vibertz
JF-Expert Member
- Mar 15, 2022
- 1,365
- 2,501
Wawakilishi wa Tanzania katika mashindano ya CAF champions league Simba na Yanga, watakuwa na kibarua kigumu cha kumeenyana na miamba ya soka la Africa. Simba watatangulia kucheza siku ya Ijumaa tarehe 29 saa tatu usiku na Yanga kufuatia kucheza siku ya Jumamosi ya tarehe 30 muda wa saa tatu usiku.
Yanga kucheza usiku mechi ya kimataifa sio jambo ngeni kwasababu ni kawaida kwao kucheza mechi zao usiku, na hata Belouizdad alipigwa usiku ni tofauti na ilivyozoeleka kwa timu ya Simba ambapo jambo lake kwa mwarabu huwa ni jioni. Wydad, Soura, Al Ahly hawa wote walikutana na kipigo cha jioni ila safari hii Al Ahly anakuja kucheza na Simba saa tatu ya usiku
Kila la kheri Tanzania, atakayejipanga vyema ataondoka na matokeo mazuri, muda hauchezi mpira.