Ni nini kitatokea katika hili? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni nini kitatokea katika hili?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Freetown, Apr 2, 2009.

 1. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2009
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Ni nini kitatokea katika hili? iwapo hawa wamiliki hawatapatikana au ndo Chenge atakuwa hana kesi ya kujibu??? na je wao imekuwaje wawe watuhumiwa wakati ndo waligongwa???. Au wameshapewa kitu na Vijisenti ili kesi ifungwe?? kama bima ilikwisha mda wake hiyo si chanzo cha hiyo ajali naomba kuelimishwa hapa JF

  Mmiliki, dereva wa bajaj aliyogonga Chenge utata

  2009-04-02 11:52:49
  Na Mashaka Mgeta


  Sakata la mahali walipo mmiliki na dereva wa bajaj iliyohusika katika ajali dhidi ya Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, bado ni kitendawili.

  Utata kuhusu mahali walipo Zuwena Nassor (mmiliki) na dereva ambaye jina lake halijajulikana, wote wakiwa ni watu muhimu katika kesi iliyofunguliwa dhidi ya Chenge, umethibitishwa na Jeshi la Polisi.

  Ajali hiyo ilisababisha vifo vya wanawake wawili, Beatrice Constantine na Victoria George.

  Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, aliiambia Nipashe jana kuwa upelelezi unaofanywa na jeshi hilo tangu kutokea ajali hiyo Machi 27, mwaka huu haujaweza kuwapata watu hao wawili.

  ``Inaonekana dhahiri kwamba mmiliki na dereva wa bajaj hiyo si watu wema, kwa maana tangu tulipotoa agizo la kuwataka wajisalimishe hawajajitokeza,``alisema.

  Kova alisema kuna ugumu wa kimazingira unaoweza kukwamisha zoezi la kuwasaka `watuhumiwa` hao ili wafikishwe katika mkondo wa sheria. Kwa mujibu wa Kova, miongoni mwa sababu za ugumu uliopo katika kuwakamata watu hao ni matumizi ya anwani zisizokuwa sahihi.

  Alisema kwa mujibu wa taarifa za awali kutoka mtandao wa polisi na Mamlaka ya Mapato (TRA), mmiliki wa bajaj hiyo anasadikiwa kutumia anwani isiyokuwa yake.

  ``Hili ni tatizo kwa Watanzania walio wengi, kwa mfano mtu anaweza kutumia anwani yetu, S.L.P 9040, kumbe ni kwa sababu palikuwa na ndugu yake hapa,`` alisema.

  Pia Kova alisema sababu nyingine zinaweza kuwa ukiukwaji wa taratibu za usajili na umilikishaji wa bajaji kwa upande mmoja ama uajiri wa dereva kwa upande mwingine.

  ``Kama kutakuwa na tatizo katika maeneo hayo, ni dhahiri kwamba watu hawa wataendelea kujificha kutokana na hofu kwamba watakapojitokeza, watafikishwa mahakamani kama Chenge,`` alisema.

  Hata hivyo, Kova alisema polisi inaendelea na uchunguzi ambao ni mapema kuweka siri zake hadharani, na kwamba hatima ya yote sheria itachukua mkondo wake dhidi ya wahusika.

  Naye Romana Mallya, anaripoti kuwa Kova alisema uchunguzi wa kipolisi wa ajali hiyo unaendelea ikiwa ni pamoja na kuifanyia kazi bima iliyodaiwa kumaliza muda wake.

  Alisema kwa hali hiyo, timu iliyoundwa kwa ajili uchunguzi wa `ajali ya Chenge`, bado haijatoa ripoti yake.

  ``Suala la bima linashughulikiwa pamoja na kwamba ametoa nyaraka zake, tunaangalia kama zipo sahihi,`` alisema

  Chenge ambaye alikuwa akitumia gari aina ya Toyota Pick Up Hilux yenye namba T 512 ACE, aliigonga bajaj yenye namba T 736 AXC na kusababisha vifo vya wanawake hao.

  Ajali hiyo ilitokea saa 10:00 alfajiri wakati Chenge akitokea njia panda, kati ya maeneo ya Kanisa la Mtakatifu Peter na Morogoro Store jijini Dar es Salaam.

  SOURCE: Nipashe
   
 2. FRANCIS DA DON

  FRANCIS DA DON JF-Expert Member

  #2
  Jun 1, 2016
  Joined: Sep 4, 2013
  Messages: 9,391
  Likes Received: 3,903
  Trophy Points: 280
  Haya naomba niwe wa kwanza kuchangia, hii kesi imefikia wapi, huyo Chegge ameshafungwa?
   
 3. FRANCIS DA DON

  FRANCIS DA DON JF-Expert Member

  #3
  Jun 1, 2016
  Joined: Sep 4, 2013
  Messages: 9,391
  Likes Received: 3,903
  Trophy Points: 280
  Seriously.., hii kesi imefikia wapi?! yaan hakuna anaejua?!
   
 4. MKWEPA KODI

  MKWEPA KODI JF-Expert Member

  #4
  Jun 1, 2016
  Joined: Nov 28, 2015
  Messages: 18,139
  Likes Received: 36,853
  Trophy Points: 280
  Nakumbuka chenge alipigwa faini ya shilingi milioni moja kama sijakosea
   
Loading...