Ni sahihi, polisi mshika Tochi kuvaa kiraia na kujificha kichakani?

sifi leo

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
5,098
8,727
Wanajamvi hasa polisi kama mpo hapa, na waziri uliyepigwa chini nisadieni, kwa mara ya kwanza nimekutana na Askari wengi sana ukitoka Arusha mpaka Bagamoyo kuna Askari kibao wanawakamata watu kwa kupima speed, huku wakiwa wamevaa kiraia, na wanapokuwa wanakupiga Tochi wanakuwa wamejificha kichakani.

Pili baada ya kukupiga tochi, anakuacha unampita ndio anampigia trafiki aliyevaa sare ya kazi, na kumwambia umepita kwa speed kiasi gani na kumwambia akukamate. Je, watu hawa wapo sahihi?
 
Kama umekutana nae huyo hawez kukukamata isipokuwa ana monitor ur driving discipline at speed limited regions so utakutana nao wengine sehemu nyingine wakikusomea makosa yako,

Ushaur zingatia alama za barabaran,hilo halina.kosa na linalofanyika.hapo ni kukufanya.uwe na.self control.uzoeee kutii alama.za road,sio.paka uone kofia nyeuoe
 
kwa nini anajificha kichakani(akingatwa na nyoka), kwa nini havai uniform? kupima speed nakubarian na wewe mkuu, kwa nini wanajificha? sheria inamtaka askari gani hasivae uniform na kwa kazi zipi ndani ya jeshi la police?
ni msaada tu naomba, pili naomba unijuze speed limit ya gari ndogo kma CARNA IST, na nyingine pahala ambapo hakuna alama yyte, kwa maana ya kibao cha 30km au 50km?...
 
Kujificha porini ni kama ziara ya kushtukiza, kukufanya usiendeshe gari kwa mazoea bali sheria za barabarani,madereva wamekua wakipeana ishara sehemu zenye matrafic, kama hawapo wanatembea kwa speed kubwa hata kama ni eneo la kijiji au mji kitu ambacho ni hatari kwa raia, Speed limit kwa barabara zote za Tanzania kama hamna kibao ni 80KPH ukizidi hiyo unaweza tozwa faini vilevile. Ukiendesha barabara ya Mafinga Mbeya utakutana sana na torch maeneo yasiyo na vibao kutokana na ubovu wa barabara maeneo hayo.
 
nim

nimekusoma mkuu, ila ziara za kushutukiza imekuwa kama fasheni sasa, au ndo hapa kazi tu, ila wanapokea mlungula kama kawaida, nadhani kuna haja ya wakubwa zao kupita maeneo yale.
 
Hhahahahhahahaah tatizo sio wao kupokea mlungula tatizo ni sisi kutoa mlungula, ukikubali kosa na kulipa faini hawawezi kukuomba mlungula. Mfano wewe unaona kipi bora ulipe faini 30,000 au umpoze na buku 5 uendelee na safari?
 
wanajamvi hasa polisi kama mpo hapa, na waziri uliyepigwa chini nisadien, kwa mara ya kwanza nimekutana na Askari wengi sana ukitoka Arusha mpaka Bagamoyo kuna Askari kibao wanawakamata watu kwa kupima speed, uku wakiwa wamevaa kiraia, NA wanapokuw wanakupiga Toch wanakuwa wamejificha kichakani.

pili baada ya kukupiga toch, anakuacha unampta ndo anampigia trafiki aliyevaa sare ya kazi, na kumwambia umepita kwa speed kiasi gani na kumwambia akukamate je watu hawa wapo sahihi?
Ni sahihi.
 
Mie mwenye huwa nashangaa,unaona eti Wanajeshi wanaenda vitani eti wanajificha,sasa kwanini ajifiche kichakani badala ya kupambana huku mnaonana,sijui kwanini hawa jamaa wanakera sana aisee.
We kama unaenda vitani nenda muonane uso kwa uso,atakaemuwahi mwenzie kwa risasi au bom amuue,ila wao unakuta eti kajificha vichakani,na amevaa majani ili asionekane,ahhh
 
kwa nini anajificha kichakani(akingatwa na nyoka), kwa nini havai uniform? kupima speed nakubarian na wewe mkuu, kwa nini wanajificha? sheria inamtaka askari gani hasivae uniform na kwa kazi zipi ndani ya jeshi la police?
ni msaada tu naomba, pili naomba unijuze speed limit ya gari ndogo kma CARNA IST, na nyingine pahala ambapo hakuna alama yyte, kwa maana ya kibao cha 30km au 50km?...
Nakubariana=Nakubaliana
Hasivae=Asivae
 
Mie mwenye huwa nashangaa,unaona eti Wanajeshi wanaenda vitani eti wanajificha,sasa kwanini ajifiche kichakani badala ya kupambana huku mnaonana,sijui kwanini hawa jamaa wanakera sana aisee.
We kama unaenda vitani nenda muonane uso kwa uso,atakaemuwahi mwenzie kwa risasi au bom amuue,ila wao unakuta eti kajificha vichakani,na amevaa majani ili asionekane,ahhh
Hahahhahaha kweli sukari imeleta shida
 
Hiyo ni mbinu muhimu sana hata mimi naikubali kwa wakati bado hatuja weka kamera za barabarani. Nchi zingine kaka ukizidisha mwendo kasi sehemu yenye limit kama inachukua picha baada ya masaa ndani ya masaa matatu unatumiwa bili ya fani kwa njia EMS, unalipia mpaka gharama za EMS.
Hata kama gari ulimpa mtu mwenye gari ndiye anabeba dhamana ya kulipa fine.
 
nadhani wako sahihi. kama wakitumia mbinu za kawaida madereva wanajulishana na kuwakwepa huku wanavunja sheria, ni sawa kuhamia kwenye mbinu za kiintelijensia zaidi na kwa hili wameonyesha kuwa wao ni askari mahiri.
 
Hiyo ni mbinu muhimu sana hata mimi naikubali kwa wakati bado hatuja weka kamera za barabarani. Nchi zingine kaka ukizidisha mwendo kasi sehemu yenye limit kama inachukua picha baada ya masaa ndani ya masaa matatu unatumiwa bili ya fani kwa njia EMS, unalipia mpaka gharama za EMS.
Hata kama gari ulimpa mtu mwenye gari ndiye anabeba dhamana ya kulipa fine.
hapa kwetu wewe kama dereva utajuaje speed aliyotuma huyo aliejificha ni yako au kakubambikia? anatuma na picha pia?
 
Kwani kwenye nchi wanazo tumia camera we unadhani unaletewa picha. Ni faini imeandikwa unaruhusiwa kubisha ukishindwa unalipa zaidi na penalty ya kuchelewa kulipwa.
Hata kwa polisi ukibisha wala hawaakulazimishi utaandikiwa kosa utakutana nao mahakamani.
 
Back
Top Bottom