Ni Taifa gani analolitetea sheikh Farid? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni Taifa gani analolitetea sheikh Farid?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by gollocko, Jun 1, 2012.

 1. gollocko

  gollocko JF-Expert Member

  #1
  Jun 1, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 2,827
  Likes Received: 1,542
  Trophy Points: 280
  ""Ni kweli siku tatu za vurugu mimi sikulala nyumbani, ila sitaji nilipokuwa nikilala…nachukua tahadhari, unajua sisi hatuna jeshi wala silaha, ila linaloandikwa likufike litakufika tu. Heri mimi nife nikiwa jasiri kuliko kuacha taifa langu likiangamia.”

  Haya ni maneno aliyozungumza Sheikh Farid mara baada ya kuachiwa kwa dhamana hapo juzi.Lakini tukirudi nyuma tutakumbuka kuwa hawa wakina Sheikh Farid walitumiwa sana na Maalim Seif Sharif Hamad katika kukikampenia chama cha CUF na mara zote baada ya chaguzi za Zanzbar kwisha na CUF kushindwa walikuwa mstari wa mbele kupinga matokeo huku wakiandaa maandamano ya kuwalaani waunguja(CCM) kwa kuwapoka ushindi wapemba(CUF).

  Hii ilifikia mpaka wakina Sheikh Farid kuwahamasisha wapemba kuwatenga waunguja huku wakipakaza vinyesi kwenye nyumba zao na hata kuviweka kwenye visima vya maji wayatumiayo waunguja(rejea matukio ya vurugu baada ya uchaguzi mkuu wa 2005).
  Baada ya kupata serikali ya umoja wa kitaifa na wapemba kuongoza serikali hiyo sasa wakina Sheikh Farid wamekuja na hoja nyingine ya kuupinga muungano.
  Hapa nashindwa kuwaelewa wakina Sheikh Farid wanatetea Taifa gani? La wapemba, la waunguja au la Zanzibar?
   
 2. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #2
  Jun 1, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,202
  Likes Received: 1,007
  Trophy Points: 280
  Katiba ya Zanzibabar imetungwa hivi karibuni na ilikiuka katiba ya Tanzania kwa kutamka wazi kuwa Zanzibabar ni nchi na ikiainisha mipaka yake. Kwa kuwa viongozi tulio nao sasa ni watu wasiotaka kujihusisha katika maamuzi magumu walijifanya kama kwamba hawaoni katiba mama ikivunjwa. Matokeo ya kuvunjwa kwa katiba ndiko sasa kunakotoa ujasiri wa watu kuinuka na kudai mambo mbali mbali kama nchi inayojitegemea. Katiba ya Muungano haina tena uhalali wa kuyahoji makundi yaliyopo ndani ya nchi ya Zanzibabar kwa kuwa imeishakatwa makali na katiba mpya za Zanzibabar. Kwa kifupi machafuko ya Zanzibabar ni matokeo ya watawala tulio nao sasa kukwepa wajibu wao wa kiutawala.
  .
   
 3. kwamwewe

  kwamwewe JF-Expert Member

  #3
  Jun 1, 2012
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,314
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Luka 19:27 Na sasa, kuhusu hao maadui wangu ambao hawapendi niwe mfalme wao, waleteni hapa, mkawaue papa hapa mbele yangu."`

  19:28 Yesu alisema hayo, kisha akatangulia mbele yao kuelekea Yerusalemu.
   
 4. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #4
  Jun 1, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Wanatetea taifa la 'Kihuni'.
   
Loading...