Ni nini kinachoitafuna Zanzibar ndani ya NECTA? 10 baya la mwisho shule saba?

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,591
36,004
Kwa masikitiko makubwa naomba kuwauliza wenzetu wa Zanzibar swali ambalo kwa kweli limekuwa likinitatiza miaka mingi sana. Nalo ni udhaifu mkubwa sana wa taaluma ya Zanzibar ndani ya baraza la mitihani NECTA.

Cha ajabu kabisa ni kuwa, wakati Zanzibar hiyo ikiwa hoi mbele ya NECTA, wapo Wazanzibar wengi sana ambao ni wana vipaji vya hali ya juu sana mfano kina Mohamed Gharib Bilal na wengine wengi sana. Hawa wana vichwa vilivyojaa vipaji.

Katika matokeo ya kidato cha sita ACSEE-2016 Unguja pekee imetoa shule saba kati ya kumi za mwisho, nini tatizo?

Siongelei kuhusu swala la ghafla bin vuu shule kongwe za serikali za vipaji kurudi kwenye chati maana hilo linahitaji uchambuzi wake. Ni wachache watakaoamini kuwa shule zote kongwe za serikali za vipaji kurudi "top ten" kwa kishindo kumetokana na jitihada binafsi za wanafunzi. Shule zote nne? Hapana! Hili tutakuja kulichambua baadaye! Kwanza niwaulize hawa watani zetu, nini tena kimewapata?

Shule 10 zilizofanya vibaya:

1.Mpendae-Unguja
2.Ben Bella-Unguja
3.Tumekuja-Unguja
4.Green Bird Boys-Kilimanjaro
5.Jang'ombe-Unguja
6.Kiembe Samaki-Unguja
7.Tanzania Adventist-Arusha
8.Al- Ishan Girls-Unguja
9.Azania-Dar es Salaam
10.Lumumba-Unguja
 
Shule za vipvipaji za serikali zimekuwa zikifanya vizuri siku zote kwenye mitihani ya kidato cha sita unaweza kulinganisha na matokeo ya mwaka jana, juzi na hata miaka miwili iliyopita utaona shule kama kibaha, kisimiri, mzumbe, ilboru na tabora boys zimekuwa hazikosi top ten. Acha upotoshaji wa makusudi na kulalamika kwa kutumia sababu za udini bali wazanzibar waangalie wapi wamejikwaa warekebishe taifa hili ni letu sote
 
Kwa masikitiko makubwa naomba kuwauliza wenzetu wa Zanzibar swali ambalo kwa kweli limekuwa likinitatiza miaka mingi sana. Nalo ni udhaifu mkubwa sana wa taaluma ya Zanzibar ndani ya baraza la mitihani NECTA.

Cha ajabu kabisa ni kuwa, wakati Zanzibar hiyo ikiwa hoi mbele ya NECTA, wapo Wazanzibar wengi sana ambao ni wana vipaji vya hali ya juu sana mfano kina Mohamed Gharib Bilal na wengine wengi sana. Hawa wana vichwa vilivyojaa vipaji.

Katika matokeo ya kidato cha sita ACSEE-2016 Unguja pekee imetoa shule saba kati ya kumi za mwisho, nini tatizo?

Nalazimika kuyaandika haya kwani yamekuwa ni kama maji yaani siku zote ni wao tu. Hali hii ilipelekea hadi kuandamana na Joyce Ndalichako kulazimika kuondoka NECTA na ndipo walipopata walau kaunafuu. Lakini ghafla bin vuu hali imerudi ileile kwa kishindo. Nini tatizo?

Siongelei kuhusu swala la ghafla bin vuu shule kongwe za serikali za vipaji kurudi kwenye chati maana hilo linahitaji uchambuzi wake. Ni mpuuzi pekee ndiye atakayeamini kuwa shule zote kongwe za serikali za vipaji kurudi "top ten" kwa kishindo kumetokana na jitihada binafsi za wanafunzi. Shule zote nne? Hapana! Hili tutakuja kulichambua baadaye! Kwanza niwaulize hawa watani zetu, nini tena kimewapata?

Shule 10 zilizofanya vibaya:

1.Mpendae-Unguja
2.Ben Bella-Unguja
3.Tumekuja-Unguja
4.Green Bird Boys-Kilimanjaro
5.Jang'ombe-Unguja
6.Kiembe Samaki-Unguja
7.Tanzania Adventist-Arusha
8.Al- Ishan Girls-Unguja
9.Azania-Dar es Salaam
10.Lumumba-Unguja

Mohamed Said, FaizaFoxy

CCM ZANZIBAR NDIO WA KUJIBU....LABDA WAYAPENDA HAYA ...SI UNAJUA UKITAWALA WAJINGA ..TENA
 
Back
Top Bottom