Magari ya mafuta yaliyowaka moto Kigamboni. Laana ya dhuluma ilihusika?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,754
Hapa nitasimulia kilichotokea katika uhalisia wake!

Kuna mafuta mazito ya kuendeshea mitambo yanaitwa IDO (INDUSTRIAL DIESEL OIL) Haya yanapatikana kwa njia mbali mbali lakini zilizo maarufu ni

1. Kuchuja oil chafu
2. Kuchuja toka kwenye matank yenye mabaki ya mafuta ghafi toka nje ya nchi kama yale ya TIPPER
3. Kuchuja toka kwenye meli za mafuta zinaposafishwa baada ya kumaliza kushusha mzigo
4. Kuchuja toka kwenye matank yanayofanya biashara ya mafuta yanaposafishwa
5. Kuchuja toka kwenye dample la 'slage' (tope la uchafu wa mabaki ya mafuta)
6. Kuchoma tairi
Kati ya hizo zote IDO inayotokana na kuchoma tairi ndio super na ni imflammable moto mara moja kwakuwa ni nyepesi mno

Ughali wa diesel duniani umeipandisha chart IDO .. Sasa hivi hata oil chafu ni dili kubwa sana.. Bei imepaa kutoka Tsh 400 mpaka 750 kwa lita.. Na IDO kwa sasa lita moja inaenda mpaka 1800 kulingana na eneo

Ni nini kilitokea kwenye ajali husika? Niligusia laana ya dhuluma kama swali japo inaweza kuwa ajali isiyo na chembe ya mahusiano na hilo!

Biashara nyingi duniani hufanywa kupitia madalali.. Hata serikali zetu kwenye manunuzi yake zimeshaangukia mara nyingi tu kwenye mikono ya madalali!

Dalali ni mtu wa kati anayekusaidia kupata kitu kwa haraka unapokihitaji na hujui pa kukipata.. Wana uzuri wao na wana ubaya wao ila ukweli mmoja ni kwamba dalali hafahamu kitu kinaitwa huruma, ukimzingua anakuzingua twice!

Juzi kabla ya jana kuna mfanyabiashara alipata tenda ya kupeleka IDO nje ya nchi.. Na kwa kuanzia ilitakiwa walau lita laki moja.. Akawapa watu kazi na watu wakapeana connection mpaka mzigo ukapatikana maeneo ya Kigamboni kwenye kiwanda kimoja kinatengeneza hayo mafuta ya IDO kwa kutumia tairi

Kwahiyo siku ya kwanza baada ya connection kukamilika magari makubwa mawili (horse) yakafika mpaka eneo la kupakilia mzigo.. Lakini hapo hapo kuna mmoja kati yao akauza ramani kwa tajiri.. Tajiri akafika mpaka eneo husika akajua kumbe mzigo unapatikana hapa.. Halafu akawazingua watoa connection kwa kushusha bei ili biashara pengine ishindikane
Na kweli wazee wa connection wakashindwa hivyo kufika jioni biashara ikawa imekufa! Imagine watu walipoteza siku nzima hapo! Kesho yake mapema, majuzi sasa.. Tajiri akaenda mwenyewe penye mzigo na kupatania bei upya na akapakia mzigo kisha akasepa

Gari zile zikaenda mpaka dample la tipper pengine kuchakachua kidogo na ile inayopatikana kwenye tope la mabaki ya mafuta ya Tipper.. Ili pengine kukamilisha mzigo na kuongeza kafaida zaidi

Ni kwenye kuchanyanya huko ndio ajali ilitokea.. Unapochanganya kitu kizito na chepesi unahitaji kichanganyio kama mashine ya blender hivi ili upate kitu kimoja kinachofanana

Sasa imagine gari limebeba mafuta zaidi ya lita 30,000 yanayoweza kulipuka.. Kufanya chochote na haya mafuta kunahitaji tahadhari kubwa!

Ni katika mchakato wa kuyachanganya huko huko ndani ya tank mashine ikapiga shoti na kutokea mlipuko mkubwa
Gari iliyopata hiyo shida ni moja lakini ya pili ingeponaje kwenye mazingira kama hayo? Maana zilikuwa eneo moja zote! Je hakuna majeruhi? Vifo je?

