Ndugu wanaJF,
Kuna baadhi ya vitu huwa vinatumiwa tu na wanawake, lakini pia vipo vinavyotumiwa na wanaume tu, japo vipo ambavyo twaweza kutumia pamoja. Sitaki kuzungumzia perfume maana nahc kutakuwa na ubishi sana. Unakuta perfume imeandikwa 'for women' lakini mwanaume kajipulizia nyingi, vitu kama simu kutegemeana na rangi twaweza kutumia wote.
Hoja yangu ni matumizi ya LIPBUM kwa wanaume. Mimi huwa nikienda salon nikipakwa najihc kama njiani nasemwa kwasababu sijui. Naomba tusaidiene hapa hasa wale wanaotupaka au wanaotengeneza au wauzaji.
Na huu upepo....acha kujipaka uone lips zinavokuwa kama kisigino
mi sioni shida ila zisiwe za rangi kama wanazopaka kina ommy dimpoz na wabana pua wenzie
Nililazimika kuzitrumia kwa mara ya kwanza Iringa ilikuwa ni mwezi wa sita, kuna baridi na upepo mkali sana. Nilipasuka lips mpaka zikawa zinatoa damu pamoja na kujilamba sana lakini haikusaidia, nikaletewa hayo mafuta ya mdomomoni na yalinisaidia sana kupona.
Kikubwa inategemea mtu anazitumia katika mazingira yepi, anajipodoa tu au anatumia kwa sababu za msingi??
Ha haaa eti lips kama kisigino,sio kama goti la mbuzi?
ha ha ha shahidi wewe???best mume wangu ulikuwa nae wapi hadi uwe shahid na ujue anatumia nini???
Hujui habari ya michepuko ww ni mgeni Yerusalemu hii
kwa nchi za baridi hata wanaume wanatumia hio kwa sababu midomo inakauka hadi inapasuka,usipotumia hio utapasuka midomo hadi inatoa damu. ila kwa hapa dar tuwaachie dada/mama zetu.
sweetie mimi natumia vaseline petroleum jelly
mie jana tu nimeona mtangazaji wa television moja hapa tz kapaka lipstic ya pink imemkolea kweli kweli sa sijui ndo fashion
Ya kipind cha barid na upepo ni mazuri hayangai kwenye lipi na wala hayana harufu....
Afu baby Nina kesi njoo home haraka miss neddy anasema anajua lip unazotumia wewe na shahid ni yeye...
hata Mokoyo anapaka shahidi mimi lol
Na kweli tangia excel aondoke napata wasi wasi