Ni sahihi kuuza viwanja mashamba ili kumsomesha mtoto chuo?

youngkato

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
3,254
2,910
Wakuu kuna ndugu yangu mmoja.

Ana mtoto wa kike amemaliza kidato cha sita, amepata nafasi ya kwenda chuo lakini amekosa mkopo.

Wazazi wake hawana pesa kabisa ila wana viwanja (kijijini kwao) na mashamba ila hayana thamani kubwa sana.

Sasa wao wanaona kama chuo ni kutoboa maisha mwanamke anataka wauze mashamba wamsomeshe mtoto wao.

Mwanamke hataki kuuza anataka asubiri mwaka mwingine aombe tena mkopo.

Je, ni sahihi kuuza mashamba kumsomesha mtoto au wasubiri aombe tena mkopo mwakani.

NB anaenda kusoma kozi ya ualimu ngazi ya degree.
 
Dah inasikitisha sana, kama Mimi ndo huyo mwanafunzi ningewazuia wazazi wasiuze hayo mashamba maana mambo yakibuma baadae wataishia kunilaumu
Mi naona bora dogo angejikita kwenye kilimo kwasababu mashamba yapo apige fedha za kutosha ndo adisaid either akasome au aendelee na kilimo.

Kilimo kwanza pesa iko shambani.
 
kwa mtazamo wangu na hali ya ajira ilivyo sio sahihi kabisa

bora asubiri mwaka unao fuata aombe mkopo, maana hata baada ya kusomeshwa kuna mawili

1. kukosa ajira na wao kujutia mali walizo poteza
2. kupata ajira baada ya masomo na wazazi kutegemea makubwa toka kwake na akishindwa timiza lawama tena
 
Hapo watapoteza vyote mashamba na binti, binti ataliwa kimasihara na vijana wa hovyo na pengine akapewa na ngoma kabisa. Ushauri ni wasubiri mwakani aombe tena.

Inauma sana unasomesha mtoto kwa gharama zako halafu mtoto asipate ajira au badala ya kurudi na cheti anarudi na mjukuu au magonjwa mazito mazito.

Wakuu kuna ndugu yangu mmoja.

Ana mtoto wa kike amemaliza kidato cha sita, amepata nafasi ya kwenda chuo lakini
Amekosa mkopo.

Wazazi wake hawana pesa kabisa ila wana viwanja (kijijini kwao) na mashamba ila hayana thamani kubwa sana.

Sasa wao wanaona kama chuo ni kutoboa maisha mwanamke anataka wauze mashamba wamsomeshe mtoto wao

Mwanamke hataki kuuza anataka asubiri mwaka mwingine aombe tena mkopo

Je ni sahihi kuuza mashamba kumsomesha mtoto au wasubiri aombe tena mkopo mwakani

NB anaenda kusoma kozi ya ualimu ngazi ya degree
 
Uza shamba somesha mtoto wa kike then akimaliza chuo anakuja na kijamaa kiko so broke in the name of love kwamba kinataka kumuoa. So unakuwa umepoteza shamba umepoteza na mtoto.

The choice is urs
 
Wakuu kuna ndugu yangu mmoja.

Ana mtoto wa kike amemaliza kidato cha sita, amepata nafasi ya kwenda chuo lakini
Amekosa mkopo.

Wazazi wake hawana pesa kabisa ila wana viwanja (kijijini kwao) na mashamba ila hayana thamani kubwa sana.

Sasa wao wanaona kama chuo ni kutoboa maisha mwanamke anataka wauze mashamba wamsomeshe mtoto wao

Mwanamke hataki kuuza anataka asubiri mwaka mwingine aombe tena mkopo

Je ni sahihi kuuza mashamba kumsomesha mtoto au wasubiri aombe tena mkopo mwakani

NB anaenda kusoma kozi ya ualimu ngazi ya degree
Batch 2 baado, amekosaje?
 
Ni akili mbovu kuuza kiwanja usomeshe mtoto chuo. Hela zitaisha na elimu haina mwisho huko mbele atasomeshwa na nini wakati asset zote zimeuzwa kama si kupalilia na kukuza umasikini?
 
Elimu hii ya Tz amabyo wahitimu tupo mtaani tunapiga vibarua vya zegee per day 15000?, Chuo kikuu hakuna maana tena it's all about fashion tu, ila kimsingi hao wazazi wanatakiwa waambiwe ukweli wasubiri mtoto aombe mwakani na atapa!!. Gharama za chuo kikuu n kubwa compare na hayo mashamba, mtoto anatakiwa ale, anatakiwa asikosei pesa za mahitaji ya steshenari, mtoto wa kike anatakiwa avae aendane na wenzake....!! Kam familia ndio hiyo ya kutegemea mashamba hope ndani ya mwaka wa kwanza mhura wa pili binti ataomba kustisha masomo.
Akili nzuri ni uza mashamba mtafutie vyuo vya ufundi asomee mwaka 1 au 2 then ajiajiri huku akisubiri kupata mkopo.
 
Hao wazazi walitumiwa barua wamzae huyo mtoto? Kuna mambo mengine sio ya kujadili. Wauze hayo mashamba haraka sana mtoto asome. NI HAKI YAKE WALA SIO HISANI YA WAZAZI. Pia hao wazazi wasisomeshe ili baadae waje kusaidiwa na mtoto. Mtoto sio kitega uchumi.
 
Hii mambo ni ngumu sana labda tofauti na tunavyoweza, kuna familia wanaishi kwenye lundo la umaskini kwenye nyumba mbovu ili kusomesha watato
 
Kuuza mali za hivyo kunaweza kuwa na athari za muda mrefu katika ustawi wa familia .
 
Mi naona bora dogo angejikita kwenye kilimo kwasababu mashamba yapo apige fedha za kutosha ndo adisaid either akasome au aendelee na kilimo.

Kilimo kwanza pesa iko shambani.
Hivi nyie ambao mnasemaga Pesa ipo shambani au vijana kalimeni huwa mnajua gharama za kilimo pamoja na mda utakao chukua au huwa mnatumia maneno tu pasipo kuongea kwa vitendo,,, mtu yupo ofsini anakula kiyoyozi eti kalimeni kilimo kina faida. Hovyo kabisa kwa Miundombinu gani hii ya Tz. Bora muwe mnakaa kmya t
 
Back
Top Bottom