Ni nani yuko nyuma ya BBC Swahili?

Ni nani yuko nyuma ya BBC Swahili?

kudamademede

Member
Joined
Jan 1, 2020
Posts
62
Reaction score
241
NANI YUKO NYUMA YA BBC SWAHILI?

Kama tunavyofahamu wote kuwa BBC Swahili ni chombo cha habari kinachoripoti habari za ulimwengu wa njia ya Kiswahili ambayo ni lugha ya Taifa letu Tanzania.

Kwa muda mrefu sasa chombo hiki kimekuwa kikiripoti taarifa zinazotokea ndani ya nchi kwa njia inayoleta ukakasi kwa watanzania hasa wazalendo wa nchi yetu pendwa Tanzania.

Dunia nzima ilikumbwa na janga la homa ya mapafu COVID-19 ambayo imekuwa gumzo duniani kote ikipelekea maisha ya watu kubadilika na tabia mpya kuzaliwa.

Katika kupambana na janga hili lililotishia sana maisha ya watu, Wizara ya Afya iliyochukua tahadhari zote kama zilivyoelekezwa na wataalamu mbalimbali wa afya ndani na nje ya nchi. Jitihada hizi kwa mara nyingi zilibezwa na kuhujumiwa kupitia chombo cha habari cha BBC Swahili kwa kuripoti habari zenye kutia hofu watanzania na kukosoa utendaji kazi wa wizara ya afya hapa nchini.

HII INAPELEKEA KUHOJI NI NANI YUKO NYUMA YA BBC SWAHILI

Ni kweli kwamba hamna anayewapangia BBC Swahili waripoti nini, lakini pia wajue tuna ruhusa ya kuhoji wanachoripoti hasa kama kina maslahi na nchi yetu.

Kuna mambo mengi yaliyofanywa na Rais wa Tanzania mheshimiwa John Magufuli kwa kipindi cha miaka mitano ya muhula wake wa kwa za wa urais; chombo hiki kimekinga mgongo kutoongelea mambo haya kabisa huku kikiwa mstari wa mbele kuwapa nafasi wale wanaoonesha nia ya kuikosoa na kupinga serikali ya Tanzania pamoja na utawala wa rais Magufuli.

Wakati huu ambao vuguvugu la uchaguzi linaendelea kupanda na kila kona gumzo kuu ikiwa ni uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020, yameonekana matukio mengine ambayo sio ya kufumbia macho hasa kutokana na sintofahamu kwamba chombo cha habari cha BBC Swahili kinafanya vitu hivi kwa ajili ya kumnufaisha nani hasa.

Katika kipindi ambacho Tanzania imekuwa kwenye mapambano na janga la COVID-19, muhubiri mmoja hala nchini mwenye maelfu ya wafuasi ambaye ni mwanzilishi na msimamizi wa makanisa ya Ufufuo na Uzima duniani kote, Askofu Josephat Gwajima alikuwa mstari wa mbele akitoa elimu kwenye jamii kupitia vipindi vya ibada kanisani kwake.

Siku ya Jumapili tarehe 05.07.2020 BBC Swahili kupitia ukurasa wao wa Twitter walichapisha habari inayolenga kukanusha kile Askofu Gwajima alichosema kuhusu hatari ya mionzi ya 5G na jinsi unavyoathiri afya ya seli katika mwili wa binadamu.

Leo tena tarehe 10.07.2020 BBC Swahili imechapisha taarifa ya kuondolewa kwa ujumbe unaofanana na huo kwenye ukurasa wa Instagram wa Askofu Gwajima. Hii bila shaka ni kuijulisha dunia mafanikio ya jitihada zake za kutaka kile alichokiongea Askofu Gwajima kisisikike kwa watu duniani kote.

Ikumbukwe kuwa Askofu Gwajima ni mtia nia wa kiti cha Ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi CCM katika jimbo la Kawe- Dar es Salaam. Hii imezua sintofahamu kwa maelfu ya watu nje na ndani ya nchi wanaompenda na kumfuatilia Askofu Gwajima huku wakiamini ni mtu ambaye amejitoa sana katika kipindi kigumu cha janga la Corona hasa ukizingatia hofu iliyokuwa imetanda.

HII IMEPELEKEA KUHOJI TENA; NANI ALIYE NYUMA YA BBC SWAHILI?

