Ni nii maana ya chama cha upinzani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni nii maana ya chama cha upinzani?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Dingswayo, May 27, 2011.

 1. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #1
  May 27, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Katika siasa zetu za Tanzania, labda ni kwa sababu ya kuwa chini ya chama kimoja kwa muda mrefu, vyama vya upinzani vimekuwa vikionekana kuwa ni vyama vya uchochezi na kuleta vurugu. Kwa kifupi mtazamo ambao umekuwa ukitolewa na kuboreshwa kuwa ni vyama vya wasaliti.

  Mfumo wa vyama vingi umeingizwa nchini bila wananchi kufundishwa na kuelezwa kikamilifu maana halisi ya vyama vya upinzani na majukumu yake. Wakati wa chama kimoja, elimu ya jamii ilizingatiwa sana kwani ilikuwa ni chombo cha kuendeleza itikadi ya chama hicho. Elimu hiyo ya jamii ilitolewa kwa kutumia njia mbalimbali, mojawapo ya njia hizo ikiwa katika Elimu ya Watu Wazima. Tunaona kuwa baada ya kuingizwa mfumo wa vyama vingi, elimu hiyo kwa jamii haikupewa tena kipaumbele. Kukosekana kwa elimu hiyo ndio chanzo ch kuleta mkanganyiko huu tunaounna sasa, wa wananchi kutoolewa ni nini hasa maana ya chama cha upinzani na majukumu yake. Ndio maana leo tunaona ni jambo la kawaida viongozi wa vyama vya upinzani wakitupiana lawama na kulumbana wao kwa wao. Ni ajabu zaidi kusikia hata raisi wa nchi ambayo inatamka kwamba Tanzania ni nchi ya kidemokrasia, anatamka kuwa vyama ya upinzani ni vyama vya msimu!

  Jukumu kubwa la chama cha upinzani ni kuangalia kwa makini sera za chama tawala, na kuzipinga pale ipasapo, na kutoa mikakati na sera mbadala na kuwafahamisha wananchi kuhusu masuala yote ambayo yanahusu uendeswaji wa serikali.

  Kutokana na tafsiri hiyo, tunaona kwamba vyama vingi vya upinzani hapa Tanzania havitimizi majukumu yao ipaswavyo. Vinapoteza muda na malengo ya vyama vyao kwa kuanza kulumbana na wapinzani wenzao. Kwa kufanya hivyo, vinajidhoofisha vyenyewe.

  Ukosefu wa elimu ya uraia imetufanya wengi wetu kuingia katika malumbano ambayo yanafanya safari ya kuelekea demokrasia bora kuwa nyepesi. Kuna haja ya kuanziasha makakati wa kitaifa wa kutoa elimu ya uraia kwa wananchi. Jambo hili litafanyika kama serikali itakuwa na nia ya kuleta demokrasia ya kweli nchini.
   
 2. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #2
  May 27, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,182
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  Ulazima wa elimu ya uraia upo sana kwa mwananchi wa kawaida kuelewa dhana ya mfumo wa vyama vingi na umuhimu wake katika uendeshaji wa masuala ya kila siku ya serikali na sio ile maana ambayo ipo kwamba chama cha upinzani ni fujo, kupoteza amani na utulivu wa nchi, hawana sera au ni wapinzani wa kila kitu kumbe maana haswa sio hiyo bali ni waangaliaji wa kile kinachofanywa na serikali na penye mapungufu kukosoa
   