Huko YouTube kuna online Tv inaitwa Tanganyika imeweka kichwa cha habari TAZAMA INATEKETEA na picha kubwa ya mlipuko! Nimeishia tu kucheka!

Nimemaliza!
 
Aya ya mwisho kuna jambo la ndani zaidi unalolijua hahaha!
Ukiangalia huku ni uwandani hakuna hata nyumba kakini ona habari yenyewe sasa..halafu ukitazama hakuna cha maana kilichoelezwa
JamiiForums-1707842856.jpg

Mwenye mzigo kakosa mzigo
Mwenye biashara yake mtaji umeyumba
Mwenye magari yake ni kilio ama kicheko kutegemeana na bima
Kuna watu wamekosa kazi hapo
Kuna hasara kubwa imetokea
Pengine kuna kesi ya kujibu
Vp kuhusu vifo au majeruhi?
Biashara kuanza upya itachukua muda
Mshana Jr..... hao wote waliohusika kwenye hiyo biashara naweza kuona, si watu wa mchezo. Maana wamegawana hasara, bora tukose wote. Uchunguzi utafanyika ukweli utajulikana, mpaka watu wanafikiria kugawana hasara ina maana ni manguli. Waliofariki kama tujuavyo marehemu ana haki. Watakaohusika kwenye uchunguzi huenda wakanufaika pande zote tatu/ vivyo hivyo majeruhi na wahanga wa wafiwa watasaidiwa.

Kuna biashara madalali wanakuwa ni matycoon lkn wanakuwa kama vivuli. Wataonekana tu dhulma itakapofanikiwa.
 
Wakati wa Ben tulidalaliwa radar... Jamaa walipiga ndefu mpaka tukaonewa huruma tukarudishiwa bakshish baada ya kitambo kirefu
Halafu tukadalaliwa kwenye kivuko.. Tukapigwa ndefu halafu kikawa kibovu kweli dalali hana roho (ya huruma)
Halafu tukadalaliwa kwenye ndege... Ngoja niishie hapa!
 
Hata mie nkikupa connection sitegemei unizunguke kwenye dili hile, na swaumu ilivyo kaliii.....nipe changu kabsaaaa...

Ila hii nchi yapo mambo yanafanyikaga kimaghumashi, lisipotokea tatizo maisha yanaenda ila likitokea la kutokea utasikia watuhumiwa watapandishwa kizimbani

anyway Pasaka baadhi wala wenyewee ....na Iddi twasherekea wote,
 
Kuna biashara madalali wanakuwa ni matycoon lkn wanakuwa kama vivuli. Wataonekana tu dhulma itakapofanikiwa.
Wakati wa Ben tulidalaliwa radar... Jamaa walipiga ndefu mpaka tukaonewa huruma tukarudishiwa bakshish baada ya kitambo kirefu
Halafu tukadalaliwa kwenye kivuko.. Tukapigwa ndefu halafu kikawa kibovu kweli dalali hana roho (ya huruma)
Halafu tukadalaliwa kwenye ndege... Ngoja niishie hapa!
Umeweka vema mkuu. 🤝
Kuna muda dalali anakuwa mtu wa jikoni/anapika kila kitu.
Anajiwekea 10% yake, alafu mzigo unawekwa anaona.
Unaambiwa katoe mzigo/alafu ule mzigo umeingia unauona mwingi tena?
Unapita hivi..
Kila hatua mpya, mashetani wapya.
Malaika walewale.
 
Umeweka vema mkuu.

Ule msemo wa mafuta na maji havichangamani una deadline? Exemption?
Wanafanya stirring kama kupekecha mtory vile au wanatumia zile mashine kama za bakery za kuchanganya ngano
Ukinunua pipa 20 za oil chafu huwezi kukosa pipa tatu zilizochakachuliwa

Oil chafu bora ni ile kutoka kwenye engine na ambayo haijachanyanywa na hydraulic.. Hydraulic ni ngumu kuwaka

Je unaijuaje oil chafu super
Kwa macho ni ngumu ila ukichovya karatasi na kuiwasha itatarika na sometimes utaona bubles .. Vil vile oil chafu iliyochanganywa na hydraulic ni nzito kuwaka
View attachment 2178623
 
Back
Top Bottom