Ni sahihi zaidi kuoa kabila lako?

Ni sahihi zaidi kuoa kabila lako?

Ryzen

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2012
Posts
7,312
Reaction score
8,754
Kuna rafiki yangu mmoja (yeye ameoa) alinipa story kuhusu ukoo wao, anasema mfanyakazi wa babu yake (babu wa mbali kama babu yake babu yake mshikaji wangu) aliwahi kumpiga mume wa dada yake huyo babu, huyo mume alitoka damu na mila na desturi ya kabila ao hio ni laana na isitoshe huyo umme wa dada yake alilaani nyumba ya babu yake huyo rafiki yangu na kwakuwa alimlaani babu basi hio laana inatafuna watoto wa kiume pekee.

Anasema basi katika ukoo wao huo watoto wa kiume wanafariki vifo vya ajabu mno. Anazidi kuhadisia kwamba kwao walizaliwa watoto wa kiume sita, wengine wa 5 wamefariki na vifo vyote ni dizaini ya ajabu tu.

Anazidi kusema kwamba aliona na yeye msafara ni ule ule kwa bahati nzuri wazee wa kimila wenye busara zao wakamshauri kwenda kuitengua ile laana na kuitengua mpaka waitafute ile sehemu tukio lile la yule mume kupigwa ndio watengulie hio laana apo.

TUENDELEE
Nikiwa kijana mdogo nilikuwa na ndoto ya kuoa Mzungu, ila umri ulivyozidi kusogea nikaona hapana aisee kale kamuda ka usiku ka kupumzika ambako unatakiwa upige story na waifu labda kuhusu mambo yanayoendelea mtaani kwenu kweli story zitanoga? Labda mke ni Mjerumani halafu wewe Mbongo kweli kutakuwa na mnogesho wa story hapo si kutakuwa na less story? (Story za hapa na pale na kusisimua ni kiungo muhimu sana cha mapenzi!.) Nikaona hapana lazima nioe mbongo mwenzangu.

Katika harakati na mawazo yote hayo sikutaka kabisa kuwa na idea ya kuoa kabila langu na sikutaka kabisa maana ni kama nimewazoea vile, kweli nilitaka kupeleka kabila geni pale nyumbani nioneshe utofauti nyumbani.

Ila sasa nikafikiria saana ivi nikioa kabila lingine si watoto wangu hawatakuwa vizuri kiutamaduni? Watoto hawatajua vizuri lugha mama ya mimi baba yao au ya mama yao, kwa maana tukiwa nyumbani lugha kubwa ya kutumika itakuwa kiswahili tu wakati mume na mke mngekuwa kabila moja mngetumia lugha mama zaidi.

Sikuishia hapo nikawaza mimi kama mwanaume ninayeamini na kuzikubali mila na desturi ya kabila langu nikioa kabila geni si wanangu watakuja kuwa partial sana katika swala zima la mila na desturi! Jambo ambalo litapoteza identity ya kabila langu kwa wanangu.

Kwa maana hiyo kumbe wanangu waki deviate kidogo kwenye utamaduni kuna matatizo ambayo yatahitaji utamaduni ili kukaa sawa basi wao hawatalielewa hilo na hili linani motivate sana kuoa mwanamke wa kabila langu anayejua mila na desturi vizuri.

Tumeona kwa kiasi fulani ndoa za mababu zetu, wazazi wetu zikiwa zimedumu. Hizi ndoa zimedumu pia hasa kwa wale ambao ni watu wa kabila moja. Pale kulipokuwa na matatizo kwa kuwa ni watu wanaoshea lugha moja, mila moja na utamaduni mmoja inakuwa rahisi kusululuhisha matatizo yanayowakabili.

Najua na naelewa ndoa ni mapenzi ya Mungu na mapenzi hayachagui kabila na wala hapa sipo kupiga debe ukabila lakini ni vema sisi wanaume ambao ndio waendelezaji wa makabila yetu na koo zetu katika nyanja zote za utamaduni, mila na desturi pia tukazingatia hili.

Ni kama jinsi wayahudi walivyo hawataki kuchanganya damu zao na koo zingine. Kwa maana hiyo nafikiri ni vema zaidi kuoa nyumbani/kabila lako binafsi naahidi nitaoa nyumbani.

Mwisho: Ikumbukwe maneno yangu sio sheria!
 
Karne hii watu mnawaza ukabila?
 
Lazima utakua mtu wa kule kwetu Tarime...
 
Back
Top Bottom