Ni sahihi kusuluhisha ugomvi wa wanandoa?

sabuwanka

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
690
751
Poleni wakuu kwa athari za mvua zinazoendelea nchini kote, poleni wachaga kwa vifo vya wenzetu 20 hapo Jana walipokuwa wakishindana kwenda kukanyaga mafuta ya upako, Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi...na majeruhi wapone haraka, Amina!!!

Tukirudi kwenye mada, miaka ya hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la msigano na migogoro katika ndoa zetu za kidigitali, tumeshuhudia wanandoa wakitukanana....kupigana nk, je ni halali, majirani ,ndugu na marafiki kuingilia migogoro ya ndoa kwa lengo la kusuluhisha?au ni heri wanandoa waachwe wamalize tofauti zao wao wenyewe na Kisha wapatane? Karibuni
 
Upo umuhimu wa kuwasaidia kupata suluhu. Japokuwa sio kila mtu ni msuluhishi. Pia hutegemea ukubwa wa tatizo lilijitokeza. Inapotokea mwanandoa mmoja akiwa na uwezo wa kujishusha ni rahisi sana kupata suluhu. Ugumu wa usuluhishi husababishwa na misimamo ya wanandoa wote kutokubali kusamehe na kujishusha.
 
Back
Top Bottom