Tofauti ya gari moja na nyingine haiko kwenye speed kama ambavyo unaiona kwenye dash board, bali iko kwenye vitu hivi vikubwa viwili:
Acceleration (Horse Power) na Torque (Uwezo wa kuvuta mzigo/Tela nk).
Gari nyingi za Petrol zina Horse Power nyingi hivyo kuwa na acceleration kubwa lakini pia zina Torque ndogo.
Yani unaweza ukakuta gari Mathalani GX mia ina Horse power (Uwezo wa Farasi 150) Lakini ukiweka ivute tela ya tani moja gari itashindwa kuondoka na huenda ikazimika). Lakini unakuta gari ya diesel mathalani Fuso ina Uwezo huo huo wa Farasi 150 lakini ukiiwekea ivute tela la tani moja italivuta kama mchezo na hata unaweza ukaondokea kwa gia namba tatu.
Ikija kwenye acceleration:
Ukiishindanisha GX mia na Fuso, GX mia itachomoka kama manyoya na itachukua sekunde chache (say 13 seconds) mpaka kufikia mathalani Speed 100 na wakati Fuso hilo hilo linaweza likachukua sekunde ishirini mpaka kufikia speed 100.
Tofauti ya hizo V8 mbili iko hapo...
V8 ya Petrol inachukua sekunde chache zaidi kuchanganya ukilinganisha na hiyo ya Diesel. Yani kama mmeondoka wote mkiwa na Initial velocity (Speed) Uo =0Km/hr na baada ya sekunde 6 ukapima final velociy Uv, utagundua kuwa ile gari ya Petrol ina uwezo mkubwa wa kuunguza mafuta na kubadili nishati ya mafuta kuwa nishati ya mwendo kuliko nishati a Diesel. Mafuta ya Diesel hayaungui haraka kama Petrol na ndio maana gari nyingi za Diesel zinafungwa kifaa kinachoitwa Turbo. Kifaa hichi husaidia kujaza hewa kwenye injini ili kuchochea combustion (moto) katika engine.
Moja ya kitu kinachosababisha diesel iwe na uwezo mkubwa ni kwa vile Diesel inaungua taratibu na inaungua katika joto kali zaidi kuliko Petrol. Kwa hiyo compresiion ratio ya hewa kwenye cylinder ya engine ya Diesel inaweza kuwa 1:10 wakati ile ya Petrol inaweza kuwa 1:7... Yani hii inamaanisha japo diesel inaungua taratibu, ule mgandamizo wa hewa unaweza kuwa mara kumi zaidi ukilinganishwa na hewa iliyoingia kwenye cylinder wakati ile ya Petrol inaweza kuwa na mgandamizo mara saba zaidi... Mngandamizo unapokuwa mkubwa ina maana kuwa lile pigo la cylinder kuizungusha cranck shafti linakuwa ni la nguvu zaidi.
Hapa ni kama vile katoto kadogo kaje kwa nguvu kakuzabe kofi moja alafu Mike Tyson akupige 'kikofi cha mahaba'. Kofi la nguvu la kale katoto kadogo linaweza likakuacha unatabasamu na wakati kofi moja dogo la Tyson linaweza kukufanya upelekwe hosiptali.
Kwa hiyo pigo moja la engine ya petrol ni sawa nakofi la katoto... Kana nguvu nyingi na kanaweza kakakimbia haraka kuja kukuzaba kofi lakini kofi lake halina nguvu sana. Diesel ni kama Tyson, ana nguvu kidogo ya kukimbia kuja kukuzaba kofi lakini akikupiga kofi lake dogo lina kuwa na nguvu nyingi sana.
Hivyo basi utaona mafuta ya Petrol yakitumika kwenye magari madogo na wakati mafuta ya Diesel yakitumiwa kwenye magari makubwa ambayo yanabeba mizigo mizito hata ya tani thelasini, kwenye engine za meli na hata treni...