Ngambo Ngali
JF-Expert Member
- Apr 17, 2009
- 3,517
- 1,367
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku cheti maalumu Katibu Mkuu Kiongozi Philemon Luhanjo kwa kutambua mchango wake katika kufanikisha kwa ufanisi mkubwa kufanyika kwa mkutano wa World Economic Forum uliofanyika jijini Dar es Salaam wiki iliyopita.Katika hafla hiyo wadau wengine wakiwamo mashirika mbalimbali,kampuni na watu binafsi nao walitunukiwa vyeti kwa kufanikisha mkutano huo wa kimataifa.source: michuziblogspot
inaelekea chenji za mkutano WEF zilitumika kuandaa hicho chakula cha jioni. Kwa nini hela hizo zisitumike kuziba mashimo ya barabara za dar es salaam ili angalau foleni ipungue? Ni kitu gani cha ziada hawa waandaaji walifanya??? Hawakutoa hela, walifanya kazi kama majukumu yao yanavyowataka at most walilipwa maofisini kwao kwa kutofanya kazi walioajiwa kufanya na badala yake waliconcentrate na maandalizi ya mkutano.