Ni nini maana ya Maisha Magumu.!!

Ni nini maana ya Maisha Magumu.!!

The Hunter

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2010
Posts
1,048
Reaction score
307
Huwa sielewi hasa mtu anaposema maisha magumu..hawa watu wanaosema maisha magumu hutumia kigezo gani hasa''
Mfano
Mfanyabiashara aliekuwa akienda kusomba manguo, simu na vifaa vingine feki toka china, asipoviuza hudai maisha magumu
Wezi wa bandarini, waliozoea kuchoropoa na kuiba mizigo ya wateja hivi leo baada ya kuja Mwakyembe na kuwasambaratisha ukikutana nao nao hudai maisha magumu
Wahandisi wababaishaji kama wale wa UDOM baada ya Magufuli kuwazibia hivi leo nao wanalia maisha magumu
Mwandishi wa habari Kanjanja akikosa kazi nae hudai maisha magumu
Matapeli hasa wanaojiita madalali ukikutana nao nao hudai maisha magumu
Magamba waliozoea kuiba mali za umma nao baada ya mambo kuwa tight hivi leo nao hulia maisha magumu
Machangudoa nao hulia maisha magumu, wenye bar na gesti bubu nao hawako nyuma kulia maisha magumu
Madogo walioko vyuoni wanaofaidika na kodi za watanzania nao hulia maisha magumu

So nisaidieni kujua maana ya nini MAISHA MAGUMU..
 
Mbona ushajijibu mwenyewe sa unataka jibu lipi tena?
 
There is great difference between fantasy and reality
 
Inaa maana hata wewe huyaoni kama magumu?
 
unaposhindwa kupata au kupata kwa shida mahitaji muhimu.nguo.makaz.chakula.elimu.kaz.umeme.maji.usafiri,mawasiliano, wewe ongeza ambayo unadhan yana patikana kwa shida kwako,majiran,ndungu na jamaa
 
Back
Top Bottom