Ni partnership ipi ilikubamba zaidi kwa ngoma zake?

bakundande jr

JF-Expert Member
Oct 22, 2021
507
670
Habari za weekend wadau wa burudani.?.

Katika anga ya muziki hasa wa hapa nchini kwetu ukizungumzia bongo fleva, hip hop na miondoko miongine mbalimbali kumekuwa na wasanii amabo mara nyingi hufanya kazi pamoja japo kuwa sio band. Na wamekuwa wakitoa ngoma tofauti na nyingi. Ni kina nani walikukosha zaidi kwa ngoma zao?

Kwa upande wangu kuna hawa jamaa Ay na mwana Fa. Kipindi hicho wakifanya kazi kwa ukaribu zaidi wametoa ngoma nyingi ambazo zilibamba kama vile dakika moja, habari ndio hia, nangoja ageuke na nyingine nyingi. Yaani kiufupi nikisikia tu Ay Fa huwa najua kitu hicho ni moto wa kuotea mbali.

Vipi mdau wewe ni wasanii gani ambao ukisikia wamefanya kazi pamoja lazima hiyo kazi uipate??
 
Back
Top Bottom