Ni sawa kubadili maDC na maDAS kwa kipindi kimoja?

sirluta

JF-Expert Member
Nov 28, 2012
6,325
2,488
Ni hoja tu inahitaji kuidadavua, wapo maDC waliotemwa kabisa na wengine wamehamishwa, vivyo hivyo kwa maDAS.

Swali ni kwamba: HOW ABOUT PENDING MATTERS?

Sura mpya zimekutana, ofisini watawezaje kushughulikia matatizo ya wananchi ambayo yalishakwishaanzishwa na hayajaisha? Haya ya migogoro.
 
Inawezekana kwani migogoro inatatuliwa kisheria sio kwa muono wa mtu.
Kwa hiyo hao waliopata hizo nafasi wanaweza
 
kuna yale mambo unakuta dc anatumia busara zaidi kuyamaliza kuliko kufuata sheria. Sasa unakuta hayajaisha, na akija mwingine inabidi yaanze upya! Bora hata das akiwepo anambrief dc mpya yanamaliziwa.
 
Kwani hakuna makabidhiano??
 
Ni hoja tu inahitaji kuidadavua, wapo maDC waliotemwa kabisa na wengine wamehamishwa, vivyo hivyo kwa maDAS.

Swali ni kwamba: HOW ABOUT PENDING MATTERS?

Sura mpya zimekutana, ofisini watawezaje kushughulikia matatizo ya wananchi ambayo yalishakwishaanzishwa na hayajaisha? Haya ya migogoro.
NI KOSA KUBWA SANA
 
Kwani hakuna makabidhiano??
mengine yanakuwa hayapo hata kwenye maandishi, lakini pia suala la makabidhiano, lina namna yake. Mtu amekosa kibarua unadhani atakabidhi kila kitu kikiwa sawa?
 
MaDC ni mapambo tu kwenye councils; mtendaji ni DED so hata wakibadilishwa kila leo watafanyiwa briefing na maisha yataendelea.
 
Serikali ya awamu ya tano haitaki kufanya kazi kwa mazoea hivyo wameangalia DCs na DAs utendaji wao na qualifications za kila mmoja ,kwa hiyo wapo sahihi hapa kas tu.
 
Back
Top Bottom