Je, kuna mtu ndani ya Tanzania ambaye anawaza kufanya hivyo kutomchafua Askofu Gwajima na kuondoa imani kubwa iliyo kwa wananchi juu yake?

Je, BBC mliwezaje kufahamu kuwa ujumbe umefutwa kwenye ukurasa wa Instagram? Hii inaleta maana kwamba jitihada zote za kuondoa ujumbe huo zimefanywa nanyi. Nani hasa anawatuma au anawaomba kufanya hivyo.

Je, vyama vya upinzani ndio vinafanya jambo hili? Kwanini BBC Swahili mtumike kisiasa katika jambo hili?

Je, hamuoni wafuasi wenu wanafatilia taarifa kwenye kurasa zenu watapunguza mapenzi nanyi hasa ukizingatia kuwa wapo watu wengi ambao wasingependa kabisa Askofu Gwajima aonewe?

Je, hamuoni kuwa mnachofanya ni shambulio binafsi ambapo chombo cha kimataifa kama BBC Swahili kufanya hivyo ni kushusha hadhi yenu na kutia doa ubora wa taaifa zenu?

Ikumbukwe watu wenye uhusiano wa moja kwa moja na BBC Swahili wanajulikana na tungependa serikali iwachunguze na kuangalia mahusiano yake na jambo hili. Hatutakubali hujuma za aina yeyote kwenye nchi yetu.

Kuona mabaya tu ya nchi na ukatafumbia macho mazuri ya yanayofanyika kila siku ni ujumbe wa aina yake kuonesha uadui wa kimaslahi au kutumiwa na mtu au kundi lenye chuki binafsi.

USHAURI WANGU

Endeleeni kuripoti habari zenye kujenga na kuelimisha. Acheni taarifa zenye mashambulio binafsi kwa mtu. Hii kamwe haitawajenga, kumbuka BBC ni taasisi, hii chuki itaota mpaka ndani ya taasisi.

Mzalendo
Mwl James Katunga
 
The fear of unknown inakusumbua.

Yaani yeyote anapotoa maoni kinzani na serikali anakuwa anatumiwa? Kuna kuwa na "mtu fulani nyuma yake?"

Yaani unataka kila mtu, kila chombo cha habari kiimbe propaganda zenu na za Magufuli?

Wengine wana akili na siyo "ndege kasuku" anayeiga kila sauti na kupokea tu bila kujiuliza maswali kwa kila kisemwacho na watawala waovu.

Ukisema upendalo watu wasikie, ni lazima waende kuchunguza na upande wa pili kuna nini. Hicho ndicho msichotaka kukisikia. Lakini mpende msipende, lazima msikie tu.

Kwanini mnaogopa na kuanza kukimbia mpaka vivuli vyenu nyie?
 
kudamademede,

Kazi ya BBC ni kuandika habari mbaya na chafu pamoja na Propaganda za kuichafua Tanzania walio nyuma hivi sasa ni Zito Kabwe pamoja na Toto Tundu Lisu. wamefungua kituo kikubwa sana cha BBC Kiswaahili service Kenya. Dawa yao ni kuinua uchumi wetu hadi wakajinyonge. JPM anafanya hayo hivi sasa na wanahaha wamfanye nini. Tuwalinde viongozi wetu kwa udi na uvumba. Ngoja huyu balozi wao aje apewe za uso.
 
Hii ni baadhi tu ya watu waliojawa na wivu ndani yao na wasiopenda kuona wengine wakionekana kuwa juu zaidi.

Hiyo kufuta ule uelimishaji kuhusu 5G alioelezea mchungaji gwajima ni dhahiri kwamba wapo watu ambao wako nyuma ya pazia wanajaribu kujificha nyuma ya BBC ili wasifahamike maana wanajua kile wanachokifuta ni cha kweli.

Hivo hawataki isambae kote kwa sababu ya huo wivu uliowajaa.
 
Dawa yao ni kuinua uchumi wetu hadi wakajinyonge.

