Ni ngumu kuwaelewa wanaume!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni ngumu kuwaelewa wanaume!!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Lizzy, Dec 14, 2010.

 1. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #1
  Dec 14, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Haipiti wiki bila kusikia jinsi wanawake tulivyo viumbe vya ajabu!!Hatueleweki...tunasema hili tukimaanisha lile...tunafanya hili wakati tunataka lile, yani hatuna moja.

  Ila ukweli ni kwamba linapokuja swala la mapenzi na mahusiano WANAUME ndio wasioeleweka.Unakuta mtu anakupenda ila matendo yake hayaonyeshi kabisa hayo....hamna kuonyesha kujali wala nini!Na sio kwamba hataki ila hajui jinsi au umuhimu wakufanya hivyo.Hapo hujakutana na asiyekupenda ila mwenye matendo yanayoashiria hivyo.

  Kusema ukweli ni rahisi sana kugundua kama mwanamke(wengi sio wote...wengine ni wasanii) anakupenda/kukujali kweli maana ni ngumu kwa mwanamke kuficha/kutokuonyesha hisia zake za ukweli mkiwa tayari kwenye mahusiano!Kwahiyo kina kaka kama unampenda mtu jitahidini kuonyesha kwa uwazi maana ni rahisi sana kuwasoma VISIVYO.....kumbuka IF YOU ARE GOOD TO US, WE WILL BE THE BEST THING THAT EVER HAPPENED TO YOU.:hug:TUNAWAPENDA SANA!!!
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Dec 14, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Mimi nadhani ni haki zaidi kusema binadamu ni viumbe wa ajabu! Hatueleweki...tunasema hili tukimaanisha lile...tunafanya hili wakati tunataka lile, yaani hatuna moja.

  Na uthibitisho wa kuwa sisi binadamu hatueleweki ni hizo lawama tutupianazo baina yetu. Tunapenda sana kunyooshea wengine vidole hata kwa yale mapungufu tuliyonayo kwa wingi.

  Mimi nishawahi kushuhudia jamaa mmoja hivi kwenye klabu ya pombe za kienyeji akimsema jamaa mwingine kwa ulevi wake wakati yeye mwenyewe kila siku hakosi kunywa dengerua.

  Pia nishawahi kumsikia changudoa mmoja akimteta changudoa mwenzake eti ni malaya. Sasa jiulize mwenyewe hapo kama sisi binadamu si viumbe wa ajabu!

  Mara nyingi huwa ni "fulani" na sio "wewe" au "mimi".....
   
 3. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #3
  Dec 14, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hhahahahha....asante!!Hapo kwa mlevi na dada poa pamenifurahisha!!
  Newayz hali iko pande zote ndio maana sikusema wanawake wote wanaeleweka ila nimeegemea zaidi kwa wakaka kwasababu ndo wagumu kuji-express kwenye mapenzi!!Sio maisha kwa ujumla!!!
   
 4. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #4
  Dec 14, 2010
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,807
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Ni kweli sana na nakubaliana na wewe kuwa wanawake wengi wapo very expressive na honesty! ( ofcse sio wote!), big up women out there! we love you![​IMG]
   
 5. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #5
  Dec 14, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Asante!!Ila we mchoyoo wa THANKS!!heheh
   
 6. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #6
  Dec 14, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  mmmmhhh kwakweli kama wote tungekuwa tunakubaliana hivi ..
  the world will be a much better place...
   
 7. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #7
  Dec 14, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  mmmhhh asante sana Lizzy..kwa kujitoa mhanga kihasi hiki...
  ni kweli niliona poster nyigi sana kuhusu hawa ngugu zetu wa kiume wakitulalamikia sana..
  asante kwa kusimama na kutetea wanawake ....
  Big Up For Lizzy...
   
 8. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #8
  Dec 14, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Asante mpnz...tuko pamoja!
   
 9. Yegomasika

  Yegomasika JF-Expert Member

  #9
  Dec 14, 2010
  Joined: Mar 21, 2009
  Messages: 7,140
  Likes Received: 23,808
  Trophy Points: 280
  Utakuwa umeangalia kipindi cha today show NBC leo asubuhi ehe~walikuwa wanaongelea kitu hii!.
   
 10. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #10
  Dec 14, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Huhhhhh??Okeyyy!Ila sijaona nimeongea kutokana na experience!!
   
 11. Yegomasika

  Yegomasika JF-Expert Member

  #11
  Dec 14, 2010
  Joined: Mar 21, 2009
  Messages: 7,140
  Likes Received: 23,808
  Trophy Points: 280
  Mmh basi kanunue gazeti la Cosmopolitan toleo la mwezi huu, kuna special article kuhusu tofauti kubwa ya maamuzi iliyopo kati ya wanaume na wanawake.
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Dec 14, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Wanaume tunaeleweka sana. Na umeonesha jinsi gani mnatuelewa-kwamba hatueleweki! Lakini kwamba wanawake ni mafumbo yasiyotegukika bado ni kweli.
   
 13. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #13
  Dec 14, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  wanawake wanakwenda na emotions ndo maana ni ngumu kuwaelewa....i mean mwanamke anaweza sema hapendi watu wafupi but akikutana na mtu mfupiatakaemfanya ajisikie special,hisia zinabadilika,na taratibu anaanza kumpenda huyo mfupi..wanaume sio emotional.ni practical zaidi....kwa hiyo ni kweli ignore what a woman say....watch her actions ndo utamuelewa....
   
 14. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #14
  Dec 14, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  lizzy nimependa sana hiyo ya kumwambia mpenzi wako...you are the best thing ever happened to me....i do that everyday.............
   
 15. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #15
  Dec 14, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  teh teh teh khaaaaa :ranger:
   
 16. F

  Ferds JF-Expert Member

  #16
  Dec 14, 2010
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 1,267
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  kama ni hivyo basi nitayafanyia kazi hayo kwa "mama ferds"................. asante kwa useful post.....respect mamaa
   
 17. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #17
  Dec 14, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hapo sasa ndio tunapogongana.....wanaume wakati mwingine unakuta matendo yenu hayaendani kabisa na hisia zenu!!
  Asante Boss:A S crown-1:
   
 18. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #18
  Dec 14, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Sasa chakuchekesha nini Kimbweka???:focus:
   
 19. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #19
  Dec 14, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kweli Boss....inamwongezea mwenzio raha!!!
   
 20. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #20
  Dec 14, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Tupe point mbili tatu basi.....binafsi hua sisomi hayo magazeti!!!:redfaces:
   
Loading...