Ni sahihi kwa Msimamizi wa Uchaguzi kuteuliwa Uwaziri?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
127,831
244,324
Ninawaomba wajuzi wa mambo ya protokali na utawala bora wanisaidie mimi na wengine wenye mapungufu yanayoshabihiana na yangu.

Mh. Balozi Ali Karume aliyekuwa msimamizi wa ndani wa uchaguzi wa marudio wa Zanzibar ameteuliwa ubunge na hatimaye ameukwaa uwaziri wa miundombinu.

Je, kwa msimamizi wa uchaguzi kuteuliwa hakuwezi kuwafanya wadau watilie shaka ripoti yake ya uchaguzi? Na je kitendo hikl ni halali? Na je, kulikuwa na haja gani kuteua msimamizi wakati kuna wazanzibar kibao wenye uwezo?
 
Unajua unatakiwa utofautishe baina ya msimamizi na muangalizi...

Msimamizi anakuwa muajiriwa wa tume na waangalizi mara nyingi sana wanatoka NGO,jumuiya za kimataifa na taasisi nyengine zisizo na serikali.

Sasa, Ali Karume alikuwa kama Muangalizi wa Ndani kwa hivyo alikuwa hana uhusiano wowote na tume ya uchaguzi ZNZ na alikuwa siyo muajiriwa wa tume ya uchaguzi wa kudumu au wa muda mfupi.
 
Kajifunze tofauti ya Muangalizi wa Uchaguzi na Msimamizi wa Uchaguzi! Una tatizo la kilugha sio kisheria.Ally Karume ni Mlinzi wa Mapinduzi matukufu ya 1964!
 
Tu unganishe na ya kesho atakayoongea Maalim Seif tunaweza pata jibu.......lakini haitasaidia kitu.Mchezo finished sasa tujenge nchi.
 
ule usemi wa nothing is impossible in zanzibar unahusika..Nashangaa zaidi kwanini kikwete hakuwa Makamo wa kwanza wa rais zanzibar kuliko kuwa kwake makamo wa rais.
 
Unajua unatakiwa utofautishe baina ya msimamizi na muangalizi...

Msimamizi anakuwa muajiriwa wa tume na waangalizi mara nyingi sana wanatoka NGO,jumuiya za kimataifa na taasisi nyengine zisizo na serikali.

Sasa, Ali Karume alikuwa kama Muangalizi wa Ndani kwa hivyo alikuwa hana uhusiano wowote na tume ya uchaguzi ZNZ na alikuwa siyo muajiriwa wa tume ya uchaguzi wa kudumu au wa muda mfupi.
asante sana kwa masahihisho mazuri mkuu , lakini vipi uhalali wa Mwangalizi kama huyu kuteuliwa uwaziri ni halali ?
 
Km wamebak
Ninawaomba wajuzi wa mambo ya protokali na utawala bora wanisaidie mimi na wengine wenye mapungufu yanayoshabihiana na yangu.

Mh. Balozi Ali Karume aliyekuwa msimamizi wa ndani wa uchaguzi wa marudio wa Zanzibar ameteuliwa ubunge na hatimaye ameukwaa uwaziri wa miundombinu.

Je, kwa msimamizi wa uchaguzi kuteuliwa hakuwezi kuwafanya wadau watilie shaka ripoti yake ya uchaguzi? Na je kitendo hikl ni halali? Na je, kulikuwa na haja gani kuteua msimamizi wakati kuna wazanzibar kibao wenye uwezo?
Kama wameweza baka katiba hiyo haiwezi kuwa haram
 
Back
Top Bottom