Ni sahihi kwa mtu anayetaka kupungua uzito kunywa maziwa fresh mara kwa mara!?

Uncle Jei Jei

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,684
2,157
Wasalaam wakuu, tafadhali naomba kufahamu kutoka kwa wataalam kama kweli ni sahihi au si sahihi kwa mtu mwenye uzito ulizidi na mwenye uhitaji wa kupungua uzito kama itakuwa sahihi kwake kutumia maziwa ya ng'ombe mara kwa mara. Asanteni.
 
Watu mnataka kupunguza uzito lkn hamtaki kuacha vyakula vyenye calories nyingi !!... Kwanini aanze kuwaza maziwa na sio maji?..nijuavyo maji ni muhimu ktk kusaidia digestion kuliko maziwa!!..yaani maji na matunda yote haya bado mtu unataka kujishindilia maziwa kila siku na tayari upo obesity!!
 
KWANZA unatakiwa ujue wewe kama wewe nini kilichokuletea unene

-mazoezi
-kula vibaya
-kuridhika
-homoni kukaa vibaya hasa insulini

PILI uanze kupambana na nini cha kufanya

TATU fahamu ya kuwa maziwa yana kiasi gani cha wanga, mafuta na protein na kisha jiulize kiasi hicho kinaweza kukuletea au kukuongezea kilo ngapi kwa siku.

Karibu tena kama una la kufunguka zaidi
 
Mkuu ni kweli tunatakiwa kuwa na uelewa japo kidogo wa vitu tunavyokula na sehemu zenyewe za kupata huo uelewa ni pamoja na humu tunapo badilishana uelewa, lakini kwa style yako sijui kama kuna msaada hapo. Nadhani maelekezo yako yalitakiwa yaelezee kama yanafaa ni kwanini!? Na kama hayafai ni kwanini!? Fullstop! Hoja ya kuanza kujiuliza sijui uanaongeza kilo ngapi, yana kiasi gani sijui cha nini na nini, majibu hayo hayaji kwa kujiuliza tu!! Bali hutoka kwenye vyanzo vya maarifa ambapo kama unafaham unasema kama hujui unacoool tu!
 
kila mwanajf anunue kamba afanye zoezi la kuruka kamba,unaweza kuanza kuruka mara kumi halafu kilasiku unaongeza kidogo mpaka utakapo wezavizuri hiyo ni dawa kubwa ya kupunguza uzito
 
Mind you, uzito haupungui kwa mazoezi, mazoezi hayapunguzi uzito..

Cha kwanza ili upunguze uzito ni misosi, punguza misosi ya mafuta sana na wanga nyingi.

Mazoezi hukusaidia kumantain uzito wako utakaokua unaupunguza kutoka kwenye chakula.

Kama huwezi kudhibiti ulaji wako hata ufanye mazoezi unalia hakuna kitakachobadilika,hata ukimbie dar mwanza utabaki vile vile.

Mazoezi yanakufanya uwe na njaa zaidi na ule zaidi, kama hauko tayari kupunguza chakula huwezi kupungua.

Ukifanya mazeozi unaunguza kalolizi nyingi, hivyo ukila kidogo maana yake unaingiza kalolizi kidogo mwilini na ukifanya mazoezi unaunguza kalolizi nyingi hapo utapungua maana kinachotoka kinakua kikubwa kuliko kinachoingia.

Mazoezi kama mazoezi hayapunguzi uzito..
 
Rahabu pole kama unashida ya ukweli nichek kwa namba 0655 580 788
QUOTE="a.rahabu, post: 16297328, member: 202367"]Hayo maziwa nakunywa sana ndo nazidi kuongezeka[/QUOTE]
 
This is noted lakini sioni ikimsaidia muuliza swali, mara nyingi sana watu wa mitandaoni mnakuwa wapita njia, i want a real person ambaye kweli ana shida, na tukaongea naye kifasaha.

Sayansi ya chakula ni sayansi kamili, inayohitaji umakini kabisa.

Back
Top Bottom