikopo yenye masharti rafiki na isiyo na riba kubwa. Michango ya mifuko ya jamii kutumika kama dhamana ili mwanachama akopeshwe.

6) Sheria irihusu mwanachama wa mfuko wa jamii kupewa michango yake kwa mkupuo pale atakapokuwa ameacha au kuachishwa kazi.

7) Kutilia mkazo swala la maadili, uzalendo, nk.

Nakiribisha discussion, comments kwenye andiko hili.
 
Uote ayo yanawezekana mkuu sema uzalendo ndo akuna ingeundwa sheria kama ya china uki urunda unalambwa.

Wa tz n waoga wasingetaman kulambwa vichwa ko wangenyooka.

Sent from my TECNO KI7 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom