Ni perfomance ipi ya msanii iliyokufurahisha zaid kwenye usiku wa tuzo za killi music awards?

Mr.genius

JF-Expert Member
Feb 20, 2012
1,369
1,169
Usiku wa tuzo za muziki kwa wasanii wetu wa hapa nyumbani killi music awards kikwetukwetu ulipambwa na wasanii na makundi mbali mbali ya kuimba na kudance licha ya 'joto' lililokuwapo la nan atachukua tuzo nyingi na hatimae ukweli ukajulikana nani mkali zaid lakini kulikua na jingine la kufurahisha la shoo kali zilizokuwa zikipigwa na wasanii wetu!

Je, kwa upande wako ni shoo ipi ya mwanamuziki alieimba usiku wa tuzo za killi ilikufurahisha sana?

Mimi binafsi nilisuuzika roho sana na shoo ya yule baba aliepiga trumpet kufuatisha wimbo wa my number one wa platnamz na wimbo wa tupogo wa ommy dimpoz (sema jina nimelisahau kidogo)

Kiukweli tunahaki ya kujivunia na kuvisifia vipaji vyetu vya hapa nyumbani hasa vinapofanya vizuri.

Nawasilisha!!
 
Back
Top Bottom