Ni nini chanzo cha kukosa uaminifu

Fungo N.

JF-Expert Member
May 20, 2011
252
43
kutokuwa na uaminifu ktk ndoa au wapenzi ni janga la dunia hususani kwa wale walio ktk ndoa.lakini hivi ni kweli haya hufanywa kwa bahati mbaya?au ni shetani tu kama wengi wanavyodai?
 
Uongo ndio chanzo cha kupoteza
Uaminifu...
Haya mambo ya shetani na pombe
Sijui bangi mmhhh ni visingizio tuuu
 
No research - no wright to speak. Pombe ni sababu, kipato ni sababu, tamaa za mwili ni sababu, tamaa za vitu mbalimbali ni sababu. Utandawazi ni sababu, All in all Ni kasi ya Shetani kuangamiza watu wa Mungu. Akuna alofanya tendo hilo akamaliza na kujipongeza, huwa ni kujilaum. Ila tamaa ikiwaka tena unarudia. Ukitoka na magonjwa ni kuangaika kujitibu.
 
Kwanza kutkuwa mwaminifu ni uamuzi wa mtu kwa sababu ya tamaa za kmwili au tamaa za mali na vitu
kujiingiza kwenye vishawishi wenyewe na kukubali miili yetu tuongoze na pia kutokuwa na msimamo.
 
No research - no wright to speak. Pombe ni sababu, kipato ni sababu, tamaa za mwili ni sababu, tamaa za vitu mbalimbali ni sababu. Utandawazi ni sababu, All in all Ni kasi ya Shetani kuangamiza watu wa Mungu. Akuna alofanya tendo hilo akamaliza na kujipongeza, huwa ni kujilaum. Ila tamaa ikiwaka tena unarudia. Ukitoka na magonjwa ni kuangaika kujitibu.
MmhhhhhNaomba data zote, reference, za researchUlizofanya ..
 
Hapo kwenye red sipo,ila maelezo yako mengine uko sawa naungana na wewe.
No research - no wright to speak. Pombe ni sababu, kipato ni sababu, tamaa za mwili ni sababu, tamaa za vitu mbalimbali ni sababu. Utandawazi ni sababu, All in all Ni kasi ya Shetani kuangamiza watu wa Mungu. Akuna alofanya tendo hilo akamaliza na kujipongeza, huwa ni kujilaum. Ila tamaa ikiwaka tena unarudia. Ukitoka na magonjwa ni kuangaika kujitibu.
 
Tamaa ndo chanzo kikubwa..baadhi ya wanaume wanatamani wanawake tofauti tofauti..km anaye mfupi kesho atatamani mrefu..kesho aliejazia miguuni..wanawake nao ndo vle tna.
 
Dah, mi kuna wakati najiuliza kwa nini Mungu alituumbia hii miili yenye tamaa ya kukutana na jinsia ingine. Ukiwa hujaolewa ukafanya hio kitu ni dhambi, lkn ni mara chache sana utakuta mwanaume aliyekaa say miaka 30 bila kufanya hicho kitu mpaka akaoa. Kadhalika mwanamke. Mtu akioa halafu akatoka nje ya hiyo kingo nayo ni dhambi. Sasa kwa nn tuna miili ya hivi? Kuna watu kama kina Ibrahimu, Yakobo walizaa mpaka na wajakazi wa wake zao, Je na wao ilikuwa je? Mbona walikuwa wanaongea na Mungu.
 
Walaumu adam na eva hao ndo waliharibu kila kitu.

kutokujiamini km unapendwa/mpenz wako ni mwaminifu yawezakua ni tatizo kubwa sana ktk mahusiano!
 
No research - no wright to speak. Pombe ni sababu, kipato ni sababu, tamaa za mwili ni sababu, tamaa za vitu mbalimbali ni sababu. Utandawazi ni sababu, All in all Ni kasi ya Shetani kuangamiza watu wa Mungu. Akuna alofanya tendo hilo akamaliza na kujipongeza, huwa ni kujilaum. Ila tamaa ikiwaka tena unarudia. Ukitoka na magonjwa ni kuangaika kujitibu.

Hapo kwenye Nyekundu, ndo jibu kamili, jamaa baada ya kitendo, fikra zikirudi ndo....(Mbona hivi tena, kumbe hamna lolote la maana, kwani hata afadhali yule wangu nyumbani)
 
Back
Top Bottom