 3. Kiwi

  Kiwi JF-Expert Member

  #3
  May 27, 2011
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 1,009
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Uelewa mdogo ndio unaosababisha watu kama Mrema wa TLP kuipigia debe ccm na kuwaambia wanachama wake kuwa mchagueni Kikwete kuwa rais. Hiyo siyo kazi ya opposition party. Chama kimoja hakiwezi kukipigia debe chama kingine. Hiyo kama ni kwenye michezo kama mpira ni kosa la match-fixing. Na pia ni kosa kwa chama tawala kutamka hadharani kuwa vyama vya upinzani ni vyama vya msimu kama alivyowahi kutamka jk. Wakumbuke kuwa kwenye demokrasia ya kweli na iliyokomaa, kila chama kinaweza kuwa chama tawala au chama cha upinzani. Leo ccm wako madarakani, kuna siku wanaweza kuwa opposition, sasa tukubali kuwa ni chama cha msimu? Mfano Marekani, kuna vipindi Republican wanakuwa chama tawala, kuna kipindi Democrats wanakuwa chama tawala. Kila kimoja kinapokuwa kwenye upinzani kinakuwa na kazi ya kukikosoa chama kilicho madarakani ili kukipa changamoto katika kufanya kazi vizuri. Na mwisho wa muda wao wapiga kura wanafanya uamuzi wao kutokana na mafanikio ama kushindwa kwa chama kilichokuwa madarakani kutimiza yale iliyokusudia kuyafanya. Kukikashifu chama cha upinzani ni sawa na kukitemea mate kioo unapojitazama na kuona huipendi sura yako. Kioo kinakuonyesha hali halisi ilivyo, kukitemea mate ama kukivunja hakutasaidia. CDM inachofanya ni kuwaelimisha watu yale ambayo yanatokea na kuwapa elimu ya uraia ili wafahamu haki zao, na waweze kuikosoa serikali na chama tawala ipasavyo. Ndiyo kazi ya opposition party. ccm kama na wao wataweza kuwa kwenye opposition, hiyo ndiyo itakuwa kazi yao. Ukiona opposition party inapigia debe chama tawala ujue kuna walakin. Hata kwenye nchi zenye katiba inayokubali serikali ya mseto kama ilivyo Uingereza sasa hivi, Liberal Democrats na Conservatives wako kwenye serikali, na Labour wako opposition. Huwezi kusikia Labour wanakipigia debe Conservatives wala kuipamba serikali iliyoko madarakani ikivurunda kwa kisingizio chochote kile. Kazi yao kama opposition party ni kuikosoa serikali na kuonyesha wapiga kura mapungufu yoyote ya serikali ya chama au vyama tawala. Wasipofanya hivyo ni kushindwa kazi ya opposition. Wale wote wanaoiogopa CDM wana hila zao. Waende shule. Waachane na semina endelezi maana zinawapumbaza!
   
 4. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #4
  May 27, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,182
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280

  Umeongea la maana sana mkuu
  Ila dhana nzima ya opposition party kwa wengi bado haijaeleweka na ndo maana hapo juu nikasema propagada zinazosambazwa na magazeti na redia na tv au tuseme vyombo vya habari ni kuwa upinzani ni vita upinzani ni kuiondoa amani na utulivu wa watanzania upinzani ni kuandamana na wapinzania hawana sera wanataka kuingia ikulu kwa nguvu. Kumbe kinachofanyika kwa sasa ni elimu ya uraia elimu ya kuwasaidia wananchi waelewe kuwa wana haki kuuliza ahadi za watawala ziko wapi, elimu ya kuwaambia kuwa wana rasilimali hawapaswi kulia umaskini, elimu ya kuwaambia haki zao za kiraia na za msingi na kuelewa wajibu wa viongozi waliowachagua katika kuhakikisha maendeleo yao na wajibu wa viongozi kuwa nao katika kuhakikisha wanapambana na kila aina ya umaskini wao.
  Dhana ya chama kimoja cha siasa ambacho wala sio chama tawala kukipinga chama kingine ni dhana mpya kwa tanzania maana inaonekana vyama vinaanzishwa si kwa malengo ya kupambana na chama tawala ili kuweza kuleta changamoto mpya na kukifanya chama tawala kisilale bali ni vyenyewe kwa vyenyewe kupambana huku mtaani na kupakana matope. Vinapopambana vyenyewe kwa vyenyewe vinakipa chama tawala kupata upenyo wa kuendelea kutawala na kupata hoja ya kuvisema na hata chama tawala kisipotekeleza sera zake kunakuwa hakuna chama mbadala cha kuwaambia wananchi mapungufu ya chama tawala
  Ndo maana nasema elimu ya uraia ni muhimu sana katika kuhakikisha kuwa dhana nzima ya chama tawala na chama cha upinzani inaeleweka na nini umuhimu wa kuwepo kw achama cha upinzani katika kuhakikisha kuwa chama tawala kinawajibika kutekeleza sera zake
   
Loading...