Ni nini msimamo wa CUF katika haya?

October

JF-Expert Member
Oct 5, 2009
2,145
92
Nimekua nikifuatilia maoni mbalimbali katika Forum hii na vyombo vya habari nikawa sijapata jibu halisi kuhusiana na msimamo wa chama cha CUF ( ´chama cha wananchi´) katika mambo kadhaa yanayotokea katika taifa hili ambapo ningeomba wadau munieleweshe
1.Nini Kauli na Msimamo wa CUF katika waraka uliotolewa na Kanisa Katoliki?
2.Nini Kauli na Msimamo wa CUF katika waraka uliotolewa na Shura ya Maimamu?
3.Nini Maoni ya CUF na Msimamo wao kuhusiana na Kadhi?
4.Mwisho ni nini msimamo wa CUF katika dhana ya Tanzania kujiunga na OIC

Wadau ningependa kupata ufafanuzi wa haya ili nijue
 
Last edited:
Wewe msimamo wako ni upi kuhusu 1-4 kabla ya kutaka msimamo wa CUF?
 
labda uongezee Nini msimamo wa CUF kuhusu ubalozi wa Vatican hapa tanzania?
 
Wewe msimamo wako ni upi kuhusu 1-4 kabla ya kutaka msimamo wa CUF?

...Ndo maana ukakopi thread yangu almost one to One na Ku replace CUF na CHADEMA?

Shame on you can´t you be creative and create your own Thread? Ndo matatizo ya kusoma shule za ku-Desa
 
Mimi haya niliyajua . Tumesha ingiliwa sasa . CCM wanatuvuta mashati tusijadili issues hapa .
 
Msimamo wa CUF yote hayo yanahitaji kura ya maoni ,maana siasa ya Taifa kuhusiana na dini ,ni kuwa serikali haifungamani na dini au serikali haina dini ila waumini ndio walio huru kufuata dini waitakayo kama haitoshi wadini hao wafanye watakayo lakini wasivunje sheria za nchi ,OIC ni maamuzi ya kiserikali na yanaweza kujadilika iwapo CUF itakuwa serikalini kwa sasa CUF ipo neutral aidha linawezekana suala hilo liatumika au kutumiwa na CUF kisiasa katika kuikandamiza CCM.
 
Asalaam Aleikum, bwana asifiwe!
Wakuu zangu nakutahadhalisheni sana na hizi habari zenu za CUF na Chadema...
Kama wewe ni mwanachama wa CUF au Chadema nakuombeni sana muachane kabisa na maswala ya dini..
Kwa taarifa za ndani nilizopata, moja ya mkakati rahisi wa CCM ambao wameuweka kiporo hadi siku maalum ni kuutangazia Umma kwamba CUF ni chama cha Waislaam na Chadema ni chama cha Wakristu - inatisha!

Maneno hayo tu yatawavuruga wananchi na CCM ataibuka mshindi pasipo kuangalia viongozi wao ktk UFISADI..
Trust me, jamani niamini ktk hili moja tu...CCM wanasubiri wakati muafaka wa kutumia dhana hiyo na hakika wananchi wengi watawakimbien,Msifanye mchezo kabisa na nguvu ya imani za watu...Acheni kubeza dini za watu, acheni kubeza makabila wala jinsia za watu.. Definition ya mtu Primitive hutokana na cultural blindness thesis kama hizi..
Please wasaidieni vyama hivi vipate kujenga demokrasia ya kweli badala ya kuvibomoa kwa maelezo yasiyojenga..
 
Desturi ya watanzania atupendi kujituma,hii ni copy and paste without word Chadema.inachekesha sanaa.
 
Angalia Date and time Post ya CUF na CHADEMA ujue nani ali copy kwa nani
 
Back
Top Bottom