Muache sasa kutuingizia hasara kama Taifa kwa kupoteza silaha bure, imagine risasi 38 zilipotea huku Lissu hajafa. Tumie hiyo silaha ya kuinua Uchumi. Sasa umefika Uchumi wa chini kati, nina imani ukifika Uchumi wa chini juu. Hawa vibaraka watajinyonga kabisa.
 
kudamademede,

Mzalendo James unawapangia BBC waongee kile anachopenda kukisikia pekee? Huo ndiyo uzalendo? Wananchi wapi unawasemea? au unamsemea Gwajima lakini umetumia mgongo wa Serikali ya Naibu Rais Bashite na mtukufu? Ukitaka BBC wakufurahishe wambie ndugu zako CCM waache Tabia mbaya ya kuwanyanyasa kuwadhoofisha kuwahujumu kuwabambikia kesi kuwapiga risasi wapinzani, hata ufanye mazuri vipi lakini ukifanya mabaya uonevu uovu kwa wapinzani mazuri yako yote yanafutika yanaonekana yale mabaya pekee, BBC siyo TBC Tv yenu ya CCM hicho ni chombo huru cha kimataifa hakichuji habari kinatoa mapungufu yote kwa uwazi acheni kuwazuia BBC kuripoti udhaifu wenu.
 
The fear of unknown inakusumbua.

Yaani yeyote anapotoa maoni kinzani na serikali anakuwa anatumiwa? Kuna kuwa na "mtu fulani nyuma yake?"

Yaani unataka kila mtu, kila chombo cha habari kiimbe propaganda zenu na za Magufuli?

Wengine wana akili na siyo "ndege kasuku" anayeiga kila sauti na kupokea tu bila kujiuliza maswali kwa kila kisemwacho na watawala waovu.

Ukisema upendalo watu wasikie, ni lazima waende kuchunguza na upande wa pili kuna nini. Hicho ndicho msichotaka kukisikia. Lakini mpende msipende, lazima msikie tu.

Kwanini mnaogopa na kuanza kukimbia mpaka vivuli vyenu nyie?
Wanataka BBC ifanye kazi kama TBCCM Yaani BBCCM
 
Natamani hii channel ingefungiwa airtime Tanzania. Huyo Kikeke atafute uraia huko kwa wakoloni
 
Natamani hii channel ingefungiwa airtime Tanzania. Huyo Kikeke atafute uraia huko kwa wakoloni
Huu ndiyo ujinga uliojaa huko CCM Yaani badala ya kuwakataza CCM waache uonevu uovu unyanyasaji kwa wapinzani unapanga njama za kumhujumu mtangazaji anayetumwa kufanya kazi na chombo huru cha habari za kimataifa.
 
BBC ni chombo cha kufikishia watu habari lakini haipelekei wao kufanya tu vile wanavyopenda na lazima wazingatie kanuni zao
BBC wapo huru siyo kama TBC ambayo sasa ni TBCCM ambao wanataka BBC iwe Tawi la CCM ijulikane kama BBCCCM .
 
huu uzi umejaa uchamaa wakati maendeleo hayana chama

Sent from my SM-G9250 using JamiiForums mobile app
Yatosha tu kusema kaandika mwalimu mkuda. Reasoning capacity sifuri. Anakiri mabaya yapo. Hataki yasemwe na BBC bali yasemwe mazuri tu. TBC inaimba usiku na mchana mazuri na sifa kedekede hata za kubumba, hilo halioni! Njia rahisi na ya uhakika kama hutaki mabaya yako yasemwe ni kutoyafanya. Hakuna atakayesema kisichokuwepo. Utakuwa uongo. Mwalimu wa sampuli hii ni wa kukimbiwa kama corona. Anafundisha ujinga!
 
Kazi ya BBC ni kuandika habari mbaya na chafu pamoja na Propaganda za kuichafua Tanzania walio nyuma hivi sasa ni Zito Kabwe pamoja na Toto Tundu Lisu. wamefungua kituo kikubwa sana cha BBC Kiswaahili service Kenya. Dawa yao ni kuinua uchumi wetu hadi wakajinyonge. JPM anafanya hayo hivi sasa na wanahaha wamfanye nini. Tuwalinde viongozi wetu kwa udi na uvumba. Ngoja huyu balozi wao aje apewe za uso.
Kuichafua Tanzania kivipi? Habari mbaya chafu zipi? Kwani CCM hawawapori ushindi wapinzani? CCM hawaibi kura? CCM hawahujumu kuwadhoofisha kuwabambikia kesi kuwapiga risasi wapinzani? Kama mnataka habari nzuri msifiwe na BBC acheni kuwanyanyasa wapinzani ishi na wapinzani bila kuwabambikia kesi kuwaonea kuwafanyia visa vya kila aina, msitake BBC ifanye kazi kama TBCCCM yenu.
 
Back
Top Bottom