Ni sawa kuisifia serikali ikiwa bado tuko hivi!?

Ni sawa kuisifia serikali ikiwa bado tuko hivi!?

Uncle Jei Jei

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2011
Posts
1,683
Reaction score
2,158
Sasa hivi kila kona hutakosa watu wanaopongeza Juhudi kubwa za serikali ya sasa! Nasema kila kona hutakosa wawili watatu na kwa bahati mbaya au nzuri hawa ndio sauti zao husikika zaidi!

Leo nimekutana na watu wengi wanasema Tundu Lisu kuliko aendelee"kuzurula" huko ulaya na marekani ni bora arudi nyumbani aone kazi nzuri inayofanywa na serikali!

Nimetafakari, nikaangaza hapa napoishi nione hiyo kazi nzuri, nimewaza nikawazua nikakumbuka huenda wanaosema kazi nzuri wanamaanisha haya yafuatayo:-

1. Ununuzi wa ndege, maana hili hawakosi kulitaja

2. Kuwabana watumishi wa umma hasa wa ngazi za chini, maana hadi leo hawana nyongeza wala maboresho yoyote kama awamu zilizopita

3. Kusafisha vyeti feki na wasio na vyeti kwa ahadi ya kutenda haki kwa wafanyakazi halali na kuajiri wenye sifa, ahadi hii bado ni ahadi hadi leo

Huenda hayo ndio kazi nzuri wanayosifia!

Nikajiuliza tena na nikatazama yafuatayo:-

1. Shule zetu za kata zilizobeba watoto wote wa masikini zinamazingira yanayofaa kujifunzia!? Hapa nikagundua,
a. Hazina madawati ya kutosha
b. Hazina maabara, library wala madarasa ya kutosha
c. Darasa moja wanafunzi wako hadi 100 kwa baadhi ya shule

Halafu nikakumbuka St. Fransis ile shule ya Mbeya, watoto wote 91 wamepata division one na Kati ya hao wasichana tisa wako ndani ya kumi bora kitaifa! Wakati kwenye matokeo ya kidato cha pili, watoto wote walipata division one point saba, walifeli wawili tu ambao kati ya masomo kumi waliyofanya wao walichanganya na B mbili!! Yaani wengine wote walipiga A flat, hawa wawili wakawa na A nane na B mbili!

Nikajiuliza, hivi hawa maskini wenzangu wanajua umuhimu wa kusomae mazingira rafiki!? Angalau ile kusoma tu umekaa kwenye meza na kiti mkiwa angalau 50 hadi 60 inatosha! Hadi hili nalo bado wanasifia!

2. Nikageukia hospital zetu, nikakuta zilizonyingi bado huduma ni duni! Ukiwa na mgonjwa seriously na hauna hela lazima unyanyasike! Hili nalo wanapongeza

3. Nikawaangalia wadogo zangu waliograduate tangu 2015, nikaona bado wako mtaani hawana hili wala lile, wakipaza sauti wanaambiwa wajiajiri na wanaowaambia hivyo wao wenyewe hawajaweza kujiajiri na kila siku wanaomba wasitimuliwe kazi maana wanategemewa! Hili nalo wanapongeza!

4. Nikapata wazo nikasema huenda wanaopongeza labda ni wakulima, nikaambiwa nao wanalalamika hawana masoko ya mazao yao! Mchele na mahindi waliyovuna mwaka jana bado bei iko chini maana walizuiliwa wasiuze nje ya nchi

5. Kingine nikaangalia Tanzania ya viwanda tuliyoahidiwa, bado nikaona ni ahadi tu na hadi sasa promo imeshuka sana! Tuliambiwa viwanda tu na hatukuambiwa vitakuwa viwanda vya level gani! Hili nalo tunapongeza tu hatuna namna japo hatuvioni!

Naomba nimalize kwa kuwauliza, katika ujenzi wa Taifa imara tunatakiwa tuanze kuwajenga watu au kujenga vitu!?

Kipi kipaumbele kati ya ustawi wa jamii na ustawi wa vitu!?

Watoto wetu wanaosomea mazingira magumu halafu mwisho wanapewa mtihani sawa na waliosomea mazingira mazuri, wataweza kushindana nao katika kuendesha na kusimamia hivyo vitu!?

Jumapili njema!
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtaji wa CCM ni ujinga wa watu. Ili watu waendelee kuwa wajinga na waendelee kusifu hawapaswi kuwa na elimu bora ila bora elimu.

Hao wachache wa St. Francis hawana madhara sana ni kama kijiko cha chumvi baharini tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hoja nzito kweli kweli sijui Lumumba watapitia wapi.Hongera mtoa mada huo ni ukweli mtupu.Anyway pakupitia Lumumba ni kujitoa ufahamu.
 
Back
Top Bottom